Agizo la Rais kunyang'anywa Passport Mkandarasi wa Maji

Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.

Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

Watu ni Waoga angeniita Bogas Kwenye Maswala ya Biashara na mikataba hapo hapo Ningemuita Bogas ni Yeye na Matako yake! Athubutu kunyang'anya Pasi ya Mmarekani ndio atajua Sangara ni Samaki na sii nguruwe! Mkondorasi ana Miradi Mingi na Sio Jukumu lake kukaa Site, Kika Mkondorasi anakuwa na Wasimamizi wa Miradi Foreman, Superintendents na Ma Project Managers Unamwambia Mkondorasi Utamnyanganya Passport mpaka siondoke mpaka amalize kazi wewe ndiye Mahakama ya Mikataba. Huyu Rais Nunda hasa!
 
Watu ni Waoga Tuangeniita Bogas Kwenye Maswala ya Biashara na mikataba hapo hapo Ningemuita Bogas ni Yeye na Matako yake! Mkondorasi ana Miradi Mingi na Sio Jukumu lake kukaa Site, Kika Mkondorasi anakuwa na Wasimamizi wa Miradi Foreman, Superintendents na Ma Project Managers Unamwambia Mkondorasi Utamnyanganya Passport mpaka siondoke mpaka amalize kazi wewe ndiye Mahakama ya Mikataba. Huyu Rais Nunda hasa!
Wewe mwenyewe muoga sana hadi unajificha nyuma ya ID feki. Hovyo kabisa. Kama kweli ni jasiri hebu jitokeze; vinginevyo ndio wale wale, kazi kupiga mikwara 24/7.
 
Passport ni mali ya serikali na imeandikwa katika page ya kwanza, kwamba inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Raisi wa JMT, au waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana wote wanayo mamlaka ya kuagiza/kuamuru passport kuchukuliwa kutoka kwa alie nayo kwa sababu mbalimbali kama vile usalama wa taifa, maslahi ya taifa na matumizi yasiyo mema.

Kwa hiyo, huyo mhindi kuna sababu maalum ya kuchukuliwa passport yake.

Raisi huwa hatoi kauli hadharani kama watu wengine bila kuwa na taarifa zote muhimu.

Wakati mwingine tuwe tunatumia muda kidogo kujifunza mambo madogo na ya msingi kama haya.
Bogus comment.....umeanza vizuri ukaharisha mwishoni. That may be applied kwa passports za nchini kwako
 
nimependa hapo "I WILI SHOO YUU" dah English ya ndaniii inabidi uwefit kuelewa vocabulary au ubebe dictionary ase.
By the way hajakutana na mkandarasi anayejiamini,asingekubali kuitwa bogus na kuamrishwa kutoa passpot mpaka amwone wakili wake! It izi noti propa kumgombeza hadharani,angeitwa chemba
 
Passport ni mali ya serikali na imeandikwa katika page ya kwanza, kwamba inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Raisi wa JMT, au waziri Mkuu au waziri mwenye dhamana wote wanayo mamlaka ya kuagiza/kuamuru passport kuchukuliwa kutoka kwa alie nayo kwa sababu mbalimbali kama vile usalama wa taifa, maslahi ya taifa na matumizi yasiyo mema.

Kwa hiyo, huyo mhindi kuna sababu maalum ya kuchukuliwa passport yake.

Raisi huwa hatoi kauli hadharani kama watu wengine bila kuwa na taarifa zote muhimu.

Wakati mwingine tuwe tunatumia muda kidogo kujifunza mambo madogo na ya msingi kama haya.
Asante kwa ufafanuzi mzuri, tatizo la watumia viroba na ngada wamezoea kupinga kila atendalo JPM hata kama lina ukweli na pia ni kawaida yao kuwatetea wabadhilifu wa Mali za umma,
 
Siyo mwekezaji ni mkandarasi...
Tutajua baadae kanjbai asituletee utapeli bils zetu kala maji hamna halafu akae na passport aje atukimbie..
Alete maji asituletee mchezo maana hata yeye mkataba unasema atajenga mradi wa maji uishe 1 March 2015 now 2017 maji hollah

