Acheni kuwabana wapenzi wenu sehemu za biashara/kazi

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Hili linaniudhi sana na linafanywa sana na wanaume, utakuta jitu limekaa sehemu ya biashara kama
Cafe n.k Basi kwa kuwa ni mpenzi wake atakaa hapo muda mrefu, tena
mwingine sio mpenzi ndio kwanza anavizia yaani mpaka anakera.
Jamani hebu subirini nje ya ofisi, najua kuna watu wataichukia hii
post lakini kiukweli si tabia nzuri.

Hasa wewe Rafiki yangu X yaani ukitoka tu kazini lazima upitie
hapo na kushinda saa kadhaa hebu wapishe wateja nao wana
muda wao.
 
Wanakaba mpaka penati sio?...pole sana naona anakubania!
Sio kwamba ananibania, mi naona sehemu nyingi tu hasa
za CAFE, watu hung'ang'ania hapo saa kadhaa maana
wakati mwingine si mmoja huwa wengi, wanachoongea hakieleweki
yaani upuuzi tupu.
 
Sio kwamba ananibania, mi naona sehemu nyingi tu hasa
za CAFE, watu hung'ang'ania hapo saa kadhaa maana
wakati mwingine si mmoja huwa wengi, wanachoongea hakieleweki
yaani upuuzi tupu.

Yaani wewe wanachokukera ni nini kama cafe ni ya kwao?
Wanakuwa nje au ndani?..manake sijajua unacholalamikia?
Wanakuzuia usifanye mambo yako? au?..........
 
Abiria chunga mzigo wako hiyo!!! Ukizubaa zubaa utakuta mwana si wako! Lazima mtu ulinde mali zako kadri uwezavyo, watu hawakawii kujisevia!!!!
 
Yaani wewe wanachokukera ni nini kama cafe ni ya kwao?
Wanakuwa nje au ndani?..manake sijajua unacholalamikia?
Wanakuzuia usifanye mambo yako? au?..........
Yaani wakti mwingine utakuta wananong'ona wewe umekaa
unahitaji kuhudumiwa, muda unapotea halafu si hivyo tu
kuonekana mara kwa mara kwa mpenzi wa aina hii kunapoteza
wateja na mvuto wa biashara kiujumla, mi naomba uache tu ndugu
yangu kwani si mtakutana nyumbani?
 
Hiyo hata mimi siipendi.......kuna mmoj niliwahi kumkuta kwenye stationery mpaka inakera .......space yenyewe ndogo yeye ndio kwanza anazidisha maongezi
 
Mtu baki waweza kuona jamaa anakaba penati...lakini huyo anayefuatwa anaweza kuwa anapenda kweli...kiasi kuwa siku asipokuja jamaa kwenye sehemu ya kazi lazima ajieleze why.

Msicheze na kupenda...hizo ni stage ambazo real love nyingi upitia.

Ndiyo inawezekana wanaume wanafanya sababu ya insecurity...lakini kwa wasichana wengi hilo wala si kero kama kweli uliye naye ndiye (kama you are not 'still searching')

Niliwahi angalia movie moja jamaa alikuwa ana date muuza bar (ulaya lol. maana muuza bar bongo kwa wengi ni sawa na malaya)...kila siku anampitia kabla hawajafunga ili warudi pamoja...was so sweet.
 
Hili linaniudhi sana na linafanywa sana na wanaume, utakuta jitu limekaa sehemu ya biashara kama
Cafe n.k
Hasa wewe Rafiki yangu X yaani ukitoka tu kazini lazima upitie
hapo na kushinda saa kadhaa hebu wapishe wateja nao wana
muda wao.

Hauna namba ya huyo rafiki yako?
 
haya bana ujumbe umefika.
binafsi bado sijaona tatizo hapo.
Hujui tu, wanafukuza hata baadhi ya wateja
si umeona jamaa hpo juu anasema jamaa anabana
kwenye stationery mpaka inakuwa kero.
 
