Afande Sele amchana Sugu, adai hajafanya lolote bungeni kutetea muziki, Sugu ajibu

" Mara natupa shuka nastuka naona sugu ananiitwa ..ananiambia mziki bongo haulipi mwanangu ni nabanduka....maana bila sugu hapa nilipo nisingefika...waaatu nazo pesaa wewe zinakutesa Mimi zinanitesa peesaa!!" Maneno ya afande hayo.

Heeh Leo anamponda mentor wake daah?
 
Dhamana lawama! hata angeingia yeye asingeweza kuzikwepa haziepukiki! Sema kidogo na Sugu alisahau alikotoka alikuwa na uwezo wa kumobilize vitu fulan hivi na ku push forwad vifanyiwe kazi na wenzie waone kuwa jamaa anakumbuka alikotoka! wanashida nyingi sio za hela supervisions na hatimiliki! sheria haziwalindi Sugu + Basata angeweza kufanya kitu!

Ingawa mwenyewe anasema yeye ni mbunge wa Mbeya na sio mbunge wa wasanii ni kweli, lakini pia kama unalivyoandika mkuu, ni kweli bwana Sugu alijisahau na akuonesha hata kukumbuka kule alipotoka i mean kwenye maisha ya kimuziki.
 
Sele vs aboud?? Afande anapoteza energy+time, aboud anakubalika sana hata km akisimamisha jiwe vs sele, aboud atashinda kwa 99.1%
 
Wasanii mjitume muache kusubiri "lift" za wanasiasa. Bila Sugu kugombea ubunge na kushinda, huu msururu wa wasanii watangaza nia tunaouna usingekuwepo akiwepo Afande Sele mwenyewe. Huo ni mchango tosha wa Sugu kwa wasanii, kawaonyesha njia mnayojaribu kuifuata sasa.
 
Ingawa mwenyewe anasema yeye ni mbunge wa Mbeya na sio mbunge wa wasanii ni kweli, lakini pia kama unalivyoandika mkuu, ni kweli bwana Sugu alijisahau na akuonesha hata kukumbuka kule alipotoka i mean kwenye maisha ya kimuziki.
. Kwa mfano mlitaka afanye nini ili tuwe na mtazamo kama wako?
 
Wasanii hao wanafiki tu maana kampeni wanafanya huko ccm sasa wanamlalamikia sugu mm nasema ukweli wasanii wa bongo movie na wamuziki na walimu ndiyo ilikuwa wapuuzi wanaisaidia sana ccm wakati wa uchaguzi lkn baada ya uchaguzi wanakuwa vidampa tu hawana thaman kwa ccm sasa mwaka huu wakome kuishabikia ccm majukwaani ili wawe upande wamadiriko kama sugu,au profesa j. Lkn akina mpoto mmmh waache tu
 
sugu aliingia kwenye siasa kuwatumikia wananchi,Sele ameingia kwenye siasa kumfata kumtumikia zito.Zito akihama chama na Afande sele anahama.hizi ndio tabia za kwenda bungeni kusema Ndioooooooooooooo kwa kila hoja!
 
Hizi Siasa za Kibongo bongo ni Siasa za Kisanii Viongozi wetu wengi ni wasanii na hata baadhi ya Wabunge ni Wasanii watupu hatuna viongozi wa ukweli wana haki ya kutupiana maneno kwa sababu wote ni wasanii watupu hakuna kiongozi hapo.
 
Nahisi hata (ikitokea akapewa ridhaa ya kuwa mbunge) kila atakapokuwa anaelekea kujisaidi aja ndogo pale bungeni, huko huko msalani atakuwa anavuta bange kwanza.
Kwani Afande Sele anayajua majukumu ya Mbunge dhidi ya serikali.!
 
Nimefurahia majibu ya sugu kwani yeye hakuchaguliwa na wasanii. Pia ameonesha ukomavu kisiasa kuwa wasanii sio wahuni bali watu wenye mawazo ya kujenga na kuisimamia serikali!
 
Sugu alichaguliwa na wananchi wa Mbeya & aliwakilisha Wana Mbeya. Hao wasanii waache unafiki, ni lini walijitokeza kumpigia kampeni? Walishinda kwenye majukwaa ya kijani, sasa leo wanalalamika nini.

Elimu inasaidia kumbe, Too low kwa afande. Asubiri yeye akawakilishe wasanii wenzake, Sugu atawakilisha wananchi wa Mbeya kwa kuwa ni mbunge wa Mbeya, sio mbunge wa wasanii.
 
Wasanii wangejitambua kwanza kabla ya kuanza kuwatupia lawama wabunge kama akina Mbilinyi na wengineo.

Kila siku wanagombana na kulogana sasa nani wa kuhangaika nao bana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom