Afisa mstaafu wa JWTZ amiliki Tsh 50 bn nje

Kuna kigogo(Jina tunalihifadhi kwa maslahi ya umma) anamiliki mabilioni(Kiasi tunakihifadhi kwa maslahi ya umma) ni mstaafu(Taasisi tunahifadhi) Habari na Mwandishi wetu.

Nyambafu!! No research No Right to speak! wana JF tupiganie MwanaHalisi lifunguliwe.
 
Siasa za kitoto hizi.
Kelele zote zile za kuitisha serikali kumbe niza hii hadithi ambayo ilikosa ushaidi ikaishia kupigwa komeo.Alichofanya Zitto ni kubadilisha namba ili iweze kufafana na ukweli.
Hii inanikumbusha ile ishu ya kutokuwa na imani na waziri ambayo iliwa ni sawa na kujaribu kutwanga maji kwenye kinu
 
Zitto kama ana ubavu awataje basi sio kutishia nyau.Tumechoka kauli za kutishia nyau anatuona sisi watoto wadogo tena mbumbumbu??
Kama hana uhakika bora afunge domo lake.
 
GAHU mnamkumbuka? jamaa ana bahati sana. Alikomba sana pesa ya jeshi enzi za WAITARA lakini hakuna anayemtaja, ingefaa TAKUKURU wawamulike hawa nao.
 
maafisa wa jwtz waliostaafu ni wengi taja ni nani au huyo zzk mzushi tu kutaka kuwafurahisha cdm
 
Usually when people are sad,they dont do anything,they just cry over their condition,but when people get angry they bring about A CHANGE
KINACHOMTOA MACHOZI MGOMBEA URAIS WA CHADEMA ZITTO KABWE AMBAE KESHAANZA RASMI KAMPENI ZAKE NI KIPI??YEYE PIA NI FISADI SEMA TU SLAA ALIJISKIA AIBU KUMTAJA PALE MWEMBE YANGA
:frusty::frusty:
 
tetesi wakati mwingine ni mbaya sana kwanini zito asimtaje tu kuliko kuwaacha watu wakihisi humu? ni mboma? shimbo? who?
 
..kama Shimbo anamiliki mabilioni yote hayo, je Mwamunyange,Hussein Mwinyi,na JK, wanamiliki bilioni ngapi?

..binafsi siamini kama Mnadhimu Mkuu wa jeshi anaweza kuwa na confidence ya kuiba mapesa yote hayo, kama wakubwa zake na wao hawashiriki ktk wizi wa namna hiyo.
 
Mh Zitto Kabwe amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la 01 Okt kuwa katika yale matrilioni ya pesa zinazomilikwa na vigogo kwenye akaunti zao nje ya nchi, mmojawao ni Afisa wa JW TZ mstaafu.

Huyo mzee lazima atakuwa 60 + yrs, atazifanyia nini pesa hizo alizotuibia ktk umri huo? Anawatafutia laana tu watoto na wajukuu zake watakaorithi mapesa hayo!

Kuna kigogo mmoja wa JW TZ aliyestaafu hivi karibuni, alituhumiwa humu JF kuwa amepokea mabilioni kwa ajili ya Askari waliopo UN mission nje na kuhifadhi nje.
Unaweza kukuta yeye hapo ana Million100 tu zingine zinawenyewe zinasubiri uchaguzi, haingii akilini kwamba serikali imeshindwa kuwabana mbavu hao watu na kurudisha mabilioni yote hayo ili zisaidie kunusuru uchumi wetu unaoteteleka kila siku, inaniuma sana mpaka sasa watumishi wa umma kibao hawajapata mishahara.
 
Ile thread ya Invisible,sikuamini kama alikurupuka licha ya kwamba ilifutwa.

BTW hivi General Ngwilizi ni mstaafu?
 
Kuna member mmoja anatumia username ya de'levis aliwahi kuleta uzi mkali sana juu ya hizo pesa za shimbo lakin thread ile hakikudumu ikaondolewa....
 
Last edited by a moderator:
Jamani Shimbo amestaafu, niliwahi ongea kwenye uzi mmoja wapo hapo nyuma kuwa kama kuna ushahidi sasa utolewe au tumemwache mzee wa watu apumnzike. Kashfa ya kwanza mlisema ana 3 trilion south africa wakati bajeti ya jeshi zima na kila kitu hata bil 800 hazifiki. Leo mnasema ana bil 50 tushike lipi? haya ni majungu na ukosefu wa adabu kwa askari muaminifu kama Lt.Gen. Shimbo. Toeni ushahidi au mwacheni apumzike
 
Jamani Shimbo amestaafu, niliwahi ongea kwenye uzi mmoja wapo hapo nyuma kuwa kama kuna ushahidi sasa utolewe au tumemwache mzee wa watu apumnzike. Kashfa ya kwanza mlisema ana 3 trilion south africa wakati bajeti ya jeshi zima na kila kitu hata bil 800 hazifiki. Leo mnasema ana bil 50 tushike lipi? haya ni majungu na ukosefu wa adabu kwa askari muaminifu kama Lt.Gen. Shimbo. Toeni ushahidi au mwacheni apumzike
Mwaminifu kwa majambaz wenzie CHAMA CHA MAJAMBAZI(C.C.M)
 
Back
Top Bottom