Mtu baki waweza kuona jamaa anakaba penati...lakini huyo anayefuatwa anaweza kuwa anapenda kweli...kiasi kuwa siku asipokuja jamaa kwenye sehemu ya kazi lazima ajieleze why.

Msicheze na kupenda...hizo ni stage ambazo real love nyingi upitia.

Ndiyo inawezekana wanaume wanafanya sababu ya insecurity...lakini kwa wasichana wengi hilo wala si kero kama kweli uliye naye ndiye (kama you are not 'still searching')

Niliwahi angalia movie moja jamaa alikuwa ana date muuza bar (ulaya lol. maana muuza bar bongo kwa wengi ni sawa na malaya)...kila siku anampitia kabla hawajafunga ili warudi pamoja...was so sweet.
Samahani naomba nitumie neno la mtaani kidogo, 'Kibongobongo'
hii tabia inaharibu biashara.
 
Yaani wakti mwingine utakuta wananong'ona wewe umekaa..unahitaji kuhudumiwa, muda unapotea halafu si hivyo tu kuonekana mara kwa mara kwa mpenzi wa aina hii kunapoteza wateja na mvuto wa biashara kiujumla, mi naomba uache tu ndugu yangu kwani si mtakutana nyumbani?

Yaani kukuuliza yale maswali tayari ushaconclude kuwa na mimi ni mmoja wao?..Mimi kama mtu wangu ana kibarua chake sina muda wa kushinda hapo kazini kwake!!..Lakini na wewe mleta mada kama umeenda ku'surf' tu haya mengine unayashadadia ya nini?...fanya kilichokupeleka!
 
Very true. Mambo ya kuuza sura ofisini kwa mwenza wako hailipi wala nini. Hata kama unaenda kum-pick si umngojee garini? Kuna utani wa ofisini ukiusikia utazimia bureee. Tena kama ndo una roho ya makaratasi ndo utakufa kibudu.
 
inaharibu biashara kama wamekaa na kuwaacha wateja, itaboost biashara kama wote wawili wakishirikiana kuhudumia wateja....

Kweli kabisa... Na tena hata wateja wanafurahia haswaa kuona couples zinashirikiana ktk kufanya biashara. Kama mpngo mzima nikunong'onezana then ujue hiyo couple ndo inaanza mahusiano..so hicho kikubwa wanachoweza kufanya..
 
Itaharibu vipi biashara??? Unless hao wateja wanafuata mengine. Maana kuna wateja hasa wa kiume wanaenda kwenye biashara fulani kwa sababu kuna mrembo....na dawa ya wateja kama hao ni kukaba tuuu. Maana mwisho wa siku nia yao ni kumuimbisha bidada.
 
Mtu baki waweza kuona jamaa anakaba penati...lakini huyo anayefuatwa anaweza kuwa anapenda kweli...kiasi kuwa siku asipokuja jamaa kwenye sehemu ya kazi lazima ajieleze why.

Msicheze na kupenda...hizo ni stage ambazo real love nyingi upitia.

Ndiyo inawezekana wanaume wanafanya sababu ya insecurity...lakini kwa wasichana wengi hilo wala si kero kama kweli uliye naye ndiye (kama you are not 'still searching')

Niliwahi angalia movie moja jamaa alikuwa ana date muuza bar (ulaya lol. maana muuza bar bongo kwa wengi ni sawa na malaya)...kila siku anampitia kabla hawajafunga ili warudi pamoja...was so sweet.

title please
 
Na hamjapenda nyie...mimi mwenyewe hapa pamoja na so many years katika ndoa napenda ingewezekana baba nanii awe nami ofisini muda wote...akae meza jirani hata kama atakuwa busy ana surf...lakini majukumu mengine yanafanya hilo lisiwezekane. Hivyo ni kuwapongeza wenye nafasi ya kufanya hivyo na wanaitumia ipaswavyo.
 
Back
Top Bottom