ACT- Tanzania: Taarifa kwa vyombo habari

Kama mnavyo fahamu, Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kitafanya mkutano wake mkuu na uzinduzi wa chama mnamo tarehe 28 na 29 Machi 2015.

Katika mkutano Mkuu chama kitapitisha katiba mpya ya chama na kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Chama, Makamu wenyeviti, Katibu Mkuu na Manaibu makatibu wakuu. Pia chama kitachagua wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.

Katika Uzinduzi wa chama tarehe 29 Machi 2015 kuanzia saa tisa alasiri, viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamealikwa.

ACT – Tanzania imemwalika Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kuzungumza kwa niaba ya vyama vya upinzani nchini kuhusu ‘ kwanini Tanzania bado ni nchi masikini na nini cha kufanya kuondoa umasikini’. Pia viongozi wote wa vyama vya siasa nchini, mabalozi wa nchi mbalimbali na wakuu wa asasi zisizo za kiserikali wamealikwa. Uzinduzi utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na radio kadhaa hapa nchini.

Mheshimiwa Samia Nkrumah, Kiongozi wa Chama cha CPP cha Ghana na mtoto wa Rais wa kwanza wa Ghana Osagyefo Kwame Nkrumah amealikwa pamoja na Mheshimiwa Ababu Namwamba, Katibu Mkuu wa chama cha ODM cha Kenya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Kenya. Vile vile ACT – Tanzania inatarajiwa kupata wageni kutoka vyama rafiki vya Ujerumani Die Linke na Umoja wa vyama vya mrengo wa kushoto Progressive Alliance.

Baada ya Uzinduzi ACT Tanzania itafanya mikutano ya hadhara nchi nzima kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Mbeya.

Tukiwa jijini Arusha ACT – Tanzania itahuisha Azimio la Arusha na kuelezea mwelekeo wa kisera wa chama katika kujenga Tanzania mpya yenye kufuata misingi Usawa, Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Demokrasia na Uadilifu.

Abdallah Khamis,
Afisa Habari

0777008686
___________________________________________________________
P.O. Box 105043, House No. 203, Mpakani A Street, Kijiitonyama, Dar es salaam.
Tel: +255 22 277 1103, Mob: +255 763 463740 / 715 784670, Email: acttanzania@gmail.com

Mbona para ya kwanza inapingana na para ya tatu?

Ipi tarehe halisi ya uzinduzi wa genge lenu?
 
mtaandika mengi sana mtasema mengi lakini Dr.Slaa ndo raisi mtarajiwa tunajua roho ya ccm imeshikiliwa na Lowasa ccm msipomtisha ccm itakufa hata mkipitishaji ccm itakufa .

Msome rafiki yako pale juu, anasema waliotoka CCM kwa kukosa kuteuliwa vyama vingine hawafai kuwa viongozi.Ni wanafiki.Maana yake anamsema pia Dr Slaa aliyetoka CCM baada ya kukosa nafasi ubunge.

By the way, ata Doamond Platinum ni Rais wa Wasaaafi, sikuhizi ni ruksa tu mtu kujiita Rais.Nasikia na kuna mwingine anajiita Rais wa Manzese kama Sugu anavyojiita Rais wa Mbeya.

Ruksa
 
Hao wajerumani msahau kabisa, hakuna anayeweza kuja kupoteza muda wake kusikiliza wahuni wakiongea kihuni tu... Sana sana mtampata huyo sjui Kwame Nkurumah mdogo na huyo katibu wa ODM kwa kuwa ni marafiki na Zitto.. Lipumba atakuja sababu mmempa heshima na mmejishusha chini aje awafundishe siasa za kistaarabu sio za majungu na fitina..

Kila la kheri wafitini, nikiamini lengo la kuanzishwa kwa chama litakufa kabla halijaanza.. Na ndio utakuwa mwisho wa mwanzo wa "mzalendo"... Huyo jamaa atatumia mpaksa senti ya mwisho lakini hawezi kujenga chama mwishowe atastaafu na kusema ameamua akafundishe Ujerumani... hahahah.... Sjui ataenda kufundisha nini, labda civics..
 
Mbona para ya kwanza inapingana na para ya tatu?

Ipi tarehe halisi ya uzinduzi wa genge lenu?
Ungesoma kwa makini ungeelewa maana ipo wazi mno.

