green29
JF-Expert Member
- Jul 4, 2007
- 311
- 41
Shikamoo,
Mimi Mike,.... waliniuliza kwanini najihusisha na siasa na sisomi, nikawambia ilikuwa ni mwanzoni na sasa nasoma niko shule na jf sijihusishi sana.
Asanteni nyote kwa uhshirikiano
Pole sana Mike! Yes ni katika maisha kuna mitihaani mingi sana. Lakini wakati mwingine unapopata adha kwa kuwapigania wanyonge na kusimamia haki hakuna sababu ya kujilaumu.
Nakubaliana na ukweli kuwa JF kama jamii ya watu tunaoipenda nchi yetu na watanzania wenzetu hatupotez muda humu ndani sababu ya kutaka kumdhalilisha mtu na wala hatuungi mkono ugaidi, uchochezi wala kudhalilishana. Tunachofanya ni kutoa sauti kwa niaba ya watanzania wote. Sauti za wanyonge. Watanzania wanaoishi katika mazingira magumu wakati viongozi waliokuwa na jukumu la kuwakomboa wameelekeza interst katika biashara zao binafsi. Kwa upande mwingine tunaisiadia serikali na Mhemshimiwa Rais katika kuijenga nchi. Rais JK katika hotuba yake iliyopita alisisitiza umuhimu wa maadili ya viongozi na kuheshimu kazi zao badala ya kutanguliza maslahi ya biashara binafsi. Uki-summarize mambo mengi yaliyomo ndani ya JF utakuta kuwa ujumbe mkubwa ni huo huo wa kudai discipline ya viongozi kwa maslahi ya taifa.
Hongera sana kwa kuipenda nchi yako. Nawaweka katika list moja na Chief Mkwawa, Mirambo, Isike, Kimweri,Mangis, Mac, Mike, Mwanakijiji, na wengine!
Nakutakia masomo mema mkuu.