QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
- Thread starter
- #21
Inaonekana wewe una chuki binafsi na CCM. Viongozi wenu wanadai ni usalama wa taifa sasa usalama wa taifa na CCM wapi na wapi? Mazingira yanaonesha CDM inahusika ili iichafue serikali na Usalama wa Taifa. Haiwezekani ktk bajeti zao waishutumu idara ya usalama kabla hata tukio la Ulimboka halijatokea ina maana bajeti zao zimeandaliwa juzi juzi tu? Hawa walijua kila kitu kuanzia kupanga migomo mpaka kumtesa ulimboka kwa kutumia watu wao waliopandikiza ktk usalama.
Viongozi wenu walishadai wana watu wao usalama wanaowapa habari za serikali bila shaka hawa ndio waliotumika kwa Ulimboka kwa sababu wametumwa na watu ambao hawana utaalamu wa kutesa watu wao ni wanasiasa. Ushahidi wa ulimboka mwenyewe unadai kuwa walikuwa wanashauriana wampige sindano ya sumu, risasi mwisho wakapatana wamgonge na gari. hapo utaona hawa hawakutumwa na idara ya usalama wa Taifa maana kama iliwatuma wangejua wanatakiwa kufanya nini na nini wameambiiwa wafanye na sio wao wenyewe kushauriana cha kufanya.
Msiipake matope idara ya usalama wa taifa maana imetukuka na inafanya kazi na serikali yoyote iwe ni ya CCM au CDM
Hatuna usalama wa Taifa tanzania, Ni usalama wa CCM.