AG: Ufafanuzi juu ya uteuzi wa wabunge na kupewa uwaziri

Swali: Bunge likikutana july, wataapa hawa walioteuliwa wakati wameshaanza kazi tayari???? Cijuw JK alikuwa wapi wakati bunge liko LIVE...
Angetoa mfano basikama imewahi kutojea rais akanwapisha mtu kuwa waziri kabla mtu huyo hajaapishwa kuwa mbunge ingeoneshaana hoja sasa hivi amejaribu kuhalalisha kilichoharimishwa. Na yeye kama wengine wanawekatafsiri yao juu ya "shughuli za bunge"na kuzifunga kwenye kile kinachofanyika ndan ya bungeni. Kuna haja ya kufungua kesi ya kikatiba hapa.
 
68. Every member of Parliament shall be required to
take and subscribe before the National Assembly the
oath of allegiance before commencing to take part in
the business of the National Assembly save that he may
take part in the election of Speaker before taking that
oath.

Tafsiri katika Kiswahili!

68.
Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.



Nafikiri pia kinachogomba zaidi hapa ni lugha, je hizi tafsiri mbili ni sahihi?...binafsi naamini hizi tafsiri mbili hazifanani wala hazipatani, kwa mfano mdogo tu;

  1. Allegiance - Uaminifu?
  2. Parliament - Bunge? National Assembly?
Na hapo bado kupitia vipengele vyenyewe, yaani mkanganyiko mtupu, nachoka! Yaani tafsiri ya Kiswahili inasikitisha na inaonesha mapungufu makubwa katika umakini unaotakiwa kwenye jambo zito kama Katiba.
62. (1). There shall be a Parliament of the United Republic which shall consist of two parts, that is to say, the President and the National Assembly.
 
Je, mtu anakuwa Mbunge kabla ya kuapishwa?...........katika tukio hili la Rais hivi karibuni.........Katiba yetu haijatofautisha kati ya Mbunge Mteule na Mbunge...........na kutokana na vipengele husika......JK yuko sahihi.........

Cha msingi katiba inabidi iwe improved...........
 
Mbona rais akichaguliwa haanzi kazi mpaka aapishwe??mbona kwa wabunge mambo yanapindishwa jamani??
Hivi ni vimbwanga kwa kweli..
 
Ninachosikitika ni kwamba wengi mnasema kuwa JK/AG wamekiuka katiba bila wale wanaokosoa kunukuu ni ibara au kipengere gani kimekiukwa! sivyo mtu yeyote anavyodhani kuwa ni sawa au si sawa basi ndio iwe haki bali tuangalie katiba inasemaje kuhusu suala hili na si kutoa hoja zetu kutoka kwenye kila kichwa cha mtu!
Chuma Chakavu kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili suala. Watu wote tumekubaliana kwamba lazima mawaziri/manaibu waziri wawe wabunge. Pia tunakubaliana kwamba wabunge wote wanatakiwa waape kiapo cha uaminifu bungeni kwa mujibu wa ibara ya 68. Ukisonga mbele kwenye ibara ya 69 (1) inasema hivi, "Kila mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku thelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama mbunge kuwasilisha kwa Spika nakala mbili......"


Ukiangalia hapo kwenye wekundu Mbunge anatakiwa aapishwe ili kushika madaraka yake kama mbunge. Hakuna kiapo kingine cha mbunge kinachoongelea zaidi ya kile cha Ibara ya 68. Hivyo Ubunge ni Madaraka ambayo unatakiwa uyashike baada ya kuapa; kabla ya kuapa huna madaraka hayo ya Ubunge.




 
Last edited by a moderator:
Mbona rais akichaguliwa haanzi kazi mpaka aapishwe??mbona kwa wabunge mambo yanapindishwa jamani??
Hivi ni vimbwanga kwa kweli..
Purple Na ukumbuke kwamba mgombea Urais akishatangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba ameshinda uchaguzi na kuchaguliwa kuwa Rais hakuna kwenda mahala popote kuhoji huo ushindi. Hivyo piga geuza mtu akishatangazwa na Tume kuwa ameshinda basi yeye ni Rais. Lakini kwa kuona umuhimu wa viapo kabla ya kushika madaraka Katiba inasema Rais ataapa kiapo cha uaminifu mbele ya Jaji Mkuu. Kama kiapo hakina umuhimu wowote kwa nini asianze tu kazi kwa kuwa hakuna chances zozote kwamba ushindi wake unaweza kuhojiwa?
 
Last edited by a moderator:
Chuma Chakavu kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili suala. Watu wote tumekubaliana kwamba lazima mawaziri/manaibu waziri wawe wabunge. Pia tunakubaliana kwamba wabunge wote wanatakiwa waape kiapo cha uaminifu bungeni kwa mujibu wa ibara ya 68. Ukisonga mbele kwenye ibara ya 69 (1) inasema hivi, "Kila mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku thelathini tangu aapishwe kushika madaraka yake kama mbunge kuwasilisha kwa Spika nakala mbili......"




