AG: Ufafanuzi juu ya uteuzi wa wabunge na kupewa uwaziri

Kuna ili taasisi ya Kukanusha habari Ikulu a.k.a Kurugenzi ya ... Iko wapi isifafanue na hili? Then tutamsikia na Nape akifafanua. Tanzania na zaidi ya uijuavyo!!!!!
 
Kuna watu nadhani huwa wanabebwa na viongozi walio juu yao. Sijawahi hata siku moja kuona Warema ametoa hoja ambayo kweli ni ya kisheria. Mara zote hudandia hoja kwa mbele.halafu huyu Jk naye hafikiri. Hakupaswa kumuacha kwenye nafasi yake kwa vile madudu yote yaliyofanywa na mawazi wake mwasheria baada ya kuona ile ripoti alimshauri nini rais? Anatetea mambo ya aibu huyu jamaa.
 
Tumekusikia Jaji, lakini mawaziri watakapoitwa kukutana na kamati za Bunge itakuwaje kwa sababu hizo kwa sisi wenye uelewa mdogo ni shughuli za bunge vile vile. Kwa kifupi, kamati za bunge ni bunge vinginevyo ni wazi kuna matatizo kwenye katiba au wanaotafsiri hiyo katiba.
mimi naona katiba hii inatafsiriwa kimaslahi kuliko matakwa ya utunzaji wa misingi ya katiba. nahisi Werema alifikiri umma huu ni kubwa jinga kiasi kwamba anadiriki kuendelea na mchakato wa kuongopea umma. kwanza atuambie ni kwanini Zanzibar wamevunja katiba hali yeye kama muhimili wa utunzaji wa katiba amekaa kimya kama vile hakuna kilichotokea . anajua kabisa KatibA YA JMT inatambua uwepo wa nafasi ya CHIEF MINISTER - WAZIRI KIONGOZI na wala siyo VICE presidents kama ilivyo sasa huko zanzibar. yeye kauchuna. kukaa kimya nako ni kuvunja katiba kwani hili ni jambo la HATARI NA uhaini MWENYE KUBISHA ABISHE. HE IS ASSUMING PROTOCOLS OF IMPUNITY. hii inathibitisha ubutu alio nao na upeo mdogo juu ya masuala ya sheria ambayo anayasimamia. si mara ya kwanza kwa WEREMA KUWA BUTU. NAKUMBUKA HATA ENZI LA SPIKA SITA WALIWAHI KUBISHANA SANA JUU YA SUALA FULANI HATA SITA AKALAZIMIKA KUMWAMBIA HII NI SIASA KWA MAANA KWAMBA HE IS TOO NAIVE ON ROLE AS MEDIATOR BETWEEN THE CONSTITTUTIONAL LAW AND NEEDS OF THE LAW ATA A PARTICULAR MOMENT. KWAHIYO UWEZO WAKE WA KUTAFSIRI SHERIA KUWA KATIKA MATUMIZI NI BUTU.
 
Jamani mie sio mwanasheria, lakini kuna wakati ninakuwa na wasiwasi sana juu ya uwezo wa Werema wa kutafsiri sheria. Niliwahi kuandika humu kwamba hukumu nyingi za Werema zilitupwa nje pale zilipokatiwa rufaa. Ukiwa jaji, na ukaona zaidi ya 50% ya hukumu zako zinazokatiwa rufaa zinatupwa nje inabidi ujiulize kama una uwezo wa kuwa jaji. Sijui kama Werema amewahi jiuliza hili.

Kulingana na katiba " Article 55(4) all ministers and deputy ministers shall be appointed from among members of parliament".

Sasa kama Werema ni mwanasheria makini, alipasa kutueleza ni wakati gani mtu anakuwa mbunge rasmi; pale anapochaguliwa/kuteuliwa au baada ya kuapishwa?

Hypothetical case: Mfano, ikiwa katika hawa mawaziri wabunge wateuliwa mmoja wapo for argument sake, akatae kuapishwa ubunge, na ameapishwa uwaziri, ataendelea kuwa waziri?

Je, sheria inaweza kufanya "ex-ante" assumption, kwamba linalotakiwa litakuwa? Ina maana mfano, unamwambia trafiki aliyekukamata unaendesha basi bila leseni inayotakiwa, kwamba unajua nilishafaulu jana kozi ya chuo cha usafirishaji kuendesha basi, kwa hiyo bwana bila shaka nitapata tu leseni. Usijali wala sio tatizo kwamba sina leseni leo. Nikamate wiki ijayo utaona nina leseni ya kuendesha basi!

