ACT - Wazalendo yazidi kupata wananachama toka CHADEMA

PHILIPLULINDA

Senior Member
Jun 1, 2013
181
89
ACT - Wazalendo yaendeleza yabomoa ngome ya CHADEMA baada ya alikuwa mgombea uenyekiti cha kwembago kuhamia ACT - Wazalendo, ni mwendelezo wa wapenda amani kujiunga ACT - Wazalendo.

Akijiunga ACT - Wazalendo mwenyekiti huyo ndugu Henry alisema kaamua mwenyewe kwa moyo mmoja na Anasema Sasa ni kufyeka mapori na kuondoa magugu ya vyama visivyo na Sera madhubuti kama za
ACT - Wazalendo. Aliwaomba wote wenye mapenzi mema na nchi wajiunge ACT - Wazalendo.
 
Unapost jambo moja mara kumi kumi, we mfuasi wa wasaliti!
 
Hahahaha Lushoto nilipozaliwa mimi au sehemu nyingine? ACT itafutika kama ndugu yake CCJ
 
Shame zitto...
Eti ulikuwa kamati za bunge PAC kuisema ccm...
Say it now....thru ATC
Living dead
 
act ni kijikundi cha wahuni wa mwandiga wakifadhiliwa toka lumumba
 
ACT wazalendo yaendeleza yabomoa ngome ya chadema baada ya alikuwa mgombea uenyekiti cha kwembago kuhamia act, ni mwendelezo wa wapenda amani kujiunga act. Akijiunga ACT wazalendo mwnyekiti huyo ndugu Henry alisema kaamua mwenywe kwa moyo mmoja na Anasema Sasa ni jufyeka mapoli na kuondoa magugu ya vyama visivyo na Sera madhubuti kama za ACT. Aliwaomba wote wenye mapenzi mema na nchi wajiunge ACT.


Kwahiyo objective yenu kuu ni kupambana na CDM?
 
Tatizo sio kupata wanachama, tatizo kuwashawishi wakupigie kura!!!!!! hizo kadi mbona mnaweza mkawa mnazigawa buree tuu wanapokea kura kaangalie kwenye sanduku alafu mwuulize mrema alikutaje mwaka ule.??
 
Kila kitu CDM,hovyo kabisa ACT,naona kazitto bado kana hasira na Chadema,Kweli haka kachama nikawaliti hawapati usingizi bila kuitaja chadema.Swine!!!!!!
 
Naona wanaojiunga ACT wanatokea Chadema tu wala sio vyama vingine. Hamna shida endelea tu kuandika ili mpate ruzuku kutoka kwa chama mama CCM.

Mkilogwa siku moja mkaandika kwamba kuna mtu ametoka CCM kuingia ACT, huo ndio utakuwa mwisho wenu.

Tiba
 
Kwa takribani miaka mitatu ndani ya CHADEMA nikiwa moja ya masalia ambaye jina lake halikufahamika, nilioshiriki mikakati mingi sana ambayo ilikuwa ni kuwapindua Dr. Slaa pamoja na Mbowe kwenye uongozi wa CHADEMA huku tukiamini kwamba, CDM ilikuwa na ubaguzi, ukabila, pamoja na udini. Nilibakia ndani ya CDM hadi pale ACT ilipoanzishwa. Tuliamini kwamba ACT ingekuwa wokovu kwa watanzania na mbadala wa CDM na CUF katika kuleta upinzani wa kweli na mabadiliko ya kumkomboa mtanzania.

Watanzania wenzangu, mtaniwia radhi kama ntawakwaza. Nimegundua madudu ya ajabu sana ndani ya ACT. Ni chama kilichoanzishwa kwa kusudi maalum la kudhoofisha upinzani nchini. Ni chama kilichojaa watu wenye uchu wa madaraka kama ilivyodhiiriswha kwa Zitto kupewa kazi ya Ayatollah (Kiongozi mkuu). Chama cha walaghai na wala rushwa. Ningependa viongozi wangu ndani ya chama waweke wazi, kwamba fedha zakuendesha chama zinatoka wapi? Kamwe chama tawala hakiwezi kutoa fedha kuendesha chama pinzani kama siyo hila chafu.

Mara kadhaa kwenye vikao vya ndani hatujawahi kujadili namna ya kuking’oa CCM madarakani, tunajadili namna ya kukidhoofisha CDM na CUF mbaya zaidi, Makada wa CCM mara nyingi wanashiriki kwenye hivi vikao vya ndani vya ACT. Ikiwa ni pamoja kupanga bajeti na stategy. Kipindi cha nyuma ilikuwa ni Mwigulu Nchemba, anasaidia, siku hizi ni Nape Nauye

Bila kusahau, Katibu wangu mkuu, Ndg. Samson Mwigamba amesema wazi kabisa kwamba ACT-Itaisambaratisha CUF Tanga na Mtwara. Zitto naye kadai UKAWA ni wasaka tonge. Mwl. Kaiijage na Dotto na team nzima ya ACT na makada wa CCM tunashirkiana kila siku kwenye mitandao tukiishambulia CDM na kusahau matatizo ya wananchi.

Hii ndio ACT.

Jitayarisheni kusikia mengi, natafuta mwanasheria atakayenisaidia kwenye mambo Fulani kisha ntawapandishieni video na audi kadhaa kuonyesha usaliti na mikakati kadhaa ya ACT na CCM tukielekea kwenye ukombozi. Hakuna siku ACT imekaa na kuishambulia CCM, sababu inajulikana na Juliana Shonza, Zitto, Mwl. Kaijage na Dotto watakuwa mashahidi wangu kwani wote tumekuwa tukifanya kazi maalum ya kuishambulia CDM kwenye mitandao kutumia ID tofauti tofauti, na huu ulikuwa ni mmoja wa Mikakati yetu. Mwisho wa siku, Mwigamba kalalia hela zetu

Naomba msamaha kwa watanzania wenzangu kwa kuwa msaliti. Nimeng’atuka rasmi ACT-Wasaliti......


(copying some where act mmoja aungama na kuomba arudi kundini chadema)
 
Back
Top Bottom