A God can be a mere theory, nothing more

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,707
3,329
Habari za hapa.

Nimefanya research juu ya ukweli wa dini na uwepo wa Mungu hasa Mungu anaeongelewa na wakiristo na waislamu.

Ktk utafiti huo nimegundua mushkel mwingi SANA kuhusiana na dini hizo na suala la uwepo wa Mungu in general as it preached by Muslims and Christians.

My be I'm wrong thus why nimeweka hoja hapa ili mwenye uelewa anieleweshe na pia aweze kujibu maswali. Lengo langu ni kutambua ukweli na sio kuleta ubishi usio na tija. so nakaribisha maswali na pia nasistiza wale wasio na hoja wajifanye kama hawajauona uzi huu.

HAYA NI MAMBO NILIOYAONA KTK UTAFITI WANGU:

1. Dini ziko nyingi (ni zaidi ya 30 na hapo hujagusia madhehebu!!) but licha ya uwingi huo kila dini inajiona iko sahihi ZAIDI ya nyengine. It cant be all religions are true but there possibility all of them are wrong.

2. Kwa huku Africa dini hizi tumeletewa, walioleta dini walileta ili kututawala. hope hili liko wazi, ie Uislam uliletwa na waarabu ambao walikuja kufanya utumwa na kutuuza sehem tofauti kama bidhaa tu. kiukweli tulipata shida sana. Pia ukiristo uliletwa na wakoloni ambao walikuja kuchukua malighafi na nguvu kazi zetu na kutuacha ktk hali ya utegemezi hadi leo hii.

Jee dini ya kweli inaweza kuletwa na madhalimu?

3. Qur-an and Bible (here and after refers to vitabu vitakatifu) vimecontain ukweli, uongo, many unreasonable teachings and contradictions on its/them. eg: Kwamba dunia ni flat, imetulia na jua ndilo linalotembea kutoka mashariki kwenda magaribi. (hope mnautambua uongo huo but if hujatambua hilo niambie nikuekee ushahidi ili tuende sawa)
Pia dini zinaruhusu mtoto wa kike kuolewa na kuingiliwa hata kama hajavunja ungo!!!! (pia naweza kuthibitisha hilo) na mengi mengineyo. (just put a number and tell me which no. you don't agree)

4. Kwamba mitume na manabii wote wametoka FAR EAST. kwamba around north Africa and western Asia. no more. (Ikiwa unaushahidi hata wa maandiko tu kupitia vitabu vitakatifu unaoonesha uwepo wa mitume apart from far east ningependa unitoe haya matongo)

Jee Mungu hakutaka kuabudiwa na watu kutoka Southern Africans? China? Korea? Northern Europe? North and Southern America? Australia?

5. Vitabu vitakatifu vinatafsiriwa kisiasa zaidi ili kuzibia errors ambazo Mungu aliacha kwenye vitabu hivyo! Eg: Mungu ameweka wazi kwenye vitabu vitakatifu kwamba jua linazama kwenye matope but Muslims wanasaidia majibu kwamba ni Red sea! wanaact kana kwamba Mungu hajui kusema Red sea! unapoulizia kuhusu jua kutembea kutoka mashariki kwenda magharibi na suala la kwamba dunia ni flat hapo unaambiwa Mungu ameielezea dunia kama ambavyo sisi tunaiona!!!

But wakati huo huo tunaambiwa vitabu vitakatifu vinaendana na nyakati!!! kwamba hata mambo ya kisansi yameongelewa mle toka enzi na enzi ambayo practise zake zinatokea sasa! Hapo unaweza kuuliza mbona hizo scientific findings hazikuongelewa kama sisi tunavyoona? Issue inakuja kwamba kwenye bible ni hivyo hivyo na kwenye Quran ni hivyo hivyo wakati hizo dini zinapingana vilivyo hadi kufikia kuitana magaidi na makafiri!!!! (Hapa nnamifano mingi tu na ushahidi just put a number and request me to proof)

