Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,802
- 71,229
Tunafahamu kuwa watumishi wote wa Umma ambao ni Viongozi na wapo Madarakani kwa kupigiwa kura (kupitia uchaguzi) waajiri wao na mabosi wao ni sie Wapiga kura wananchi wa nchi hii.
Sheria za kazi na mahusiano kazini zinatamka kuwa Mtumishi asipohudhuria zaidi ya siku 3 mfululizo na bila taarifa yeyote kifuatacho ni kufukuzwa kazi moja kwa moja naMwajiri wake!
Sasa inakuwaje kuna viongozi wanakosekana kazini zaidi ya mwezi na hakuna taarifa nasi kama waajiri tuko kimya kiasi eti mtumishi huyo anarudi toka mafichoni kisha anamfokea mwajiri kwa kuulizauliza aliko?
Au sheria hiyo haiwahusu viongozi wa kuchaguliwa? Kwamba anaweza kuchaguliwa 2025 kisha akaondoka kuishi Ukraine kulima ngano na kurudi 2029 karibu na uchaguzi na tusiulize? Au tukiuliza tunaambiwa tutashughulikiwa huku tukifokewa?