Afisa wa TRA mbaroni kwa kuomba rushwa ili asaidie ukwepaji wa kodi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282

Ofisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38), anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh milioni 50 na kupokea Dola za Marekani 1,000 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi na kujaza taarifa za uongo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba ushwa kwa mfanyabiashara Raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya HEM Heavy Equipments Company Ltd.

Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara huyo kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

“Kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000 ili aweze kumsaidia mfanyabiashara huyo.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000).
 
Jamaa boya kweli. Matangazo yote hayo kuhusu kushikwa,kutegeshwa bado anaomba rushwa? Usimuamini mtu kabisa. Kuharibu career yako kwa million 50 tu ? Haya aende anapostahili.
 
OFISA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elias Yunus(38), anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50.

Elias inadaiwa aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mfanyabishara raia wa Uturuki ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hem Heavy Equipments baada ya kumtuhumu kwamba ametoa taarifa za uongo.

Inadaiwa raia huyo alitoa taarifa za uongo kwa ofisa katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo, alisema uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kwamba Ofisa huyo aliomba rushwa ya kiasi hicho na baada ya majadiliano alipunguza hadi kufikia Tsh. Milioni 35.

Ngailo alisema masharti ya fedha hizo zilitakiwa kupewa zikiwa katika dola za Marekani 17,000.

"Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kupokea kiasi cha dola za Marekani 1,000 kama sehemu ya rushwa pia alikutwa akiwa na nyaraka mbalimbali za TRA alizokuwa anampelekea mfanyabishara huyo," alisema.

Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma umekamilika na atafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili.

Ngailo alitoa wito kwa watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani madhara yake ni hasara kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

"TAKUKURU inatoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati huu ambao tunakwenda kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu," alisema.
 
Ametuhumiwa bado hajahukumiwa Mpendwa katika Bwana
 
Kabila gani huyo jamaa?
 
Elias rafiki yangu ila ndio hivyo ajali kazini.

Nisiongee sana wakaja kutumia maandishi Yangu kama sehemu ya ushahidi.

Ila namkubali sana huyu mshikaji nitaenda kumtembelea gereza lolote atakalowekwa.
 
Katika kipindi hiki kama wewe ni mla rushwa hutakiwi kua mtu mwenye tamaa i.e kama anaetoa rushwa hajaridhika usilazimishe ukilazimisha lazima mambo kama haya hutokea
 
Back
Top Bottom