6. Dini ya mtu inatokana na namna ya wazazi and/or walezi walivyomlea. hapa ningependa kueka wazi kwamba si kila dini or imani ya mtu ni zao la wazazi but ni wachache sana wanaoamini dini or imani ambayo hawakufunzwa na wazazi wao. kwa makadirio ni asilimia 5 tu ya wanaoamini kinyume na mafundisho ya wazazi wao. na kati ya hao, wengi wamebadili imani kutokana na mapenzi (romantic love) na kipato/pesa. ni wachache sana walioamini dini nyengine kwa kutumia their logic reasoning na findings. Hata wewe unaesoma hapa unaamini hicho unachokiamini kwa sababu tu wazazi and/or walezi wako wametokea imani hiyo, nothing more. and you cant fight against reality.

Jee wazazi/walezi wote wako sahihi na imani wanazowapachika watoto wao?

7. Sifa anazopewa/anazojipa Mungu ni za uongo.

a) Mungu nimuweza wa yote. Kwanini haifanyi dunia kua sehwm salama? Kwanini mauaji? Kwanini unyama? Si anaweza yote? kwanini hazuii? For what? Ivi apa hamuoni ni sawa na mtu anaekwambia anapesa but ukimwambia nioneshe anakwambia nimeziacha nyumbani???

b) Mungu ni mpangaji wa kila kitu.
Nadharia hii jiliipinga wakati naamini na nilitetea kwamba Mungu anajua tu ila hapangi but niliambiwa napingana na maandiko. na kweli nilipewa ushahidi wa wa Maandiko Kwamba Mungu akimpangia mtu kupotoka hakuna wa kumuongoa na aliemuongoa hakuna wa kumpotosha!!!!

So ikiwa amepanga kila kitu kwanini aje aadhibu then?
Jee Mungu anaupendeleo? Sasa kwanini atupungie yeye matendo yetu? kwanini asituache tukaact by our own free will?

c) Mungu ni mkamilifu.
Kwanini anaumba vilema? Matahira? Wamemkosa nini hao? Au ukamilifu wake uko limited kwa baadhi ya vitu tu? Au vilema na matahira wameumbwa na nani?

d) Anapenda watu wote. Kwanini wengine wanahangaika sana? Kwanini wengine wanadhulumiwa sana? ukumbuke yeye ni mueza wa kila kitu.

Then kama anapenda kila mtu kwa nini ameahidi tabu na mashaka kwa vizazi vya Izrael kwa makosa ya mababu zao? Hawa wanaozaliwa sasa wamemkosea nini?

HOW UNREASONABLENESS GOD HE IS?

Sifa za uongo anazonyingi but let me skip and wait somebody who is interested on that point.

8. Ukweli juu ya Astrology. Astrology ni uhusiano wa mizunguko ya sayari na tabia za mtu kwa kuzingatia tarehe na saa aliyozaliwa. Najua hili ni somo geni kwa wengi wetu humu. but not an issue, ili nawe ujue ukweli wa astrology nitaweka link just put your information as it required on the given link so as to comment on this point.

https://alabe.com/freechart/

Hapo utagundua nini kimeinfluence tabia zako. Na kwa mantiki hiyo unapata jibu si kila unavyofanya or ulivyoepangiwa na Mungu also utajua si Mungu pekee anaeijua kesho ikizingatia alishasema hakuna anaeijua kesho. Ningependa kupokea hoja kwa point hii kwa mtu alietoa uvivu na kuingia humo. Narudia tena sipendi ubishi wa kiji.nga.

9. Miujiza na maono waliyokuwa nayo mitume ni uwezo alionao kila mwanadamu.

Inaaminika mitume waliweza kuota ndoto za kweli pia waliweza kutafsiri ndoto za wengine.
Waliweza kutabiri mambo yajayo pia waliweza kuelezea mambo mengi yaliyopita.
Pia waliweza kufanya miujiza tofauti tofauti.