Hivi hawa akina Kanjiba wanawalisha nini viongozi wa nchi hii, hatujifunzi toka kwa Chavda wa mkonge Tanga, na wale wa TRL walioingiza nchi hii matatizoni, mbele ya safari tutasikia mengi maana hao jamaa kwa kutoa 10% hawajambo
 
nimependa hapo "I WILI SHOO YUU" dah English ya ndaniii inabidi uwefit kuelewa vocabulary au ubebe dictionary ase.
By the way hajakutana na mkandarasi anayejiamini,asingekubali kuitwa bogus na kuamrishwa kutoa passpot mpaka amwone wakili wake! It izi noti propa kumgombeza hadharani,angeitwa chemba

Yule Mkandarasi anaonekana kuwa na wengi nyuma yake waliomuingiza chaka, tusubiri cinema
 
Mkuu naona umeiliza mwenyewe na umejijibu mwenyewe. Hatuna cha kukujuza hapo. Kuongeza tu kidogo mi nadhani Mzee Pombe alipaswa kutawala kabla ya Baba wa Taifa, siyo enzi hizi.

Rais amechoka kwa kuwaamini wasimamizi wa miradi na mambo mengine kwani wanamuangusha mfano alimuamini sana Makonda kumbe ametumia cheti cha mtu yeye ni mteule alieyemaliza darasa la saba tu according to Bishop Gwajima kwani shahada yake is no longer valid! You trust your aides then unakuta ni vihiyo, kweli Rais ana kazi! Viongozi wapo mfano waziri wa maji, katibu mkuu na wakurugenzi wa wizara wapo pamoja na wakuu wa Mkoa na wilaya lakini bado mkandarasi anafanya atakalo bila hofu!
 
Swala la mfanyakazi sio issue ya msingi hoja ni mkataba wa ujenzi unasemaje, uwezi kumshurutisha mtu bila ya kusema sababu za kosa lake the mere fact unakubali kuna short of funds isitoshe who's to certify funds already paid were delivered in time not to delay the schedule hivyo vitu ni muhimu sana kisheria kutokana na asili ya mkataba na namna gani contractor anafanya management ya project zake especially kama ana nyingine elsewhere na vifaa vyenyewe ndio ivyo ivyo.

Hawa wenzetu do actual planning on their mission realistically sio kama serikari ya Tanzania tunaamia Dodoma kumbe at the cost of lowering the quality of other interests groups mpaka unawaonea huruma hao waadhiri wanaotimuliwa kwenye nyumba za vyuo very pathetic.

Kwenye hili la kukaripiana huyo mkandarasi angejitia kihere here kumaliza unaweza kwenda mahakamani kudai fidia yako baada ya kukabidhi mradi ukajikuta mahakama aiwezi kukusaidia past consideration sio kigezo cha malipo yako habari za ohoo serikari ilielewa najenga na sijui tuna mkataba no one wants to hear that the court is only interested in the actual consideration as expressed in the contract kama walisema watakulipa jinsi kazi inavyoenda wewe ukajitia kihele hele cha kumaliza ndio udai there is nothing they can do endelea kudai maana hayo sio makubaliano yako ya awali na yanayotambulika kisheria.
 
Sijasikiliza yote ila nimeona sehemu anasema hakuna sehemu Mkandarasi anapewa pesa ndiyo afanye kazi. Ina maana ile dhana ya advance payment kwa wakandaras haipo duniani au kajitoa akili?

Anyway, mm sijamsikia from the beginning lkn naamini kabisa Kuna uwezekano wa uzembe kote kote. Mkuu ktk mirad hii serikali nayo ina sarakasi zake za ajabu sana.
Na ujue kuwa Advance payment inaganyika tuu kama kandarasi akiomba. Client hawezi kuitoa from no where..

Na wakati mwingine kuna miradi haina Advance..it depends on the form of contract.
 
