Acacia yaruhusiwa kuendelea kusafirisha madini kutoka mgodi wa North Mara

Hapa binafsi naona ukakasi inakuwaje Acacia aliyezuiliwa kwa kukosa leseni na upigaji tukaambiwa anahamishiwa Barrik
Leo tena Acacia anaruhusiwa kusafirisha kuna nini nyuma ya pazia kinachoendelea?
Kama nilivyoeleza kwenye jibu lililotangulia, Acacia hajazuiliwa kwa kukosa leseni, bali Acacia ni hatambuliwi na serikali kwa kutokusajiliwa nchini, lakini migodi yake mitatu, Buzwagi, Bulyanhulu, na North Mara inatambuliwa,ina leseni na inaendelea na uzalishaji wa dhahabu na kui export.

Kilichozuiwa ni export ban on makinikia na sio uzalishaji wa makinikia wala uzalishaji wa dhahabu.

Kufuatia Acacia kutokutambuliwa ndipo Barrick akainunua, ila mauziano bado hayajawa finalized, wakati hayo yakiendelea mgodi mmoja wa North Mara ulisimamisha uzalishaji wa dhahabu kwa sababu za kimazingira, sasa ndio umeruhusiwa kuendelea na uzalishaji wa dhahabu na export hadi mauziano yatakapo kamilika.
P
 
Hapa kuna kitu cha muhimu watu wanachanganya, Acacia mwenzi uliopita walipigwa ban kusafirisha dhahabu hadi auditing ya usalama wa mitambo yao ya taka utakapo kamilika, hili halina uhusiano na makinikia ambayo yalipigwa ban muda mrefu.
Nadhani wewe unaongea point sasa, maana hata ukisoma habari inasema walizuiliwa kusafirisha dhahabu kutoka mgodi wa north Mara mwezi uliopita,Hakuna waliposema makiniki, lakini watu wanaongelea makinikia.
Na Pascal anawaeleza kuhusu resolution ya dissolution inayoendelea itakamilika tarehe 3 mwezi wa 9, lakini watu hawataki kuelewa.
 
Awamu hii ni vituko vitupu,uongo,uongo na ubabaishaji wa hali ya juu!......Rais JPM na Waziri Kabudi wamekuwa masterling wa madudu yanayofanywa na awamu hii ya tano.Akina Mayalla ni vibaraka tu ...njaa kali.
Watanzania sio wajinga kiasi hiki jamani!!
Mkuu Miwani ya Maisha, kiukweli Watanzania wengi ni ignorants tuu kama wewe, ni wajinga tuu kwa kutokujua JPM na timu yake wataifanyia nini Tanzania na wanawafanyia nini Watanzania, muda ukifika utaona matokeo ya kinachofanyika, ndipo utaelewa, na ujinga utakutoka. Kama hadi wazalendo kama sisi unatuita ni vibaraka, then ujinga wako ni ujinga uliopitiliza, ila kuwa mjinga ni kutokujua tuu, ukielimishwa ujinga utakutoka.
P
 
nilidhani hatuwatambui na hawana vibali vya kuchimba madini?
Asiyetambuliwa ni Acacia, yeye sio mchimbaji wa dhahabu bali ni mwendeshaji wa migodi, wachimbaji wa dhahabu ni ile migodi yake mitatu inatambuliwa, ina leseni na vibali vyote, inazalisha na ku export dhahabu na inalipa kodi zote.
P
 
Mkuu P, inashangaza.Kampuni haiwezi kuuza share 100% kabla ya baraka ikibidi kikao cha dharula cha wamiliki Emergence General meeting.
Mimi nadhani Acacia ni brand tu ya Barrick kufanikisha tax avoidance.Baada ya Barrick kumalizana na Serikali JV, wanaweza badili jina.
Haijauza shares asilimia 100% bali imenunuliwa asilimia 100 % kwenye a hostile take over na Barrick. AGM imeisha itishwa ni September 3. Acacia ni kampuni Tanzu ya Barrick, sasa Barrick anaingia mwenyewe sio watabadili jina bali inaundwa kampuni tanzu mpya na Tanzania, makao makuu yatakuwa Mwanza, tutamiliki 16%, Watanzania wataingia kwenye bodi na management, na tutagawana economic benefits 50/50
P
 
Maswali yote muulizeni mkabila na mpiga ramli wa jiwe ndugu Mayalla atakuwa na majibu,maana yeye ndiye alikuwa akitupa update za mwisho wa Accacia sasa sijui imekuaje?yani ukabila awamu hii umetawala hata kwa mambo ya msingi.
Mkuu Swelana, karibu upate darsa
.
 
