Ahsante serikali ya CCM kwa kutuondolea kero hizi

Sasa hivi maisha ni mtelezo tu.
Dola ziko za kutosha.
Sukari hadi inamwagika.
Umeme ndo usiseme kabisa..
Gharama za masisha kwa watu ziko chini kuliko muda wowote katika historia yetu!
 
Jifunze kwanza Hati mkato na Kuandika Ndo uwe #Pusher mkuu....

Ukishajua kuandika Vizuri Ruksa kupush Tag mkuu..
MWandiko Mbaya sana mkuu..
Na mkuu sukari umenunua wapi 1200 kwa kilo..

Huo mwaka gani unauzungumzia Mwaka 2001 au ?

Ukiwa Hastag Pusher Jifunze kuwa na Aibu pia
Ndio maana nilisema wenye akili ndio watakao nielewa hila mtu kama wewe huwezi kuelewa upeo wako wa kufikiri bado upo chini wenye upeo mkubwa wamenielewa nini nime amanisha
 
Kuishi kwa shemeji na tena kwa muda mrefu ndiyo husababisha wewe kuwa na akili mgando kama hizi. Yaani shemeji yako anapogharamia umeme wa jenereta, wewe unaona kuwa tatizo la mgao wa umeme limekwisha, na pale dada yako anapobinya bajeti ya familia na kukupa wewe fedha, basi unaona maisha umeyapatia na wala hakuna tatizo la ajira.
Kweli nimekubari watanzania uwezo wa kufikiri mdogo sana yani kwa mtazamo wako unaona hayo maneno nilio ya andika nime amanisha mbona mwenzenu kanielewa nyinyi mnashindwaje kunielewa
 
Wewe unagombea uwenyekiti wa mtaa au kitongoji?

Umezunguka nchi nzima ukaona kero za wananchi jinsi wanavyoteseka au wewe ni wale wa ndiyooooo.

Vijijini hatuna barabara za kupitisha mazao yetu kwenda kwenye masoko unasema CCM imefanya mengi??
Watu hatuna waganga kwenye zahanati zilizojengwa wewe unasema kila kitu bwerere??? Kama umetumwa basi kaandike kwenye mitandao nyingine siyo JF.
Jifunze kufikiri ukifikiri vizuri nilicho andika usingesema hayo maneno mimi najua vizuri shida tunazo zipata nime andika hivyo hili machawa wafurahi lakini hakuna hata chawa alio nisapoti wamejua kama na kejeri ndio maana hawaja nisapoti
 
Mkuu mwenye Hekima kwanza Hukubali kwamba alikosea...
mwanzoni ulibananisha sana Herufi na maneno Na hukuacha nafasi ya aya wala Hakukuwa na Nukta..

Japo baadaye ulifanimisha kuweka Nakushukuru kwa hilo..

It was Sarcasm..


Kuhusu Ulichoandika Mwanzoni sikukielewa ila niliporudi tena kusoma nikagundua ulikuwa na maana gani na Kweli kabisa umeandika sahihi..
Na Nchi tunakoelekea Tutaipoteza kabisa
Nashukuru na ahsante kwa kunielewa
 
Sasa hivi maisha ni mtelezo tu.
Dola ziko za kutosha.
Sukari hadi inamwagika.
Umeme ndo usiseme kabisa..
Gharama za masisha kwa watu ziko chini kuliko muda wowote katika historia yetu!
Nashukuru umenielewa yani maneno haya hata machawa wanaopenda kusifia hawawezi kuku sapoti wanajua kabisa kama una wakejeri
 
Back
Top Bottom