Watu wengi hudhani yale ni Miujiza kutoka kwa Mungu kitu ambacho sio kweli, it just how they succeed to activate their pineal gland. Pineal gland ni part ya ubongo iliopo kati lakini chini ya ubongo wa kila mwanadamu. ingia ata google uone picha. Ukiweza kuactivate pineal gland unafungua nguvu zako za maono na miujiza. pineal gland kwa kishwahili wanaita jicho la tatu.

Ile miujiza sijui maono just ni psychic powers ambazo kila binadamu anazo sema zinatofautiana tu kidogo.

Wakiristo wengi huibiwa pesa zao makanisani kwa nguvu hizi. then ata biblia imegusia ili somo sema tu watu tuwavivu wa kusoma. always tunakarirshwa machache ili wajanja wale vyao bila tabu.

Namna ya kuactivate jicho la tatu ni kumeditate (tahajudi/kusali), hata Yesu inaaminika alikua akisali. wakiristo hawajiulizi huyu Mungu alikua akimsalia nani? Yeye si ni Mungu, si angefanya tu mambo yake bila ya kusali. ukija kwa uislamu tunaambiwa Muhammad alikua akienda milimani kusali kabla ya kupewa utume. tunaambiwa alipofatwa na mfalme najash ili kuthibitisha utume wake alisali kwanza, mifano ni mengi na inaanzia kwa ibrahim.

Point hapa ni kwamba wale waliodevelop vizuri pineal gland zao na kujitangazia utume ndio mitume iliyoorodheshwa kwenye vitabu. pia ikumbukwe ilifikia uwepo wa mitume miwili kwa wakati mmoja na ilitokea mtoto alikua mtume, baba yake alikua mtume, babu yake alikua mtume na yeye mwenyewe akazaa mtume. hiyo iko kwenye biblia na quran too. (anaepinga naweka ushahidi)

Nisiwachoshe sana. hivyo ndivyo nilivyogungua kwenye reseach yangu.
Yoyote mwenye kupinga naskiliza hoja yake.
 
Kwa sababu umejaza mawazo yanayopinga mamlaka ya Mungu, hata ukiletewa hapa majibu kwa maswali uliyouliza,itakuwa kazi bure.
Mimi ngoja nijibu moja ya maswali yako. Katika Biblia hasa kitabu cha Waefeso 4:5-7 anaposema 5 tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote. 7Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo. Hapo red, ilitakiwa duniani mwote imani iwe moja, lakini shida ni kwamba shetani naye kupitia wakala wake aliyeanzisha imani ya uongo(imani ya kupinga Mungu), mtu huyo akiitwa Nimrod, amefanikiwa kudanganya ulimwengu kwa kiasi kikubwa.
 
7. Sifa anazopewa/anazojipa Mungu ni za uongo.

a) Mungu nimuweza wa yote. Kwanini haifanyi dunia kua sehwm salama? Kwanini mauaji? Kwanini unyama? Si anaweza yote? kwanini hazuii? For what? Ivi apa hamuoni ni sawa na mtu anaekwambia anapesa but ukimwambia nioneshe anakwambia nimeziacha nyumbani???
Kumbuka Mungu akitoa adhabu juu ya binadamu waasi (Adamu na Eva) alimwambia Eva hivi kuhusu uzao wake na uzao wa shetani.
uzao wako(Eva) utamponda kichwa(nyoka), na yeye atakuponda kisigino. Ni kutokana na hapo, ndiyo maana wana wa Ibilisi na wana wa Mungu kila mmoja kwa nafasi yake humdhuru mwingine. Mungu si kwamba haoni mateso yote ambayo wana wa uovu wanawafanyia wana wa Mungu, lakini kama pambano alishaliacha mikononi mwa viumbe waliouziana utawala(mtawala wa dunia wa mwanzo alikuwa Adamu, aliuza haki hiyo alipokula tunda alilokatazwa rejea 2 Wakorintho 4:4), hakuna budi sasa wakapambana, na ni hadi mwanadamu anapotambua kuwa msaada pekee kwake kushindana na wana wa uovu unatoka kwa Mungu na akaomba usaidizi wa Mungu, ndipo Mungu huingilia kati. Tofauti na hapo, Mungu alishaacha mpambano ufanyike kwa uhuru kabisa (kuponda kichwa au kisigino), mshindi atajulikana mwisho wa mpambano, hivyo Mungu anasimama katikati ya mpambano kama mwamuzi tu.
 
