Ahmed Ally unapowaambia watu ikifika saa sita waache kazi waende uwanjani, wakifukuzwa kazi familia zao utazilisha wewe?

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,737
Nimesikitika sana kuona kijana msomi (Ahmedy Ally) Msemaji wa Simba sc katika mkutano na waandishi wa habari akizungumza maneno ya hovyo Tena yasiyo kuwa na mashiko katika ukuaji wa uchumi.

Serikali inapambana watu wafanye kazi uchumi ukue lakini anatokea mtu mmoja katika Taifa hili kukwamisha juhudi za serikali kwa kuwaambia watu

"ikifika saa sita acha kazi njoo uwanjani na boss asipokupa ruhusa tuambie tutajua namna gani ya kuzungumza nae/kufanya"

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili kumuuliza Ahmedy Ally hivi anajua namna gani watu wanavyopambana kupata kazi??

Hivi wewe Ahmedy Ally una akili sawa sawa kweli watu wakifukuzwa kazi/kwa sababu ya Simba au maneno yako ya kujifurahisha Familia zao utazilisha??

Hata Haji Manara alikua Juha pale Simba lakini Akuwahi kuthubutu kutamka maneno ya kijinga Kama haya maneno ambayo Kama watu watayafuata Basi uchumi wa nchi utashuka maana watakua hawana kazi na kutapelekea wimbi la watu tegemezi.

Maoni Yangu: Ahmedy Ally anapaswa kutakari kabla ya kuropoka Wanasimba walitegemea kuwa wamepata kijana smart kiakili baada ya Haji Manara lakini bwana mdogo anakua Juha kumzid Hajji Manara.

MICHEZO ITUMIKE KUHAMASISHA WATU WAFANYE KAZI NA SIYO KUTUMIKA KATIKA KUDIDIMIZA UCHUMI.
 
Nimesikitika sana kuona kijana msomi (Ahmedy Ally) Msemaji wa Simba sc katika mkutano na waandishi wa habari akizungumza maneno ya hovyo Tena yasiyo kuwa na mashiko katika ukuaji wa uchumi.
Kwan kweli ulichukulia serious!??
Vipi anavyosemaga Simba ikishinda jmosi mapumziko ni hadi jtatu ni kweli huwa watu hawaendi kazini kisa simba imeshinda?

Sometimes nyuzi za aibu zinaanzishwa tu humu.
Tujaribu kutumia hekima,, tusijiexpose kwa watu namna tulivyo.
 
Nimesikitika sana kuona kijana msomi (Ahmedy Ally) Msemaji wa Simba sc katika mkutano na waandishi wa habari akizungumza maneno ya hovyo Tena yasiyo kuwa na mashiko katika ukuaji wa uchumi.
Yuko sahihi hiyo ni kazi yake, na wewe waambie watu waache kazi zao waje kwenye kazi yako.
 
Kwan kweli ulichukulia serious!??
Vipi anavyosemaga Simba ikishinda jmosi mapumziko ni hadi jtatu ni kweli huwa watu hawaendi kazini kisa simba imeshinda?

Sometimes nyuzi za aibu zinaanzishwa tu humu.
Tujaribu kutumia hekima,, tusijiexpose kwa watu namna tulivyo.
MZEE HIVI UNAJUA KILA MTU ANA AKILI KAMA ZAKO WEWE??

KUNA WATU WANAAMINI KULIKO WEWE UNAVYOFIKIRI WEWE.

KAMA ALIKUA ANATANIA ANGESEMA (JOKES) WATU WANGEMUELEWA

NJOO USWAZI UONE WATU WANAVYOWAAMINI WATU WANAOONGEA KWENYE REDIO/MBELE YA CAMERAS

PUNGUZA UJUAJI NA UJENGE HOJA
 
Ni kweli angesema ni utani tu

Kwa jinsi rage alivyosemaga nahis inaweza leta shida
 
Kwan kweli ulichukulia serious!??
Vipi anavyosemaga Simba ikishinda jmosi mapumziko ni hadi jtatu ni kweli huwa watu hawaendi kazini kisa simba imeshinda?

Sometimes nyuzi za aibu zinaanzishwa tu humu.
Tujaribu kutumia hekima,, tusijiexpose kwa watu namna tulivyo.
Umepoteza muda sana kumjibu huyu asiye na akili
 
MZEE HIVI UNAJUA KILA MTU ANA AKILI KAMA ZAKO WEWE??

KUNA WATU WANAAMINI KULIKO WEWE UNAVYOFIKIRI WEWE.

KAMA ALIKUA ANATANIA ANGESEMA (JOKES) WATU WANGEMUELEWA

NJOO USWAZI UONE WATU WANAVYOWAAMINI WATU WANAOONGEA KWENYE REDIO/MBELE YA CAMERAS

PUNGUZA UJUAJI NA UJENGE HOJA
Watu wanakushangaa tu ila hujafahamu..
Yaani hoja gani nijenge hapo,,
yaani why nitumie akili yangu kwa jambo la ajabu hivyo tena rahisi sana kwa watu kuelewa?

Hivi mtu aache kwenda kazini eti Ahmed kasema???? Dah..
Basi kweli tuna watu wasio na akili kwa namna hiyo.
 
Mkuu usichukulie serious kila jambo unalosikia. Utapata tabu sana.

Akili ni nywele. La kusikia/kuambiwa changanya na lako.

Japo una point.

Tumia akili yako vizuri.
 
Watu wanakushangaa tu ila hujafahamu..
Yaani hoja gani nijenge hapo,,
yaani why nitumie akili yangu kwa jambo la ajabu hivyo tena rahisi sana kwa watu kuelewa?

Hivi mtu aache kwenda kazini eti Ahmed kasema???? Dah..
Basi kweli tuna watu wasio na akili kwa namna hiyo.
ZUNGUKA KITAA UTAPATA MAJIBU
 
Kama wewe umelibeba serious hilo swala basi wewe ndie mwenye matatizo ni maneno mangapi ya hovyo hua wanaongea hao maafisa habari 🤔🤔 kwani hua yote yanafuatwa🤔🤔 Watakao taka kwenda huo muda waende usiwapangie cha kufanya
 
Wenye kazi za maana ni yanga waliokuwa wanaenda airport kupokea wageni halafu wanalipwa hela na wageni ila ukiwa shabiki wa yanga kazi kweli hivi anayeenda airport kuwapokea wageni na anayeenda uwanjani saa 6 nani hana kazi?
 
Ila haka kajamaa ukikatilia maanani wewe ndio itaonekana mpuuzi, wakati wa Robetinho alikuwa anamsifia lengo ni kupata ushindi, leo anageuka na kusema timu ilikuwa hazichezi vizuri Ila toka aje kocha mpya timu imebadilika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom