Africa Cup of Nations (AFCON) 2017, Special thread

Naona kama Michuano hii Siku za karibuni imepoteza Mvuto Sijui shida nini Caf wafanyefanye mambo ile ladha yake irudi.

Nakumbuka ile Fainali 2000 Nigeria Vs Cameroon muda wa Kawaida tokeo 2-2 Nigeria anakuja kufa kwenye Matuta 3-4 Kanu na Ikpepa wanakosa mikwaju yao ile ndo ilikua Fainali Kwa kweli, Daa hata msosi Sikula manake nlikua team Nigeria ila round hii ntawamiss Nigeria

Baada ya Misri ya Shehata kuanza kubeba Kombe ile ya kulifuatilia ikaisha Mpaka Zambia Anakuja kubeba tena chini ya Kina Mweene,Mayuka,Katongo,Sunzu

Ntawapa Shavu Uganda Msimu huu
Misri haikuwa inashiriki kaka subiri ya mwaka huu uone
 
Mie timu zangu ni:misri,algeria,moroco,tunisia,
all maghreb countries!

Mkuu hebu acha za kizamani hizo.

Sasa all magharibo countries unashabikia kweli.

Mimi naamin huwez kuwa shabiki wa zaid ya timu mbili tena hiyo ya pili itakuwa ikikutana na ile ya kwanza unaikana

Sasa wewe zaidi ya nne hata ushabiki na utani ule udambwi udambwi wa soka unakuwa huna.
 
Ha haaa Akhui hao jamaa uliyowataja walikuwa ni balaa aise, ni moto wakuotea mbali...bila kuwasahau akina Abou trika, mohd shawki, hossam ashour, ma-defender wael gomaa, sayed mouwad n.k...misry bana ilijaaliwa kwa wachezaji....na ndiyo tim niliyokuwa naipenda sana hapa Afrika.....
Naam captain wao hassan ghaly kina mohamed shaban hao wafereji sio mchezo .
Lakini Egypt toka zama zile za national el ahaly ya ukweli kina mohamed el khateeb kina majid abdulghany walikuwa na fullback rabii yasini black hivi kina hany ramzi golini alikuwa thabeet el batal wacha mchezo .
 
Nilianza rasmi kuangalia na kujua mpira final ya Senegal sikumbuki na timu gani ila 2002 nadhani, mpaka penalty zilipigwa siku ile. Ndo ukawa mwanzo wangu wa kuwa mshabiki wa Liverpool na Germany.
 
Ingiwa huwa nashabikia Ghana miaka yote ila mwaka huu ninaonyesha Uzalendo kwa kuishabikia moja ya Nchi za Afrika Mashariki yaani Uganda!

Viva Uganda Cranes
 
Naam captain wao hassan ghaly kina mohamed shaban hao wafereji sio mchezo .
Lakini Egypt toka zama zile za national el ahaly ya ukweli kina mohamed el khateeb kina majid abdulghany walikuwa na fullback rabii yasini black hivi kina hany ramzi golini alikuwa thabeet el batal wacha mchezo .


Swadaqta l'akhy..hao walikua mashine si mchezo..

Misry ilikua inaheshimika mno,soka lao lilikua la kipekee sana Afrika...kwa sasa tunaiona Algeria ikishambulia zaidi mpaka mjerumani alitokwa jasho w/c...ngoja tuone AFCON ya mwaka huu itaamua vipi...
 
Misri haikuwa inashiriki kaka subiri ya mwaka huu uone


Hata mimi navyoona mafarao watafanya wonders, ....kwanza anahasira mno kutoshiriki mashindano, ngoja sasa kazi inaanza, na heshima irudi...

Hawa washkaji weka mbali na watoto, hofu kwangu ni ALGIERS! ila hata yeye atamezwa tu:D
 
Back
Top Bottom