Uwe unasikiliza kwa makini...
Mradi unagharimu bils 28.
Kashalipwa bils zaidi ya 20.
Ulibidi uishe 1 March 2015 mpaka leo hollah...
Sa unataka wammalizie pesa wakati mradi haujaisha na maji hakuna katika visima vyote 10
Huyo ni sawa na tapeli tu! Mi sijaona kibaya alifanya Magu. Walishazoea kuwazingua maraisi wengine sasa kiboko yao kaingia!!!!
"Nyang'anya tu baba"
 
Mkandarasi akishindwa kutekeleza mkataba ananyang'anywa passport? Tena na rais? Hadharani? Halafu anapigiwa vigelegele? Huyu kweli ni rais wa misifa tu (cheap popularity).

Jamaa keshatuona Watanzania ni zaidi ya vilaza. Yaani hatuna hata chembe ya fikra zaidi ya kushangilia kila ujinga. Yaani, wapumbavu kabisa. Haya tuone tutaendelea hivi hivi hadi lini kuifikia hiyo Tanzania ya viwanda.
Kuna contructual penalties zinapaswa zifuatwe in case of delay in construction na huwa zimeanishwa kwenye kila kila mkataba.

Kumnyang'anya mtu passport yake hakusaidii kitu zaidi tena ni kinyume kabisa na sheria za mkataba wa kaz yake ya ukandarasi manake zipo hatua kama contractor ata-default.
 
Kuna contructual penalties zinapaswa zifuatwe in case of delay in contraction na huwa zimeanishwa kwenye kila kila mkataba.

Kumnyang'anya mtu passport yake hakusaidii kitu zaidi tena ni kinyume kabisa na sheria za mkataba wa kaz yake ya ukandarasi manake zipo hatua kama contractor ata-default.
Mi nadhani president analifahamu ilo... Ila, kama mkandarasi analifahamu hilo pia na haoneshi kutishwa basi njia mbadala zitumike tu... (in Magu's thinking)
 
Washauri wa rais wanaweza kuwa wanamshauri rasi vibaya. Matokeo yake Mh.Rais anafanya maamuzi yenye utata yanaweza kwa namna moja au nyingine kuwa kikwazo kwa wawekezaji wa ndani na wakimataifa.
Ushauri mbaya umeanza kuharibu ''brand'' ya nchi yetu na sio jambo la kujivunia Tanzania kuwa branded kama Nchi isiyofuata Utawala wa Sheria

Jambo la msingi hapa ni kwamba nchi inaongozwa utawala wa katiba na sharia. Hata wawekezaji huzingatia sheria zetu zinamlinda au kumfaidisha vipi. Hakuna muwekezaji anayeweza kuwekeza mabilioni ya fedha bila kufahamu vyema sheria za nchi zenye uhusiano na uwekezaji au biashara yake. Sasa ikiwa nchi haifuati sheria na katiba muwekezaji anakuwa hana uhakika wa usalama wake. Kwa hiyo katika kuvutia wawekezaji hatuna budi kufuata utaratibu wa sheria, na kama tunaona kuna mwanya basi vyombo vya kutunga sheria vipi.

Yaani hata tukitaka kuweka sheria ya kunyanganya wawekezaji au wakandarasi passport tunaweza kuweka hiyo official kupitia bunge.

Jana katika vyombo vya habari tuliona tamko la Mh.Rais kwa Mkandarasi wa miundombinu ya maji mkoani Lindi, palepale polisi walichukua hatua ya kumpokonya mkandarasi wa watu passport yake.

Ninapinga kunyanganywa passport kwa mkandarasi huyo. Sipingani na rais maana ninajua rais kabla hajachukua hatua hushauriwa kwanza na wataalam husika. Kwa hiyo napingana na waliomshauri rais.

Sipingi kwa maana ya kumtetea mkandarasi kutokutimiza wajibu wake kwa wakati, la hasha ninapinga kutokufuata taratibu za kumwajibisha mkandarasi.

Serikali iliingia mikataba/mkataba na mkandarsi kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji. Mikataba yetu huingiwa na kutekelezwa kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya 2011 na Kanuni zake za 2013. Hiyo kuanzia uingiaji wa mkataba, utekelezaji na hata kusitishwa kwa mkataba ni lazima vifanyike kwa mujibu wa vigezo vya mkataba husika sambamba na Sheria ya Manunuzi ya 2011 na Kanuni zake za 2013. Na katika hizo taratibu hakuna taratibu za kunyanganya mkandarasi passport.