Kuwa Mkutano unaanza tarehe 28 na utaendelea tarehe 29/03 ambayo pia itakuwa siku ya uzinduzi.
 
Mbona para ya kwanza inapingana na para ya tatu?

Ipi tarehe halisi ya uzinduzi wa genge lenu?

Sio tatizo lako,elimu yako ndogo ndo. Tatizo,yeriko nahisi una ubongo wa mbu kabisaa, wewe ni chadema huku inakuhusu nini,au unataka ualikwe?ACT wanaalika wasomi kama professor lipumba,mdee,mbatia na profesor beregu,wewe utaishia kupaste thread za watu humu mitandaoni mpaka uzeeke,
 
Hata nbuyu ulianza kama mchicha ACT Tanzania inasonga mbele kwa mbele na kelele za Chura hazimzuii N'gombe kunywa maji
 
Mawakala wa Mijizi ya Escrow na rasilimali zingine za Umma wanaweweseka kisikia Chama ambacho kinapinga ufisadi kwa vitendo,wanatumia kila hila kuzuia hawa ili wasishughulikiwe.

Hakuna kitakacho wafanya muwe salama zaidi ya kuacha matumizi mabaya ya rasilimali za umma na kiacha wizi Kabisa.

ACT iendelee kusimami misingi ambayo vyama vingine vimeshindwa kuisimami.

Adui wa ACT sio chama chochote cha siasa bali ni Fisadi yeyote anaefukarisha taifa.
 
Hao wajerumani msahau kabisa, hakuna anayeweza kuja kupoteza muda wake kusikiliza wahuni wakiongea kihuni tu... Sana sana mtampata huyo sjui Kwame Nkurumah mdogo na huyo katibu wa ODM kwa kuwa ni marafiki na Zitto.. Lipumba atakuja sababu mmempa heshima na mmejishusha chini aje awafundishe siasa za kistaarabu sio za majungu na fitina..

Kila la kheri wafitini, nikiamini lengo la kuanzishwa kwa chama litakufa kabla halijaanza.. Na ndio utakuwa mwisho wa mwanzo wa "mzalendo"... Huyo jamaa atatumia mpaksa senti ya mwisho lakini hawezi kujenga chama mwishowe atastaafu na kusema ameamua akafundishe Ujerumani... hahahah.... Sjui ataenda kufundisha nini, labda civics..

Naona umeandika kwa pressure sana,huu ni mwanzo tu safari hii mtapakimbia pale ufipani.
 
Malizeni tofauti zenu za ndani kwanza, ndo mje kwa umma. Mnafukuzana kwenye uongozi kila kukicha. Hamueleweki
 
Msome rafiki yako pale juu, anasema waliotoka CCM kwa kukosa kuteuliwa vyama vingine hawafai kuwa viongozi.Ni wanafiki.Maana yake anamsema pia Dr Slaa aliyetoka CCM baada ya kukosa nafasi ubunge.

By the way, ata Doamond Platinum ni Rais wa Wasaaafi, sikuhizi ni ruksa tu mtu kujiita Rais.Nasikia na kuna mwingine anajiita Rais wa Manzese kama Sugu anavyojiita Rais wa Mbeya.

Ruksa
hata EL anajiita raisi monduli
 
​Unaijua sababu ya Mwenyekiti wenu mtarajiwa na wenzie kufukuzwa CHADEMA!? Usiniambie huijui.

Wanataka kuisambaratisha Chadema kivipi???.

Hata Mtei alitoka CCM na kuunda Chadema.. Slaa alikuwa CCM n.k.

Je ni makosa kuhama chama na kuanzisha Chama!??
 
Kwa hiyo walikuwa wanasubiri Zitto afukuzwe kwanza CHADEMA ndo wafanye uzinduzi wao rasmi.

Hiki chama sidhani kabisa kama kitadumu.

We Nyani ni nani aliyekuroga? ivi ukiulizwa uoneshe barua ya zitto kufukuzwa unaweza ionesha? barua valid mpaka sasa ni ya zitto kujiondoa mwenyewe kwenye genge la mahafidhina wabaka demokrasia.

Na bado mtasema sana mwaka huu, ACT -wazalendo wameanza kueneza uzalendo kwa watanzania. Tutajua wanasiasa na wababaishaji wa siasa.
 
Back
Top Bottom