Naungana mkono hoja yako 100% wanaobisha wabishe ila huo ndio ukweli, uwepo wa Mungu upo kinadharia zaidi, Mzungu aliandika biblia ili kuifanya dunia iwe sehemu ya amani tu lakini alikuja kuieneza Afrika ili kuogofya waafria na kuwafanya inferior ili iwe rahisi kuwatawala.

Angalia
  • Mungu mweupe (mzungu)
  • Malaika weupe(wazungu)- shetani mwausi(mwafrika)
  • Manabii wote walikuwa wazungu
  • Yesu mzungu
  • Utamaduni wao hadi wakutembea uchi ni baraka- wetu sie waafrika sio wakistarabu
  • Baraka zote zipo kwao- laana Afrika
Hivi kweli hakuna hata mweusi mmoja ambaye mungu alimuona kipindi hicho akambariki??????

Lazima tukubali biblical theory ilienezwa sana baada ya wazungu kuona Charles DArwin kaja na Evolution theory hali ilionesha mwafrika ni mtu wa kwanza kuishi katika sayari ya dunia, hapo ndipo walipojifanya kuja kuieneza sana dini ukizingatia walihofu kipindi cha industrial rev isingekuwa rahisi kupata cheep lobour kama wasingetumia biblia. ukweli biblical theory is just a myth, uwepo wa mungu pia ni dhahania tu.
 
Hata mimi kuna maswali huwa najiuliza, Kwa nini mungu ali muumba lucifer(shetani)? Wakati alikua anajua kabisa atakuja kuleta madhara , matatizo baadae. Kwa kua yeye anajua mwanzo mpaka mwisho wa wakati ko alikua anajua exact time ambayo lucifer ange asi, idadi ya malaika ambao wange muunga mkono nk.Too bad lucifer hakua na element of surprise.
Kwa nini ali mtupa shetani duniani wakati ana jua kabisa Adam Na Eve walikua hawana uwezo wa kumshinda ambapo leo hadi vizazi vyao vina teseka?
 
Naungana mkono hoja yako 100% wanaobisha wabishe ila huo ndio ukweli, uwepo wa Mungu upo kinadharia zaidi, Mzungu aliandika biblia ili kuifanya dunia iwe sehemu ya amani tu lakini alikuja kuieneza Afrika ili kuogofya waafria na kuwafanya inferior ili iwe rahisi kuwatawala.

Angalia
  • Mungu mweupe (mzungu)
  • Malaika weupe(wazungu)- shetani mwausi(mwafrika)
  • Manabii wote walikuwa wazungu
  • Yesu mzungu
  • Utamaduni wao hadi wakutembea uchi ni baraka- wetu sie waafrika sio wakistarabu
  • Baraka zote zipo kwao- laana Afrika
Hivi kweli hakuna hata mweusi mmoja ambaye mungu alimuona kipindi hicho akambariki??????

Lazima tukubali biblical theory ilienezwa sana baada ya wazungu kuona Charles DArwin kaja na Evolution theory hali ilionesha mwafrika ni mtu wa kwanza kuishi katika sayari ya dunia, hapo ndipo walipojifanya kuja kuieneza sana dini ukizingatia walihofu kipindi cha industrial rev isingekuwa rahisi kupata cheep lobour kama wasingetumia biblia. ukweli biblical theory is just a myth, uwepo wa mungu pia ni dhahania tu.

Na wewe unawaza hivi...?

Sitaki kuamini.
 
