4000 waambukizwa Ukimwi Kinondoni ndani ya miezi mitatu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Monday, December 28, 2009 1:11 PM
IMEDAIWA kuwa ndani ya miezi mitatu kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu watu wapatao 4072 wameambukizwa virusi vya ukimwi katika Manispaa ya Kionodnoni jijini Dar es Salaam Hayo yalijulikana baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi katika Manispaa hiyo kutoa takwimu hiyo.

Kati ya watu hao, 1,165 ni wanaume na 2,911 ni wanawake ambapo wote walipewa rufaa kwenda katika vituo vya kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU nchini.

Katika taarifa iliyotolea na kamati hiyo imesema watu hao wataanza tiba ya huduma ya kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU na katika Manispaa hiyo kuna jumla ya vituo 17 vya kupata vidonge hivyo.

Imesema kwa sasa katika vituo hivyo wameshafikia wagonjwa 12,829 ambao wamejiandikisha.

Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kwa sasa wagonjwa wanaotumia dawa hizo ARVs ni 7,033 huku wengine wakiendelea na huduma za uchunguzi na ufuatiliaji na endapo CD4 zitashuka chini ya 200 wataanzishiwa dawa.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa manispaa imetenga kiasi cha Shilingi. milioni 109.9 ili kuimarisha vita dhidi ya kuenea ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka wa fedha unaoishia Julai mwakani.

http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3820334&&Cat=1
 
hivi dawa ya ukimwi itapatikana lini? Kupatikana kwa dawa ya kuponya ugonjwa huu utakuwa ni suluhusho la ukweli Africa. Watu wanateketea, watoto wanabaki yatima, taifa linapoteza nguvu kazi. Ukimwi unawapata waliomo na wasiokuwemo. Jamani tubadili tabia, tunapukutika tukijiona.
 
Dawa ni kuacha kabsaaa ngono uzembe. Ebu fikiri iwapo:

  • kula ni kujenga mwili na kuweza kuishi
  • kulala ni kupunguza uchovu
  • kufanya kazi ni kujiongezea kipato
  • kusoma ni kujiongezea maarifa
Kama utajiuliza moyoni mwako mara kwa mara nini faida ya ngono kamwe huwezi kujihusisha nazo kabsaaaaa!.
 
mhh hizi takwimu zimepatikanaje??methodology please ..4000 wameambukizwa within 3 months?au katika 3 months ndo wameweza kupima watu na kugundua 4000 wana maambukizi? iam missing something here
 
mhh hizi takwimu zimepatikanaje??methodology please ..4000 wameambukizwa within 3 months?au katika 3 months ndo wameweza kupima watu na kugundua 4000 wana maambukizi? iam missing something here

usicheze na research za ofisini badala ya field, cooked figures ambazo zinaishia kwenye njia mbaya za kusolve matatizo
 
UKIMWI siku hizi umekuwa ni mtaji kwa watu kuweka matakwimu ya uongo uli waendelee kuvuna mabilioni ya misaada kwa waathirika halali wa janga hili, takwimu za uongo hizo zisizo na evidence na proof!
 
usicheze na research za ofisini badala ya field, cooked figures ambazo zinaishia kwenye njia mbaya za kusolve matatizo

kwa kweli mkuu naungana na wewe..i have been in research for 15 good years..and this figure really shocked me!!
 
katika hao 4000 wangapi ni memba wa jf? bikozi hapo kinondoni ndo kuna memba kibao wa jf. kimewaka!
 
Back
Top Bottom