illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,119
heshima kwenu,
Sisi watumishi wa wilaya ya Muheza kulia kwetu ni kitu cha kawaida sana huwa tunashangaa hivi huyu ofisa utumishi hii wilaya ni ya kwake ama ana fanya kazi ya serikali?
kwa kweli naomba mwenye kujua hatua sahihi za kufuata au sehemu ya kuripoti atujulishe tumejaribu kuingia kwenye mtandao wa utumishi sehemu ya malamiko ambapo inabidi u sign up lakini naona kama mtandao haufanyi kazi kifupi ni kwamba huyu mama hataki kuwapandisha watu vyeo kuna watu walianza kazi na ngazi ya vyeti wakajiendeleza mpaka ngazi ya degree lakini bado wanamshahara wa ngazi ya cheti kutokana na unyeti wa taarifa hii nashindwa kuwaandika majina na ushahidi kwani inaweza kuharibu huu uhusiano wa kinafiki tulionao.
cha pili ni kwamba mtu anapo onyesha jitihada za kudai haki au kufuatilia madai yake wiki inayofuata mtu huyo atakuwa na wakati mgumu kwani atamfuatilia na kuhakikisha anamlima barua anaitwa mama mwilongo majibu yake ni ya mkato na ya ukali sasa jamani sisi watanzania tumesoma kwa gharama ili kuisaidia nchi yetu na kujiwezesha kiuchumi halafu serikali inakubali kweli tuichukie nchi yetu kwa ajili ya huyu "malkia" isitoshe tunafanya kazi huku vijiji kwenye mazingira magumu mtu kama mimi nina degree yangu ni mtu wa kulipwa laki mbili na nusu kweli.
mwanzo ilikuwa unapo maliza masomo unapewa barua ya uthibitisho na kupandishwa cheo na ngazi ya mshahara watu lakini inabakia maandishi tu bila utekelezaji ambapo utaongezewa tu majukumu ya kazi bila marekebisho ya mshahara. watu walikuwa wanaenda kulalamika kwa kutumia barua za uthibitisho.
sasa hivi amegundua mbinu mpya ambapo ana kupandisha cheo bila maandishi huwezi kukataa kwa sababu kesho yake hata uki banja kwenye kikao utalimwa barua ya kujieleza eti kwa nini unakuwa msumbufu wakati kikao kinaendelea .
yaani kwa kweli ukisikia mtu ameitwa kwa ofisa utumishi kule bomani lazima arudi na machozi du kweli hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo