Afungwa JELA kwa kuuza NYAMA YA MBWA

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Godfrey Sanga amehukumiwa kwenda jela kifungo cha miaka mitano baada ya mahakama kuthibitisha kuwa julai 7 alichinja mbwa wanne na kuwauza katika klabu ya pombe za kienyeji iitwayo TUPENDANE,kijana huyo pia amekiri mbele ya mahakama hiyo ya mkoni njombe kuwa si mara ya kwanza kwake yeye kuuza nyama ya mbwa na mara nyingine huwa anachuna mizoga iliyokufa na kuanza kuichuna ngozi na pia kuuza nyama kilabuni hapo,
sosi:RFA
NB:kama hili limetokea njombe,basi tuwe makini na mahali popote,huyu jamaa hayupo peke yake,niliwah kuleta bandiko hapa kuwa kuna jamaa hapo magomeni alikamatwa kwa tabia ya kuuza kuku waliokufa
 
wamemuonelea tu, mbona ya nguruwe inaliwa na wanaangalia tu na huku wakijua fika kuwa inawakera wanajamii wengine?
 
kosa linakuwa pale unapowauzia wengine na kutumia hiyo nyama pasipo wao kujua,

wamemuonelea tu, mbona ya nguruwe inaliwa na wanaangalia tu na huku wakijua fika kuwa inawakera wanajamii wengine?
 
Royals,kwa wale walioridhia,,,,,,,,,huenda hakua anasema kuwa ni nyama ya wu wu
 
Last edited by a moderator:
kosa linakuwa pale unapowauzia wengine na kutumia hiyo nyama pasipo wao kujua,

sure riga,,,,,,mfano kuwalisha watu mizoga.....ambapo mshtakiwa bwana Sanga alikiri mbele ya mahakama kuwa huwa anaokota mizoga na kuichuna ngozi na kisha kuwauzia watu,,,,
 
Kuna mwingine kule Singida naye alikuwa anafanya biashara hiyo. Yeye alikuwa mtaalamu sana na hakuwahi kukosa hicho kitoweo. Wateja wake wakikuwa wanamsifia kwa kuuza "nyamapori" ya ukweli.

Mbinu alizokuwa anazitumia: Yeye ni muwindaji (sungura, swala, nyumbu-ingawa hakuwa na kibali)hivyo kila siku alikuwa anatoka na mbwa wake visu viwili vikali na upinde na mishale. Akiona mbwa anamvuta kwa kutumia yule wake then anamwua na kumbeba, anaenda katika pango lake na kumchuna. Nyama anaiuza na vichwa anakula yeye mwenyewe. Hadi anakamatwa alikiri kuwa na hazina kubwa ya nyama kavu za mbwa hao, na mahali zilipo na wateja wake ni akina nani...:hungry:

Ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni...mmoja kati ya wateja wake baada ya kuona "jamaa" yao kakamatwa alilaani sana kwani asingeendelea kupata kitoweo kwani kilikuwa ni bei rahisi mno.:closed_2:
 
Sishangai .............tembelea mtandao huu (www.163.com) uone vile wengi tunakula mizoga katika "supermarkets" kutoka China, Japan, Hong Kong na kwingineko
 
Karibu na soko la Wakulima Njombe; kwa hali hii nahisi na mimi nimekula nyama ya mbwa au nishakula nyama ya mnyama huyu kwa kuishi kwangu Njombe bila kufahamu.

Pole sana aisee yani hata kama ni IRINGA lakini kumlisha mtu MBWA bila idhini yake ni hatari, Wewe chukulia hujalishwa utakaa kwa amani.
 
Back
Top Bottom