EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, ameunda Tume maalumu kuchunguza sakata la upotevu wa fedha za kigeni, dola za Marekani 50,000 (takriban Sh milioni 90) katika mazingira ya kutatanisha katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha.
Habari zilisema mbali ya askari Polisi wawili waliowekwa ndani kwa kutuhumiwa kuiba fedha hizo na kutoa maelezo yao, pia wako askari wengine wanne wametoa maelezo, lakini hawakuwekwa rumande.
Fedha hizo dola 50,000 zilizooneshwa mahali ziliko na mmoja wa watu watatu wanaosadikiwa kuhusika na ujambazi kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki maarufu jijini Arusha kwa jina la toyo ama bodaboda zimeyeyukia mikononi mwa polisi katika mazingira ya kutatanisha.
Habari zilisema askari waliokwenda eneo ambako dola ziliko, walirudisha majibu kuwa dola zilizopatikana ni dola 900 tu, hatua ambayo inadaiwa kupingwa na mtuhumiwa wa ujambazi aliyeongozana na askari hao.
Kutokana na utata huo uongozi wa hoteli hiyo ulitaka kujua kwa kina juu ya upatikanaji ama kutopatikana kwa fedha hizo kwa maandishi na sio maneno.
::HAbariLeo