9. Miujiza na maono waliyokuwa nayo mitume ni uwezo alionao kila mwanadamu.

Watu wengi hudhani yale ni Miujiza kutoka kwa Mungu kitu ambacho sio kweli, it just how they succeed to activate their pineal gland. Pineal gland ni part ya ubongo iliopo kati lakini chini ya ubongo wa kila mwanadamu. ingia ata google uone picha. Ukiweza kuactivate pineal gland unafungua nguvu zako za maono na miujiza. pineal gland kwa kishwahili wanaita jicho la tatu.

Ile miujiza sijui maono just ni psychic powers ambazo kila binadamu anazo sema zinatofautiana tu kidogo.

Mkuu Mashaxizo, hapa nakubaliana na wewe na hili mimi niliishalizungumzia hapa;
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo Bila Kujijua!.

Ila hii hoja yako ya hakuna Mungu, ni kazi ya shetani!.

Mungu yupo ndio The Supreme Being!, Mwanza na Mwisho, Alfa na Omega, ambaye vitu vyote vimeumbwa nae.

Mungu yuko kwenye form ya spirit, God is Power, ndio nguvu inayowezesha kila kitu, ikiwemo uhai 'life force' na ana sifa kuu 4;

  1. Mungu ni omnipotent (all-powerful), Mungu ndio mwenye nguvu kupita nguvu nyingine zozote, ana emetupa sisi binadamu sehemu ya nguvu hizo kupitia 'WillPower'.
  2. Mungu ni omnipresent (in all places at the same time), yaani yuko mahali pote kwa wakati mmoja, ikimanisha Mungu yuko ndani yetu, na yote ambayo Mungu anayetenda anayatenda kutokea ndani yako!.
  3. Mungu ni omniscient (He knows everything), hivyo kila kinachotokea Mungu anakijua, yakitokea majanga, japo yanasababishwa na shetani, Mungu alijua na asipozuia inamaana ame approve, hivyo jambo lolote linalotokea, lilikuwa litokee, liwe zuri au baya ni kazi ya Mungu kwa sababu hata shetani yuko chini ya mamlaka ya Mungu.
  4. Mungu ni omnibenevolent (He only does things that are all good), yaani alipouomba ulimwengu na vyote vilivyomo alidhamiria yute yawe ni mema na mazuri tuu, ila shetani alipoasi, ndie mwenye jukumu la majanga, mateso na maovu yote!.
  5. Mungu alipomuumba binadamu, alimuwekea Uungu ndani yake, lakini pia akampa choice ya utashi wa kuamua au amfuate Mungu kwa kutenda yaliyo mema pekee, au amfuate shetani, kwa kutenda yaliyo maovu!.
  6. Tunaposema kutenda sio lazima matendo, actions, hata kwa kuwaza tuu mawazo maovu ni kumtumikia shetani, au kwa kusema maneno maovu, ni kumtumikia shetani.
  7. Shetani ana mission moja tuu duniani, kuyafanya yale yote yaliyo kinyume na Mungu, na utendani wa shetani ni kama ulivyo utendaji wa Mungu, yaani ile njia Mungu anayoitumia kumpa nguvu mwanadamu, ndio njia hiyo hiyo shetani anaitumia kumpoteza mwanadamu, tofauti pekee kati ya nguvu za Mungu na nguvu za shetani, nguvu za Mungu ni original na ziko ndani ya binadamu tangu siku ile ameumbwa, yaani ziko within, wakati nguvu za shetani ziko nje na ziliingizwa ndani kupitia kula tunda, hivyo ni aquired.
  8. Hivyo chochote kinachotokea duniani ni ama kwa nguvu za Mungu au nguvu za Mwanga, yaani Holly Spirit, ama kwa nguvu za shetani, nguvu za giza powers of the devil, na kuna wakati mwingine nguvu hizi hutumika kutenda mema au miujiza kama chambo, kwa shetani kuji disguise as God ili aweze kupata mavuno makubwa, hivyo kuna wahubiri kibao, wanafanya hadi miujiza kwa kutumia jina Mungu, lakini sii wa Mungu bali ni tricks za shetani. Majo ya kazi kubwa ya shetani ni kuwaaminisha binadamu kuwa hakuna Mungu kama anachofanya mtoa mada hii, anamtumikia shetani kwa kujua au bila kujijua, namna pekee ya kumsaidi ni maombi ili afunguliwe toka kwenye giza alimo aone mwanga.
  9. Tofauti pekee kati ya wema wa Mungu, na wema wa shetani, au miujiza ya Mungu na miujiza ya shetani ni conditionalities, kwa vile nguvu za Mungu ni original na kila mtu amepewa, miujiza ya Mungu au wema wa Mungu hutokea au huweza kufanyika naturally unconditional bila kuwekewa masharti yoyote, kwa Miujiza ya Mungu kutokea, unapaswa kuamini tuu. Lakini miujiza ya shetani au wema wa shetani ni conditiona una masharti lazima uyafuate!, ili itendeke au ataambiwa fanya hiki au kile!. Hivyo kuna wengi wanamtumikia shetani bila kujijua wakidhani wanamtumikia Mungu!.
  10. Ili uweze kujijua unamtumikia nani, au huko unakosali ni kanisa la Mungu au la shetani, kwanza ni wewe mwenyewe kutake your own initiative kutaka kumjua Mungu wa kweli, na hili unaweza kulifaniisha kwa kusoma vitabu vya dini kumjua Mungu kisha jifikirie kile kinachofanyika kwenye dhehebu lako ndicho Mungu alichofundisha?. Muulize Mungu aliyeko ndani yako kuwa hiki ni sawa?!, utaisikia sauti ikikuambia ukweli halisi!.