Kuna michezo nyuma ya pazia ambayo sisi tunafichwa. 100% Acacia imenunuliwa na Barick. Wakati huo huo Acacia anaruhusiwa kuendelea na Kazi wakati haexist Tena. Zile billions of money hazieleweki.
It's so funny.
Hakuna mchezo wowote tunaochezewa nyuma ya pazia au tunafichwa kwa sababu wenzetu hawa wako very transparent wanasema wazi kila kitu na sisi tumekuwa tukiripoti humu.

Kwanza sio kweli kuwa Acacia doesn't exist, Acacia does exist ndie mmiliki wa ile migodi yake mitatu ila hatambuliwi, migodi yake mitatu inatambuliwa na uzalishaji wa dhahabu katika migodi yake mitatu unaendelea.

Sasa amenunuliwa na Barrick ila the sale is not finalized, wakati wakikamilisha taratibu za mauziano huku uzalishaji wa dhahabu katika migodi yake mitatu unaendelea.

Zile billions za Noah zetu ni sisi tulisame wenyewe.
P
 
It means that all noises made by our prezda were nothing. And he wanted to fool Tanzanians.
Mkuu Joshydama, no they were not nothing, they are something, sasa tunapata 16% na kugawana 50/50 za economic benefits, this is not nothing, it is something.

Kuhusu ku fool Watanzania, pia sio yeye, yeye alidanganywa yaani he was mislead na akina sisi waona mbali, tulitoa angalizo humu kuwa rais wetu anadanganywa.
P
 
Ha ha ha haaaa! Maiti kusafirisha dhahabu! Only in Tanzania!
Mkuu Mag3, kwanza kwenye voodooism you can walk copse, it's true Acacia is dead but not yet buried, hivyo it still exist even in death until it is put to its final resting place on 3rd September.
P
 
oh....kumbe AGM haijapitisha? which means kuna uwezekano wa azimio kukataliwa halafu ikawa back to square 1?
AGM bado itafanyika tarehe 3 September; kwa mujibu wa kanuni za PUSU tayari majority waliishakubali na kabla ya AGM lazima kila shareholder asaini ile scheme document ni kiapo na kinasainiwa mahakamani, asiyekubali analipwa shares zake according na kusepa.
P
 
Kitu kimoja lazima mwelewe katika mgawanyo wa kazi duniani. Nchi maskini zina all the world precious resources included but not limited to gold. Walaji na wanunuzi wakuu wa gold ni mabeberu. Dhahabu ya Geita haiwezi kuuzwa Songea au Malawi. Lazima tuwauzie mabeberu (washiriki wa maendeleo? Maana majina yao yanabadilika kulingana na context). Marketing, processing, exportation na kazi zingine kuhusu gold zinafanywa na makampuni ya kibeberu. Sisi kazi yetu ni kupiga kelele na misifa ya kijinga (professorial rubbish) mwisho wa yote lazima beberu aingie zizi kuwasjughulikia. Ndicho kinachotokea sasa na ndicho kitakachoendelea kutokea Tanzania. Tumebana weeee mwisho tumeachia wenyewe bado tuko misifa yetu ya kijinga. Namna ya kujadili mikataba hatuna ujuzi wala business strategies tunaishi katumbua mimacho kama mjusi kabanwa kwenye mlango. Mibeberu inatupigia mahesabu wapi yatupigebkutokana na umbumbu wetu kwenye negotiations. Cry my Beloved Tanzania, my country.
 
Kama nilivyoeleza kwenye jibu lililotangulia, Acacia hajazuiliwa kwa kukosa leseni, bali Acacia ni hatambuliwi na serikali kwa kutokusajiliwa nchini, lakini migodi yake mitatu, Buzwagi, Bulyanhulu, na North Mara inatambuliwa,ina leseni na inaendelea na uzalishaji wa dhahabu na kui export.

Kilichozuiwa ni export ban on makinikia na sio uzalishaji wa makinikia wala uzalishaji wa dhahabu.

Kufuatia Acacia kutokutambuliwa ndipo Barrick akainunua, ila mauziano bado hayajawa finalized, wakati hayo yakiendelea mgodi mmoja wa North Mara ulisimamisha uzalishaji wa dhahabu kwa sababu za kimazingira, sasa ndio umeruhusiwa kuendelea na uzalishaji wa dhahabu na export hadi mauziano yatakapo kamilika.
P
Aliweza je kuuza hisa DSE bila kutambuliwa, anyway propaganda Za wakati ule
 
Back
Top Bottom