Kwa kweli tuna Mwanasheria Mkuu!!!
 
mbona wanataka kutuchanganya hawa jamaa, ngoja nirudi nikapitie katiba tena, I'll be back!
 
68. Kila mbunge atatakiwa kuapishwa katika bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za bunge; lakini
mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa spika hata kabla
hajaapishwa.

kwa mujibu wa kipengele hiki, mtu aweza kuwa mbunge kabla ya kuapishwa, then akiapishwa cha uaminifu ndo anaweza kushiriki kazi za bunge. Otherwise kwa nini aitwe "mbunge" na katiba kabla ya kuapishwa kwake?
 
Hii si mahakama, ambaye hakufurahisha na uteuzi aende akafungue kesi ya katiba. Mbona sioni m2 akitoa ufafanuz wa kisheria km AG alivyofanya?
Naona maneno ya kanga 2 humu.
 
Jamani mie sio mwanasheria, lakini kuna wakati ninakuwa na wasiwasi sana juu ya uwezo wa Werema wa kutafsiri sheria. Niliwahi kuandika humu kwamba hukumu nyingi za Werema zilitupwa nje pale zilipokatiwa rufaa. Ukiwa jaji, na ukaona zaidi ya 50% ya hukumu zako zinazokatiwa rufaa zinatupwa nje inabidi ujiulize kama una uwezo wa kuwa jaji. Sijui kama Werema amewahi jiuliza hili.

Kulingana na katiba " Article 55(4) all ministers and deputy ministers shall be appointed from among members of parliament".

Sasa kama Werema ni mwanasheria makini, alipasa kutueleza ni wakati gani mtu anakuwa mbunge rasmi; pale anapochaguliwa/kuteuliwa au baada ya kuapishwa?

Hypothetical case: Mfano, ikiwa katika hawa mawaziri wabunge wateuliwa mmoja wapo for argument sake, akatae kuapishwa ubunge, na ameapishwa uwaziri, ataendelea kuwa waziri?

Je, sheria inaweza kufanya "ex-ante" assumption, kwamba linalotakiwa litakuwa? Ina maana mfano, unamwambia trafiki aliyekukamata unaendesha basi bila leseni inayotakiwa, kwamba unajua nilishafaulu jana kozi ya chuo cha usafirishaji kuendesha basi, kwa hiyo bwana bila shaka nitapata tu leseni. Usijali wala sio tatizo kwamba sina leseni leo. Nikamate wiki ijayo utaona nina leseni ya kuendesha basi!

Kwa kweli tuna Mwanasheria Mkuu!!!

you have made my day,ama kweli mwanasheria mkuuuuuuuuuuu wa serikali ameifanana vizuri sana hii serikali yake
 
Kuna watu nadhani huwa wanabebwa na viongozi walio juu yao. Sijawahi hata siku moja kuona Warema ametoa hoja ambayo kweli ni ya kisheria. Mara zote hudandia hoja kwa mbele.halafu huyu Jk naye hafikiri. Hakupaswa kumuacha kwenye nafasi yake kwa vile madudu yote yaliyofanywa na mawazi wake mwasheria baada ya kuona ile ripoti alimshauri nini rais? Anatetea mambo ya aibu huyu jamaa.
Kamati kuu ya CCM ndio mshauri mkuu wa rais na si AG.
AG yeye ni kusubiri kufafanua tu. na kuisemea ikulu amechukua cheo cha kurugenzi ya habari

Hofstede,
Majibu ya maswali ya Wabunge kikawaida hayaandaliwi na waziri, yanaandaliwa na Katibu Mkuu na watendaji wengine wa wizara. Kikawaida waziri ni msomaji tu na mwakilishi wa serikali bungeni.

Umesema hili ni mara ya kwanza, hapana hata wakati wa Nyerere na Mwinyi lilikuwa linafanyika hasa alipokuwa anabadilisha baraza la mawaziri. Hivi nani anakumbuka vizuri alipoteuliwa Malecela kuwa PM ilikuwaje? Kama nakumbuka vizuri aliteuliwa ubunge na uwaziri mkuu hapo hapo. Wakati huo waziri Mkuu alikuwa hathibibitishwi na bunge kwanza.

