Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,012
Hilo ni suala jengine, la INCOME DISTRIBUTION.
Hio kikawaida ni changamoto, tena haipo kwenye Nchi za Ulimwengu wa tatu tu, bali hata huko kwenye maendeleo.
HOJA YA MSINGI.
1. Uchumi unakuwa.
2. Shilingi haijashuka thamani kwa asilimia hamsini tangu 2005; JK alipopata Urais.
3. kushuka kwa thamani ya shilingi sio lazima kiwe ni kiashiria cha kudorora kwa uchumi.
4. Kuwa na Currency Note ya Tshs sio jambo la kubezwa. kwani wangapi wanaenda sehemu mbali mbali na kutakiwa kulipa hela zaidi ya Tshs 50000 kununulia bidhaa au huduma?
Baada ya HOJA hio, tunaweza kufungua mjadala wa Income Distribution, ambao utakuwa mrefu mno.
Nawasilisha
Uchumi upi unaokua? Kama wa mafisadi kweli unakua na utaendelea kukua ..at least kwa miaka mingine 5..lakini kwa wananchi wa kawaida uchumi unarejea nyuma..na mifano michache iliyotolewa na wadau ni kielelezo tosha..Mathalan..
--Kushuka kwa thamani ya TSh dhidi ya USD.
--Bidhaa muhimu kupanda bei wakati kwa kasi kisichoendana na kuongezeka kwa kipato.
Halafu labda niongezee hapo kwenye pengo la maskini na tajiri, pamoja na kwamba lipo hata kwene dunia ya kwanza, huwezi ukalinganisha paka wa NYC na paka wa Tandale..ingawa wote ni paka..hivi ni vitu viwili tafauti kabisa, sawa na mchana na usiku.