Afisa NSSF apigwa na vibaka Kimara

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Taarifa za ndani zinadokeza kuwa afisa mmoja wa NSSF (Bw. Kinunda) amejeruhiwa na kulazwa hospitali ya Aga Khan baada ya kupigwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka huko anakoishi Kimara. Kwa muda sasa wakazi wa maeneo ya Kimara wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi hasa baada ya kuongezeka kwa wimbi la vitendo vya ujambazi.

Kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya kuaminika Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama vimejikuta vikiziwa ujanja na makundi ya vibaka na majambazi na kuwaweka katika hali ya kushindwa kujibu mashambulizi ya uhakika huku ukusanyaji wa habari za kiintelijensia ukiwa duni katika maeneo mengi ya Jiji la Dar.


Hadi hivi sasa haielweki kama vyombo hivyo vina uwezo wa kupambana na vibaka hawa ambao wanaoekana kujenga vibanda katika maeneo mbalimbali nchini. Kama hali hii inaendelea wananchi wanaweza kuanza kuhusisha usalama wa mitaa yao na wale walioko madarakani au wale wanaotaka kuchaguliwa.
 
Hawa ndio kati ya wale elfu tatu waliopewa msamaha wa Rais...

Nampa pole sana jamaa yetu na tunamuweka kwenye maombi, Mungu atamsaidia...

Suala la Vibaka limekuwa tatizo kubwa sana, sio Kimara peke yake, ni maeneo yote na hali itaendelea kuwa mbaya zaidi...
 
Kimara na Mbezi ya Kimara ujambazi na vibaka wamezidi. Kibaya zaidi lazima wakukate mapanga au wakuue, ndiyo tabia yao. Polisi wanatakiwa kuimarisha ulinzi maeneo haya. Hata hivyo pia wenyeji lazima watakuwa wanawafahamu jamaa hawa. Kuna watu wameamua kuyakimbia majumba yao huko au unaweka grill zito kama la jela Segerea. Wana bunduki hawa jamaa wanaweza tu kuamua kufunga mtaa, wanapora, wanaua, wanakata watu mashoka na mapanga. Very sad indeed. Pole ndugu Kinunda.
 
Baba Kova upo? Unyakumbuka maneno ya yule mtumishi wa Mungu wa Kimara Mavurunza?? Unasubiri nini kuwapisha watu wengine?
 
tatizo la huko polisi hasa wa pale Kimara na Mbezi kwa Yusufu, wanawasupport hawa vibaka. hata mkiwapeleka wezi the next morning utamwona mtaani au anaambiwa asafiri kidogo kisha arudi. Tatizo ni mfumo wa jeshi lenyewe.
 
Back
Top Bottom