Ukiangalia hapo kwenye wekundu Mbunge anatakiwa aapishwe ili kushika madaraka yake kama mbunge. Hakuna kiapo kingine cha mbunge kinachoongelea zaidi ya kile cha Ibara ya 68. Hivyo Ubunge ni Madaraka ambayo unatakiwa uyashike baada ya kuapa; kabla ya kuapa huna madaraka hayo ya Ubunge.





Mimi naona tungejikita zaidi kwenye version ya kiingereza ya katiba na tupate maana au tofauti kati ya PARLIAMENT na NATIONAL ASSEMBLY, na vile vile nini mantiki ya OATH OF ALLEGIANCE, inawezekana lugha zikawa zinatukanganya kwa maana ya tafsiri ya ibara au kipengere husika kuja kwenye kiingereza. Yaani napendekeza soma ibara hiyo uliyonukuu katika katiba ya kiingereza na uone kama utapata maana zinazoshabihiana
 
Katika mambo yote serikali ya CCM iliyofanya kwa ufasaha bila kukosea ni hili la uteuzi wa wabunge na kuwapa uwaziri. Kuna watu humu wanadai Rais amevunja kifungu cha katiba ambapo kwangu mimi ni kifungu cha "kusadikika" maana hamna hata mmoja aliyesema ni kifungu kipi cha katiba ya JMT ambacho kimevunjwa. Tuelewe hakuna mahala popote ndani ya katiba au kwenye sheria za nchi palipoandikwa kwamba Rais hawezi kumteua mtu kuwa waziri mpaka pale atapoapishwa kuwa mmbunge. Ni vizuri tukaacha siasa za kitoto ama kwa neno lingine siasa rahisi za kulaumu kila jambo.
Nimesikitishwa sana na mwenyekiti wa CDM kuupotosha umma wa Watanzania kwa jambo ambalo naamini analielewa vizuri tu. Na kwa siasa hizi, CDM inaelekea pabaya na kusipofanyika juhudi za kumtoa huyu Mbowe hiki chama kitapoteza nuru yake iliyong'aa vizuri. Watu hawakuipenda CDM kwa siasa za upotoshaji. Waliipenda kwa hoja thabiti zenye mashiko na si huu upuuzi wa Mbowe.
Shime wana CDM wenzangu, huku tukifanya operation vua gamba tuanze sasa na operation kumuondoa Mbowe. Naona tunahitaji mawazo mapya ya mwenyekiti, huyu bwana kachoka.
 
Mimi naona tungejikita zaidi kwenye version ya kiingereza ya katiba na tupate maana au tofauti kati ya PARLIAMENT na NATIONAL ASSEMBLY, na vile vile nini mantiki ya OATH OF ALLEGIANCE, inawezekana lugha zikawa zinatukanganya kwa maana ya tafsiri ya ibara au kipengere husika kuja kwenye kiingereza. Yaani napendekeza soma ibara hiyo uliyonukuu katika katiba ya kiingereza na uone kama utapata maana zinazoshabihiana

Mkuu nina katiba ya kiswahili!

Ila najua kuna Parliament na National Assembly ambapo mojawapo huwa linamhusisha Rais pale Katiba inaposema Rais ni sehemu ya Bunge ila yeye si Mbunge. Ni sehemu ya Bunge kwa kuwa ili sheria (muswada) uwe sheria lazima isainiwe na Rais.
 
Hofstede,
Majibu ya maswali ya Wabunge kikawaida hayaandaliwi na waziri, yanaandaliwa na Katibu Mkuu na watendaji wengine wa wizara. Kikawaida waziri ni msomaji tu na mwakilishi wa serikali bungeni.

Umesema hili ni mara ya kwanza, hapana hata wakati wa Nyerere na Mwinyi lilikuwa linafanyika hasa alipokuwa anabadilisha baraza la mawaziri. Hivi nani anakumbuka vizuri alipoteuliwa Malecela kuwa PM ilikuwaje? Kama nakumbuka vizuri aliteuliwa ubunge na uwaziri mkuu hapo hapo. Wakati huo waziri Mkuu alikuwa hathibibitishwi na bunge kwanza.

Mbunge wa viti maalumu wa CHADEMA ninayemsema ni somebody Rebecca Mhando. Kama unakumbuka vizuri kuna majimbo uchaguzi uliahirishwa kwa wiki mbili. NEC ilipoteua viti maalum iliacha nafasi chache ikisubiri matokeo ya ubunge kwenye majimbo hayo. Yalipotoka CHADEMA waliongezewa viti kikiwemo cha huyo Mhando. Wakati huo Wabunge walikuwa wameapishwa na bunge kuahirshwa mpaka January au February ndio huyo mama alikuja kuapishwa.

Ccm waligoma asishiriki kuchagua meya Arusha lakini AG akatoa ufafanuzi kwamba huyo ni mjumbe halali na akaruhusiwa kupiga kura.

Kushiriki shughuli za bunge kunakoongelewa na katiba ni kuuliza maswali, kujibu maswali, kuchaguliwa kamati za bunge na shughuli zote ambazo zinafanyika ndani ya bunge. Kuandaa budget hufanywa na serikali kupitia watendaji Kama Katibu mkuu na pia mawaziri. Hili hufanywa nje ya bunge. Ila kukitokea utata waziri akaitwa kuhojiwa na kamati ya bunge nafikiri hapo itabidi aende Yule ambaye ameapa.
 