Mbunge wa viti maalumu wa CHADEMA ninayemsema ni somebody Rebecca Mhando. Kama unakumbuka vizuri kuna majimbo uchaguzi uliahirishwa kwa wiki mbili. NEC ilipoteua viti maalum iliacha nafasi chache ikisubiri matokeo ya ubunge kwenye majimbo hayo. Yalipotoka CHADEMA waliongezewa viti kikiwemo cha huyo Mhando. Wakati huo Wabunge walikuwa wameapishwa na bunge kuahirshwa mpaka January au February ndio huyo mama alikuja kuapishwa.

Ccm waligoma asishiriki kuchagua meya Arusha lakini AG akatoa ufafanuzi kwamba huyo ni mjumbe halali na akaruhusiwa kupiga kura.

Kushiriki shughuli za bunge kunakoongelewa na katiba ni kuuliza maswali, kujibu maswali, kuchaguliwa kamati za bunge na shughuli zote ambazo zinafanyika ndani ya bunge. Kuandaa budget hufanywa na serikali kupitia watendaji Kama Katibu mkuu na pia mawaziri. Hili hufanywa nje ya bunge. Ila kukitokea utata waziri akaitwa kuhojiwa na kamati ya bunge nafikiri hapo itabidi aende Yule ambaye ameapa.
Malecea alikuwa mbunge wa Mtera toka mwaka 1990 hadi 2010 na ni wakati huo huo alikuwa waziri mkuu na Vice President. Tazama record zako vizuri..

Pengine tujieleze vizuri hapa ni kwamba swala sio lugha na tafisri yake bali ukweli unaojulikana. Unaposema neno MEMBER of the Parliament ina taratibu zake uwe member na ndio maana unaapishwa hivyo kiapo ni muhimu ktk kumfanya mbunge mteule kuwa member, kifupi huwezi kuwa member wa Parliament kama hujaapishwa japokuwa unaweza kushiriki kumchagua Spika maana hata yeye ni kati ya watu wanaounda Bunge. Na hivyo kuna sababu ya mbunge kuruhusiwa kumchagua Spika nayo ni kwamba Spika ndiye atakaye waapisha wabunge pasipo yeye kiapo cha mbunge yeyote hakitafuatana na katiba.

Leo hawa Mawaziri tayari wameisha apishwa na kuwafanya mawaziri na tayari wanaweza kuanza kazi za Uwaziri kinyume cha ibara ya 56. Hivyo kutayarisha bajeti ni mamlaka yaliyopo chini ya uongozi wa waziri hata kama inaandikwa na mtu mwingine kama tunavyozisoma hotuba za rais, na Waziri hatakiwi kuifanya kazi hiyo ama nyingine yeyote ya uwaziri hadi awe kisha apishwa bungeni (kiapo cha kwanza).

Haya mengine yooote tutabishana hapa lakini ukweli utabakia kwamba JK katufungia kanyaboya kisheria hawa sii mawaziri bali bado ni wateule hadi watakapoapishwa bungeni na hawatakiwa kushiriki ktk shughuli zozote za serikali kama waziri hadi watakapo apishwa bungeni..
 
Kamati kuu ya CCM ndio mshauri mkuu wa rais na si AG.
AG yeye ni kusubiri kufafanua tu. na kuisemea ikulu amechukua cheo cha kurugenzi ya habari

Hata NAPE nae huwa anafafanua........
Ikulu inakanusha......

Chezeya serekale ya kishkaji wewe!!
Unaendesha nchi kwa kupima upepo!!
 
Hivi nilikuwa najiuliza mbona huyu jamaa ni Jaji ambaye hana rekodi kwenye rekodi za mahakama? yaani Judgement? Nimegundua leo baada ya ufafanuzi huu wa ajabu kabisa kuwahi kutolea,

Maswali kwake,
1. Hivi vikao vya kamati za Bunge ni shughuli za Bunge? kama ndio hawa mawaziri watawezaje kushiriki huko kupitisha bajeti zao wakati hawajaapishwa?

