Aden rage asimamishwa na kamati ya utendaji ya simba

Mzee itang'are umeambiwa Kaimu nafasi ya Kaburu we unaleta mapinduzi? Si usubiri uchaguzi ugombee na wewe uone kama wanachama watakupa ridhaa yao!! HIZO NI FUJO!! Anyway tumsubiri Rage nini atasema...
 
Sio Rage tu inasemekana hata wasimamizi wa mazoezi ya simba[julio na king] nao wamepigwa chini.
 
kwa uelewa wangu kamati ya utendaji ipo chini ya Rage! Mwenye mamlaka ya kuitisha kikao cha kamati tendaji ni Rage, sasa ya wao kumvua labda kuna kitu chini kapeti! Time wil tel

Hapa ndio hata mimi sielewi bado hii habari. Si inatakiwa basi kamati yote ya kamati ya utendaji ivunjwe?
 
aaaaaaah mimi sina comment yoyote.!bali nasubilia maneno ya shombo ya alhaji,naju ntacheka tu kwaninavyo mjua michezo ya leo sikosi ha ha ha ha haaaaa...
 
Jioni hii kupitia enewz za eatv mzee kinesi athibitisha kuwa kamati ya utendaji kisheria imewasimamisha rage na makocha wote 2: King na julio.
 
Alitaka kuleta siasa za CCM mpaka katika soka la simba,kubwa ni vile alivyopeleka timu kucheza mechi kule kwa mwigulu NcheMba ili kudhohofisha mkutano wa slaa.
 
Source: jane blog

Kamati ya utendaji ya simba imemsimamisha mwenyekiti wa SIMBA RAGE na kuwafukuza makocha wote wa simba JULIO na KIBADENI.

Kaimu mwenyekiti wa Simba JOSEPH ITANGIRE amesema maamuzi hayo yamefikiwa na kamati ya utendaji ya simba hivyo wanachama wa simba siku ya mkutano mosi Desember ndiyo wataamua arudi au asirudi kutoka na kura zitakavyopigwa .

RAGE amesimamishwa baada ya kukiuka utaratibu wa kufanya mkutano November yeye akajipangia Desember wakati makocha wameshindwa kufanya vizuri mzunguko wa kwanza hivyo timu itakuwa chini ya Suleiman matola na kocha aliyekuwa anafundisha Gol maiya ya Kenya zamani
 
Wakati wa Field Mashow Hassan Dalali umewadia.Chini ya Rage tumeteswa sana na wasomali wa Yanga,Bin Khleb na Manji,wwanajitwalia wachezaji wetu kama simba mwenye njaa anavyoshika swala serengeti.Mara Twite,Yondani,Bathez,shaban Kondo,Kaseja nk.Sasa watamchukua yeye Rage mwenyewe,

Ha ha ha ha ha ha teh teh teh ..............................
 
unajua mwenyekiti yupo nje ya nchi kwasasa, sasa hawa jamaa huwa wanavizia Rage aende nje ya nchi ndo wampindue hapo ndo huwa wanakosea! Wanapaswa kumvaa akiwepo

Umeona eeh kama namuona siku atakapo rudi atawashushua kama kawaida atasema kikao chao ni KITCHEN PARTY....hila ukweli huyu ni janga la Taifa ametucost ata sisi YANGA kumbe alisaini mkataba wa AZAM bila ridhaa ya kamati tendaji, naamini Yanga na Simba zingekuwa kitu kimoja kwenye hili wangepata maslahi makubwa.
 
Jioni hii kupitia enewz za eatv mzee kinesi athibitisha kuwa kamati ya utendaji kisheria imewasimamisha rage na makocha wote 2: King na julio.
tujaalie katiba ya Simba inaruhusu kikao cha Kamati tendaji kuitishwa na kuendeshwa bila ya kuitishwa na kusimamiwa na mwenyekiti. Lakini je, kikao kilichoitishwa kwa namna hiyo bila ya kumhusisha mwenyekiti (ndivyo inavyoelekea) kinawez kupitosha ajenda nzito kama ya kumfukuza mwenyekiti huyo? Simtetei Rage wala nini, ila nachelea waije wakashindwa mara ya pili kumn'goa kwa sababu tu ya kukiuka katiba yao wenyewe. Na kama ni hivyo, wanastahiki waumie kwa kuongozwa naye. Iweje viongozi wazima hawaijui katiba yao wenyewe? Na kama wanaijua, kwa nini hawajiamini kwa kumkabiili ana kwa n kwnye kiko ambacho Rage mwenyewe watamtaka awepo? Wanamwogopa nini iwapo wana hoja za msingi?
 
Ngoja arudi, atakwambia hatambui maamuzi hayo, kikao kilichao kaa hakikuwa na uhalali ( send off)
 
kwa uelewa wangu kamati ya utendaji ipo chini ya Rage! Mwenye mamlaka ya kuitisha kikao cha kamati tendaji ni Rage, sasa ya wao kumvua labda kuna kitu chini kapeti! Time wil tel

nipo pamoja na ww jana wakati tupo uwanja wa Taifa tukitazama mechi ya timu ya taifa na Zimbabwe Rage alipigiwa simu akajibu kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali wa Simba kwa sababu kikao kilichokaa kumsimamisha ni batili kwa mujibu wa katiba mwenye mamlaka ya kuitisha kamati ya utendaji ni mwenyekiti na makamu wake,simba mpaka sasa haina makamu mwenyekiti aliepo ana kaimu hana mamlaka ya kuitisha kamati ya utendaji inamaana wamekiuka katiba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom