Abdulrahman Kinana: Who is he?

He is very professional ... katika utendaji wake wa kazi! Nilibahatika kufanya nae kazi sehemu fulani, na nili-appreciate kichwa chake!

Yeye ni mwanachama mwenye heshima sana ndani ya CCM, na mara nyingi hutumiwa kusuluhisha mipasuko ndani ya chama (Mbeya alishafika!).

Kwenye biashara, kila unapomkuta Sir Andy Chande basi nae Kinana yupo! hawa ni washikaji sana kibiashara, na mara nyingi wako kwenye Bodi za serikali pamoja!
 
ARK aliwahi kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.......

Ni nini alichokifanya wakati huo???
 
Kinana bado yumo kwenye siasa kwani bado mjumbe wa National Executive Committe na Central Committe ya CCM.

Pia alikuwa mbuge na speaker wa bunge la Africa Masharika lililomaliza kipindi chake mwaka juzi.

Pia alikuwa campain manager wa mgombea urais wa CCM mwaka 1995, 2000, pia nadhani hata mwaka 2005.

Kama ilivyodokezwa hapo juu, alitishiwa kuwa si raia na achane na nadhani ndio maana ameamua kujiweka mbali na active politics za ndani.
 
Wanomuelewa mh KINANA wanasema kwa kweli ile ndio machine iliyobaki kwenye CCM.

Yeye ndio master mind wa mipango mengi ndani ya Chama na ndio maana Ujumbe wake ndani ya CC na NEC ni wa bila kupata upinzani.

Kwenye Serikali Hii ya Mafisadi yeye ni mshauri wa Mipango mingi hususani ile ya inayohusu masuala ya Kiprotocol na Usalama , wanasema yeye ni INT wa nguvu sana.

Inaelezwa pia kwa kipindi kirefu sasa amekuwa ni MJUMBE MUALIKWA wa BARAZA la mawaziri. Kwa sasa inaonekana ni kama muhimili wa mambo fulani ndani ya chama na serikali.

ULAJI wake anaupata zaidi kwenye biashara zake na ni mjumbe wa BODI nyingi tuuuuu.

Kumbuka kuwa anapata STAHIKI kama za mawaziri baadhi ya wakati.

Jamaaa inasemekana si mtu wa KUKURUPUKA na mipango yake mingi huenda na kukamilika kwa UFANISI zaidi.
 
Kinana acharuka, asema ametumika kama pilipili kwenye kachumbari!

Tanzania Daima

KADA maarufu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema hahusiki na usafirishaji wa meno ya tembo nje ya nchi, ikiwa ni siku moja tu tangu gazeti moja la wiki, lichapishe habari iliyomuelezea kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyosafirisha meno hayo.

Hata hivyo, kada huyo amekiri kuwa mmiliki wa Kampuni ya uwakala wa meli ya Sharaf Shipping Agency, iliyohusika kusafirisha makontena yaliyokuwa na nyara hizo za serikali, kabla ya kukamatwa nchini China yakiwa safarini kupelekekwa Hong Kong.

Gazeti hilo lilimtaja Kinana kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa na hisa 7,500 kati ya 10,000 katika kampuni hiyo, huku hisa nyingine 2,500 zikiwa zinamilikiwa na mshirika mwenzake, Rahma Hussein. Thamani ya hisa hizo ni sh 1,000 kila moja.

Kinana alitoa ufafanuzi huo katika mahojiano maalum na Tanzania Daima.

"Nimeisoma habari hiyo na kwa bahati mbaya sioni anayenilaumu wala kitu ninacholaumiwa nacho. Kwamba nina hisa katika kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf ni kweli.

"Lakini mimi sina nafasi yoyote ya kiutendaji na wala sishughuliki na uendeshaji wa kampuni hiyo. Kwa kweli sikujua na wala sikuhusika kwa namna yoyote ile na usafirishaji wa makontena hayo na mengine yoyote," alisema Kinana.

Alisema anachojua yeye ni kwamba, maofisa wa kampuni hiyo waliuliza na kuambiwa kuwa shehena iliyokuwa katika makontena hayo ni plastiki zilizotumika.

Alifafanua kuwa, wenye wajibu na mamlaka ya kukagua shehena zote zinazosafirishwa nje ya nchi ni mamlaka za serikali na si kampuni ya uwakala wa meli.

Alisisitiza kuwa, hana mamlaka kwa mujibu wa sheria kukagua mali inayosafirishwa japokuwa anaweza kuuliza bidhaa iliyopo katika makontena hayo.

"Ni dhahiri kabisa kwamba, habari hii imeandikwa na jina langu kutumika katika malengo ambayo siyajui. Nahisi kama jina langu limetumika kama pilipili katika kachumbari ili kunogesha habari.

"Kwa bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa kupasha habari, basi umma umedanganywa," alisema Kinana.

Kwa mujibu wa habari hiyo, sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali liliibuliwa kwa mara ya kwanza na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, katika Bunge lililopita la bajeti.