2. Hivi , mbona kwenye buinge la Mwezi April Spika ailikataa swali la Cecilia Pareso kwa hoja kwamba lilitumwa kabla hajaapishwa na hivyo alikuwa hana haki ya kufanya hivyo, leo hawa mawaziri wataweza vipi kusimamia wizara na haswa mchakato wa kibajeti?
 
Kimsingi naona sheria inakaa kimya katika hili kwenye Katiba ya JMT,

inasema waziri atateuliwa miongoni mwa wabunge, sasa sijui sheria inayohusu mbunge inasemaje......katiba inavyotamka Mbunge inamanishi mbunge mteule (MP Elect) au MP kwa maana ameshachaguliwa na kuapa kushika rasmi shughuli za kibunge??!!!

mimi confused kodogo hapa!
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Werema, amevunja Katiba.Amekiuka Ibara ya 59(3) ya Katiba yetu. Ametoa nje ushauri aliopaswa kuishauri Serikali tu.

Ameuanika ufafanuzi wa uteuzi wa Rais wa Mawaziri,ambao bado sio Wabunge,kinyume na Katiba na Taratibu za kikazi.Kwa mujibu wa Ibara iliyotajwa hapo juu, Mwanasheria Mkuu ni Mshauri Mkuu wa kisheria wa Serikali tu.

Hutoa ushauri pale unapohitajika.Huu ufafanuzi aliombwa na nani? Werema anavuka mipaka...

Mie napita tu mkuu...
 
Kikwete ni mjanja sana!
Hata wewe nakushauri wewe VUTA-NKUVUTE: Ukitaka kula vizuri, weka taahira wengi ambao hawaelewi chochote kwenye vitengo. maana hichi ndicho alichofanya Kikwete! Werema ni bogus hujapata ona! Sheria hajui, hasomi vitabu yaani yupo yupo tu.
 
Tuna AG kweli? ni binafsi sikuona ugumu wowote hapo wa lkushindwa kuwaapisha, sasa wanazidi kufanya jambo kuwa gumu bila sababu.....wangeweza kuaapisha tu kwa kutumia ofisi ya bunge hapo dar, katibu wa bunge ni rahisi yeye na spika kwenda pale Dar.... kisha wakarudi zao huko Dodoma kama hawap Dar pia
 
Malecea alikuwa mbunge wa Mtera toka mwaka 1990 hadi 2010 na ni wakati huo huo alikuwa waziri mkuu na Vice President. Tazama record zako vizuri..

Pengine tujieleze vizuri hapa ni kwamba swala sio lugha na tafisri yake bali ukweli unaojulikana. Unaposema neno MEMBER of the Parliament ina taratibu zake uwe member na ndio maana unaapishwa hivyo kiapo ni muhimu ktk kumfanya mbunge mteule kuwa member, kifupi huwezi kuwa member wa Parliament kama hujaapishwa japokuwa unaweza kushiriki kumchagua Spika maana hata yeye ni kati ya watu wanaounda Bunge. Na hivyo kuna sababu ya mbunge kuruhusiwa kumchagua Spika nayo ni kwamba Spika ndiye atakaye waapisha wabunge pasipo yeye kiapo cha mbunge yeyote hakitafuatana na katiba.

Leo hawa Mawaziri tayari wameisha apishwa na kuwafanya mawaziri na tayari wanaweza kuanza kazi za Uwaziri kinyume cha ibara ya 56. Hivyo kutayarisha bajeti ni mamlaka yaliyopo chini ya uongozi wa waziri hata kama inaandikwa na mtu mwingine kama tunavyozisoma hotuba za rais, na Waziri hatakiwi kuifanya kazi hiyo ama nyingine yeyote ya uwaziri hadi awe kisha apishwa bungeni (kiapo cha kwanza).

Haya mengine yooote tutabishana hapa lakini ukweli utabakia kwamba JK katufungia kanyaboya kisheria hawa sii mawaziri bali bado ni wateule hadi watakapoapishwa bungeni na hawatakiwa kushiriki ktk shughuli zozote za serikali kama waziri hadi watakapo apishwa bungeni..

Mkuu Mkandara,
Angalia records zako, Malecela alikuwa balozi wa TZ nchini Uingereza alipoteuliwa kuwa waziri mkuu.

Alienda kugombea Mtera 1995. Records zako haziko sahihi, zirekebishe. Mwaka 1990 hakukuwa na jimbo la Mtera.
 
Back
Top Bottom