Jumapili njema.

Pasco

Haya ndio yale madhara ya kula tunda la mti wa kati tunda la ujuzi wa mema na mabaya
Neno litasimama, mambo yote yatapita lakini neno litasimama milele, wale wote waliojaribu kuichallange Bible miaka na miaka na hata kuandika tafiti na nadharia za kusadikika na kufikirika huku wakijaza mabuku na mabuku, walishaondoka na kusahaulika lakini NENO limeendelea kusimana
 
...mtoa mada ukitaka kujua unaamini kuwa Mungu yupo rejea pionti yako namba tano, nanukuu "kuziba errors ambazo Mungu ameziacha" so stop wasting our time kwa kuleta porojo kwenye mambo ya msingi ambayo nafsi yako pia inaamini ukweli Wa Mungu. Nenda ukany..e ukalale....
 
Japo nina shida na taabu za kila aina siwezi hadharani na kusema hakuna mungu. Nina imani ipo nguvu kuu takatifu juu yangu. Darwins alikuja na evolution theory yake karne ya 18 mungu ameshahubiriwa sana. Wazungu walileta habari njema Africa na penginepo kama ilivyoandikwa. Tunawiwa shukrani kwao badala ya kuwatukana
 
"Nimefanya research juu ya ukweli wa dini na uwepo wa Mungu hasa Mungu anaeongelewa na wakiristo na waislamu."

Mkuu Mashaxizo mie nina mashaka na hayo maelezo yako hapo juu. Uliposema kwamba umefanya research nikadhani kwamba utakuwa umezama ktk mafundisho ya hizo dini na kuja na mambo mapya, hivyo nikawa na hamu ya kuona ulichokipata kwenye hiyo research,lakini aina ya maswali uliyokuja kuuliza hayana tofauti na ambao hawajadai kufanya research.
Hebu kwanza tuambie hiyo research yako uliifanya vp? kwa sababu kama kweli ungekuwa umefanya research basi usingekuja kuuliza maswali kama hayo. Swali lako la kwanza tu linaonesha haujafanya research.
 