Ilidaiwa kuwa, nyaraka hizo zilionyesha kuwa, kilichokuwa ndani ya makontena hayo ni plastiki zilizodurufishwa na baada ya ukaguzi kufanyika, iligundulika kuwa, kilichokuwemo ni pembe za ndovu.

Habari ya gazeti hilo hata hivyo, ilimnukuu ofisa mwandamizi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, akieleza wazi kuwa kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani, wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa, makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.

Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Philipines, China, Singapore na Hong Kong.

Kaaaaaazi kweli kweli !

Warya Kinana amechelewa kujitetea....Kila kitu kipo wazi,atajificha wapi wakimueleza kuwa wanawafahamu hata wale vijana wa Ngaramtoni wanaowatuma kuwinda hao Wanyama?Ugomvi hapa sio nani mmiliki wa SSA bali mzigo unaosafirishwa na SSA ni wa nani?......Bado Tanzania tuna safari ndefu hawa viongozi wetu ndio wanaofanya kila uovu.Kinana si Mmiliki tu wa Sharaf pia ndiye mtu ambaye anahusika na hizo Nyara zilizokatwa Singapore!
 
Siajabu watu kama hawa kukataa. Tumeshazowea, hata yule mkuu wa wilaya alietuma watu wakawinde wanyama pori kule Wamimbiki(Morogoro) eti kakataa kua yeye hahusiki ila kamati ya Mwenge ambayo yeye ndiye mwenyekiti wake. Confusion na kujichanganya tupu!
 
Yumo huyo!!
Did any body expect him to confess that he owns the cargo? He is inn unless proved otherwise. Kama si wake, dili zima analijua angalau. Kionanan wee!
 
Warya Kinana amechelewa kujitetea....Kila kitu kipo wazi,atajificha wapi wakimueleza kuwa wanawafahamu hata wale vijana wa Ngaramtoni wanaowatuma kuwinda hao Wanyama?Ugomvi hapa sio nani mmiliki wa SSA bali mzigo unaosafirishwa na SSA ni wa nani?......Bado Tanzania tuna safari ndefu hawa viongozi wetu ndio wanaofanya kila uovu.Kinana si Mmiliki tu wa Sharaf pia ndiye mtu ambaye anahusika na hizo Nyara zilizokatwa Singapore!

Kinana, moja wa watu watatu wenye busara (wengine wakiwa Mwinyi na Msekwa) ambao wamepewa jukumu la kupatanisha makundi ndani ya CCM - nani atamgusa ? Hivi humo ndani ya CCM hakuna hata moja asiye FISADI ? Kaazi kweli kweli !
 
Yupo mkuu. Anaitwa Kingunge Ngombale Mwiru.
 
Yupo mkuu. Anaitwa Kingunge Ngombale Mwiru.

Huyo Mzee Kingunge ana ugomvi na ofisi ya Bwana Pinda (PM).Kampuni ya Bwana kingunge ijulikanayo kama SMART ndio watoza ushuru wa Stendi ya Mabasi ya Ubungo toka 2004...Mheshimiwa Pinda aliwahi kumuamuru Auditor General kupitia Hesabu za Kampuni hiyo ambayo inalalamikiwa na Uongozi wa Wilaya ya Kinondoni kuwa wanatia ndani mapato! Viongozi wetu wengi si waadilifu.....
 
Warya Kinana amechelewa kujitetea....Kila kitu kipo wazi,atajificha wapi wakimueleza kuwa wanawafahamu hata wale vijana wa Ngaramtoni wanaowatuma kuwinda hao Wanyama?Ugomvi hapa sio nani mmiliki wa SSA bali mzigo unaosafirishwa na SSA ni wa nani?......Bado Tanzania tuna safari ndefu hawa viongozi wetu ndio wanaofanya kila uovu.Kinana si Mmiliki tu wa Sharaf pia ndiye mtu ambaye anahusika na hizo Nyara zilizokatwa Singapore!

Mkuu Mwawado heshima mbele.

Huyu Warya Kaale tulishamstukia siku nyingi jamaa ni fisadi wa siku nyingi sijui alivyoweza kukwepa vyombo vya habari kwa muda wote eti sasa wanahabari ndiyo wanaanza kumstukia.

Kinana anahusika na ujio wa wale waarabu walionyakua ardhi Loliondo,Tena yeye ni rais wa hiyo kampuni.Ni Kinana huyu huyu aliiba mashine za kufulia nguo za Hospital ya mkoa wa Arusha [Mount Meru hospital] na kuanzisha kampuni ya Falcon drycleaner.

Kinana ana husika na mradi wa kuwapatia uraia wa Tanzania wakimbizi wote wa kisomali walioko Chogo mkoani Tanga.Wakimbizi wa Kikongo,Burundi na Rwanda walikataliwa na kulazimishwa kurejeshwa makwao.
 
Back
Top Bottom