African Barrick/TBC hawatambui haki za wagonjwa?

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
ABG na GGM wameleta wataalam wa upasuaji nchini kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji wagonjwa wa 'mdomo wa sungura' huko kanda ya ziwa (source: TBC Habari).

Tatizo langu ni kurusha hewani wagonjwa wakiwa wanafanyiwa upasuaji, I wonder kama wana ridhaa ya wagonjwa (ambao wengi ni watoto wa chini ya miaka 10) ili kurusha hewani picha kutoka chumba cha upasuaji.

Dhahabu mumeichukua, sawa. Ingawa mnatudanganya na hivyo viupasuaji ambavyo mi-VX ya serikali ingeweza kugharamia, basi heshimuni haki za wagonjwa kwa kujali faragha zao.
Aaaagh!
 
Brother njaa mbaya sana.
As longer as wanatoa msaada wa matibabu basi 'wanatakiwa' wafanye lolote wanalojisikia.
 
Wasipowaonyesha watatimizaje azma yao ya marketing in the name of CSR. Kwanza am sure wamepata free airtime kukuza company reputation
 
naunga mkono hoja!usiri wa wagonjwa lazima uheshimiwe.huu upasuaji ungeweza kufanywa na wataalamu wa hapa nchini,waache kutuzuga.
 
Brother njaa mbaya sana.
As longer as wanatoa msaada wa matibabu basi 'wanatakiwa' wafanye lolote wanalojisikia.

mimi nadhani ABG wanataka kupata huruma ya wananchi, wafunike skendo za kulisha watu sumu, kutelekeza wafanyakazi wao walioumwa wakiwa kazini na kubwa zaidi la kuzorotesha maendeleo ya taifa kwa kuchukukua dhahabu kwa mrabaha mdogo.
Cha huzuni ni kuona kituo cha televisheni cha serikali ndio kinatumika kutupaka 'lube' ili watutumie vizuri.
 
Wasipowaonyesha watatimizaje azma yao ya marketing in the name of CSR. Kwanza am sure wamepata free airtime kukuza company reputation

Kitambo kidogo walionesha dokumentari fulani inayohusu mambo haya, ila hawakufika mbali hivi, walionesha tu picha za watu kabla ya upasuaji, ile michakato ya awali ikiwemo safari za wagonjwa kuja Darisalama na mwisho wakaonesha wakiwa wameshapona, hakukuwa na video za chumba cha upasuaji, tena wakati mgonjwa akipasuliwa...
This time they've gone beyond the line, I wonder hawa kina Sakina Datoo wako wapi?
 
Back
Top Bottom