Mkuu nina katiba ya kiswahili tu basi!

Ila najua kuna Parliament na National Assembly ambapo mojawapo huwa linamhusisha Rais pale Katiba inaposema Rais ni sehemu ya Bunge ila yeye si Mbunge. Ni sehemu ya Bunge kwa kuwa ili sheria (muswada) uwe sheria lazima isainiwe na Rais.
je katiba yako ya kiswahili imetofautishaje kati ya parliament na national assembly? na kuhusu oath of allegiance kiswahili kinasemaje kwenye katiba? naomba msaada kwa hayo mambo mawili labda tutapata muafaka.
 
Labda uelewa wangu ni mdogo. Hivi hata ingekuwa Kateua jina lingine la Waziri Mkuu mbali na wa sasa angeanza kazi bila ile kura ya ridhaa ya Wabunge?
 
Kama katiba haisemi lazima waapishwe ndani ya Ukumbi wa Bunge kwa nini Mh. Makinda asiwaapishe hawa wateule kabla ya kula kiapo cha uwaziri? Viongozi wetu wajifunze kutafuta suluhu ya matatizo badala ya kuyakuza
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.



Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
06 Mei, 2012

Hivi Vyuo vyetu havina utaratibu wa kufuta shahada na stashahada zilizoexpire? Maana shahada nyingine zinadhalilisha fani
 
Labda uelewa wangu ni mdogo. Hivi hata ingekuwa Kateua jina lingine la Waziri Mkuu mbali na wa sasa angeanza kazi bila ile kura ya ridhaa ya Wabunge?

Waziri Mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa majimboni. Lakini waziri Mkuu lazima athibitishwe na bunge hivyo kikao cha dharura cha bunge kingeitishwa kupitisha Jina na baada ya hapo kwa pamoja wangeunda baraza la mawaziri.
 
Wanabodi,
hapa tutaendelea kubishana mpaka asubuhi.

Hebu na tuachane na vifungu vya sheria twende kwenye ukweli halisi.
1. Ili uwe waziri lazima kwanza uwe mbunge!.

2. Ili uwe mbunge lazima ule kiapo cha uaminifu bungeni!. Maana ya kiapo hiki ndio mamlaka ya kibunge. Hata rais baada ya kuchaguliwa, anapewa mamlakana kiapo!. Vivyo hivyo kwa wabunge wanapewa mamlaka na kiapo!.

3. Yaani ubunge ni pre condition ya uwaziri haijalishi unafanya kazi wapi!. Huwezi kuwa waziri kabla hujawa mbunge na kuteuliwa pekee hakukufanyi kuwa mbunge kitendo cha kuapishwa ndio mamlaka ya kibunge!.

4. Katiba imetoa kazi moja tuu kwa mbunge ambaye hajaapishwa anayoweza kuifanya nayo ni kumchagua spika!. Baada ya hiyo kama waziri ni lazima kwanza awe mbunge, hii inamaanisha nafasi ya uwaziri inatokana na ubunge hivyo chochote waziri anachofanya ana derive mamlaka kutokana na ubunge.

5. Hoja ya kuwa eti kiapo cha ubunge ni kwa matumizi ya vikao vya bunge tuu ni hoja muflisi!. Yaani waziri hata akisaini tuu dokezo ni kazi ya kibunge kwa sababu ni kupitia ubunge wake ndiko anapata hayo mamlaka ya kusaini hilo dokezo.

6. AG amechemsha big time na sasa tutamshuhudia rais aki pull the cart before the horse!.
 
Kama katiba haisemi lazima waapishwe ndani ya Ukumbi wa Bunge kwa nini Mh. Makinda asiwaapishe hawa wateule kabla ya kula kiapo cha uwaziri? Viongozi wetu wajifunze kutafuta suluhu ya matatizo badala ya kuyakuza

Kuna katiba ya Tanzania na taratibu za bunge. Taratibu za bunge ndio zimesema mbunge ataapishwa kwenye kikao cha kwanza cha bunge baada ya kuchaguliwa. Huu ni utaratibu tu.
 
Pasco,
Nikuulize swali babake Sioyi mpaka anakufa alikuwa mbunge au hakuwa mbunge? Kama alikuwa mbunge aliapishwa wapi? Na aliapishwa na nani?

Kuwa mbunge sio lazima kwanza uapishwe na spika. Kuapishwa sio pre condition ya kuwa mbunge bali ni pre condition ya kushiriki shughuli za bunge ( national assembly).

Ubunge wako unaanza Mara tu baada ya kutangaza na NEC, baada ya kuteuliwa na NEC na baada ya kuteuliwa na rais.

Waziri akisaini dokezo au akiandaa budget anaandaa kama mtendaji wa serikali mhimili ambao ni tofauti na bunge. Kufanya hivyo vitu hata Katibu Mkuu anafanya wala Haina uhusiano na kuwa mbunge.
 
Back
Top Bottom