Sheria ya Manunuzi ya 2011 na Kanuni zake za 2013 na Mikataba ya miradi mikubwa kama ya miundombinu ya maji imeweka utaratibu mzuri sana wa kumwajibisha mkandarasi anayechelewesha kazi.

Kanuni ya 112 ya Kanuni za Manunuzi ya Umma unasema kuwa ikiwa mkandarasi atachelewa kumaliza kazi kwa mujibu wa mtakaba, atakatwa 0.1% mpaka 0.15% ya thamani ya mkataba wake kwa siku zilizocheleweshwa. Na makato hayo hayatazidi asilimia 10(10%) ya thamani ya mkataba.

Na kama utaendelea kuchelewesha kazi above the limit of liquidated damage, taasisi nunuzi itasitisha mkataba kwa kuwa mkandarasi amekiuka mkataba. Mkataba utasitishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 113 na Mkataba husika. Kama kusitishwa kwa mkataba kutasabibishwa na uzembe wa mkandarasi mitambo na vifaa vyote vitakavyokutwa site zitakuwa mali ya taasisi nunuzi

Hakuna kanuni inayotaka mkandarasi apokonywe passport.

Hii ni kuwatisha wawekezaji hasa wa nje
Umemaliza mjadala mkuu! Shikamoo PPRA
 
nimependa hapo "I WILI SHOO YUU" dah English ya ndaniii inabidi uwefit kuelewa vocabulary au ubebe dictionary ase.
By the way hajakutana na mkandarasi anayejiamini,asingekubali kuitwa bogus na kuamrishwa kutoa passpot mpaka amwone wakili wake! It izi noti propa kumgombeza hadharani,angeitwa chemba
d18f96b9caeb468c432236f50158d99a.jpg
 
Yaaah ni kweli mh.mara kadhaa anakuwa na jazba ni vema madaktari na washauri wafanye kitu hapo maana kiafya si kitu kizuri lakini pia kama kiongozi mkuu sisi wananchi wenye mapenzi mema na nchi hii hatuoni raha kila siku kumuona mkuu akilalamika juu ya ubovu wa maeneo kadhaa naamini hatua anazochukua ni sahihi kabisa na ushauri wangu aongeze dozi ingawa pia awashirikishe wataalamu wa kila fani kabla ya kuamua jambo lolote hasa wanasheria kutegemeana na jambo husika.
 
Kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa Mheshimiwa Rais ameagiza Mkandarasi wa Maji huko Lindi anyang'anywe pasipoti yake.

Ila kwa upande wangu sioni kama limefuata sheria kwani pasiport ni mali ya nchi iliyompatia mhusika na kwa mujibu wa sheria ya pasipoti, nchi husika huomba raia wake alindwe kwa namna yoyote na host country na ikibidi kukamatwa basi nchi husika ijulishwe. Swali langu, je Mkandarasi huyu kavunja sheria ipi ya nchi?

Kama alichelewa kulipwa fedha za mradi tulitegemea ajenge kwa fedha zake mfukoni?? Naomba kujuzwa kwani elimu yangu ni ndogo.

"Under the law of most countries, passports are government property, and may be limited or revoked at any time, usually on specified grounds, and possibly subject to judicial review"

huu ni udhaifu mkubwa wa watendaji mahala fulani, either wizarani au mkoani. Mkataba wa kumbana mkandarasi upo, ainisho la malipo yanatakiwa yalipweje kwa kila hatua ya mradi ipo, sasa mtu analipwa karibu 80% na kazi hajamaliza na mradi haueleweki huu ni udhaifu mkubwa. Kama watendaji wangesimamia vizur hakuna haja ya raisi kwenda pale na kufokeana na mkandarasi. Huo mradi uchunguzwe kwanini watendendaji walikuwa wanamwogopa kumbana mkandarasi mpaka raisi aende kumbana? na wananchi wanazidi kuteseka kwa kukaa bila maji safi na salama?
 
Back
Top Bottom