Last edited by a moderator:
Kwa sababu umejaza mawazo yanayopinga mamlaka ya Mungu, hata ukiletewa hapa majibu kwa maswali uliyouliza,itakuwa kazi bure.
Mimi ngoja nijibu moja ya maswali yako. Katika Biblia hasa kitabu cha Waefeso 4:5-7 anaposema 5 tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote. 7Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo. Hapo red, ilitakiwa duniani mwote imani iwe moja, lakini shida ni kwamba shetani naye kupitia wakala wake aliyeanzisha imani ya uongo(imani ya kupinga Mungu), mtu huyo akiitwa Nimrod, amefanikiwa kudanganya ulimwengu kwa kiasi kikubwa.

Mkuu ilitambulikaje kwamba hapo hapakustahiki kuwa 'imani moja'? Alitambua nani? We unahisi kwanini Mungu alishindwa kulinda maandiko?
 
Kumbuka Mungu akitoa adhabu juu ya binadamu waasi (Adamu na Eva) alimwambia Eva hivi kuhusu uzao wake na uzao wa shetani.
uzao wako(Eva) utamponda kichwa(nyoka), na yeye atakuponda kisigino. Ni kutokana na hapo, ndiyo maana wana wa Ibilisi na wana wa Mungu kila mmoja kwa nafasi yake humdhuru mwingine. Mungu si kwamba haoni mateso yote ambayo wana wa uovu wanawafanyia wana wa Mungu, lakini kama pambano alishaliacha mikononi mwa viumbe waliouziana utawala(mtawala wa dunia wa mwanzo alikuwa Adamu, aliuza haki hiyo alipokula tunda alilokatazwa rejea 2 Wakorintho 4:4), hakuna budi sasa wakapambana, na ni hadi mwanadamu anapotambua kuwa msaada pekee kwake kushindana na wana wa uovu unatoka kwa Mungu na akaomba usaidizi wa Mungu, ndipo Mungu huingilia kati. Tofauti na hapo, Mungu alishaacha mpambano ufanyike kwa uhuru kabisa (kuponda kichwa au kisigino), mshindi atajulikana mwisho wa mpambano, hivyo Mungu anasimama katikati ya mpambano kama mwamuzi tu.

Nakusoma vyema mkuu.

Embu tujaribu kueka inference hii:
Kwamba wewe unawatoto wako wawili, unawapenda sana, ukawambia kitu fulani msifanye (coz kinamadhara kwao) but watoto wakakengeuka na kufanya. Jee utawaacha tu kwa vile ulishawakataza?

Does it logically? If not, why?
 
Naungana mkono hoja yako 100% wanaobisha wabishe ila huo ndio ukweli, uwepo wa Mungu upo kinadharia zaidi, Mzungu aliandika biblia ili kuifanya dunia iwe sehemu ya amani tu lakini alikuja kuieneza Afrika ili kuogofya waafria na kuwafanya inferior ili iwe rahisi kuwatawala.

Angalia
  • Mungu mweupe (mzungu)
  • Malaika weupe(wazungu)- shetani mwausi(mwafrika)
  • Manabii wote walikuwa wazungu
  • Yesu mzungu
  • Utamaduni wao hadi wakutembea uchi ni baraka- wetu sie waafrika sio wakistarabu
  • Baraka zote zipo kwao- laana Afrika
Hivi kweli hakuna hata mweusi mmoja ambaye mungu alimuona kipindi hicho akambariki??????

Lazima tukubali biblical theory ilienezwa sana baada ya wazungu kuona Charles DArwin kaja na Evolution theory hali ilionesha mwafrika ni mtu wa kwanza kuishi katika sayari ya dunia, hapo ndipo walipojifanya kuja kuieneza sana dini ukizingatia walihofu kipindi cha industrial rev isingekuwa rahisi kupata cheep lobour kama wasingetumia biblia. ukweli biblical theory is just a myth, uwepo wa mungu pia ni dhahania tu.

Well Apologise lady, watu wamefungwa na nidhamu ya uoga, wanashindwa kutrace hata historia ya imani yao, wanashindwa hata kusoma matabu yao matakatifu na kuona walivyochanganyiwa pilau na mrenda. fikra zao zimefungwa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom