3 Years Review: Bajaj Boxer Bm 150X

Vangiporini

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
313
231
Mnamo mwaka 2019 nilinunua Boxer 150x ikiwa mpya kabisa, na nilifanya maamuzi magumu kutokana na changamoto nilizokuwa nikiambiwa kuhusu pikipiki aina ya Boxer lakini niliamua tu kuinunua hivyo hivyo kwa kuwa nilitokea kuipenda sana.

Tangu nimeinunua nimekua naipigia kazi balaa (matumizi binafsi sio bodaboda) maana nipo maeneo ya kijijini na means kubwa ya usafiri ni pikipiki. Lakini pia imeshakula masafa marefu sana.

Mpaka sasa Odometer inasoma 50,000 km
Haijawahi Kufunguliwa engine (zaidi ya kufungua cover kuadjust tappets)
Haijawahi kutoa moshi (poston rings bado zinadunda)
Power bado iko vizuri
Ulaji wa mafuta bado sioni tofauti

Kwa muda wa miaka mitatu na huyu mnyama nimezingatia sana vitu vifuatavyo;
kubadili oil & oil filter kila inapohitajika
kutembelea gear according to the speed & mzigo
Epuka mafundi wajanja wajanja wasio na uelewa wanaodhani kila kitu ni lazima kigongwe kwa nguvu
Don't mess with the carburattor hutaki pikipiki yako ile mafuta unataka ile ugali?
Katika periodic maintainance usisahau kukaza nuts & bolts, rublication sehemu mbalimbali pamoja na kucheck rubber bushings for wear & tear

IKIMBUKWE KUWA, Fundi wa kwanza ni wewe...wewe ndio unakijua chombo chako na hata ikitokea tofauti yoyote wewe ndo wa kwanza kulitambua hilo, kuna baadhi ya matatizo hata ukimpa chombo chako fundi atest hmas long as kinatembea, hawezi kugundua kirahisi bila wewe kumwambia na hakikisha fundi hawi mbishi (hii ndo shida ya mafundi).

IMG_20210115_183830_913.jpg
 
Hapo kwenye carburettor kila manufacture kuna jinsi ana set mchanganyiko kulingana na eneo alipo au eneo aliokusudia itumike ....utofauti wa usawa wa bahari sea level kwamba we uko mita ngap above sea level unaleta tofauti kwenye performance ya chombo husika ....perfomance ya piki piki kama hio moshi mjini where ipo just 800m -1000m above sea level na singida ambayo ipo mita 1300 hivi ni tofauti...... low air pressure

Kwa hio ukinunua ni ruksa kuiset namna unataka....mixture ikiwa too lean inakuwa na speed but less torque at lower rpm ..engine speed ikiwa too low performance inakuwa mbaya sana haswa ikiwa na mzigo...me three wheler yangu ..ina mafuta ya kutosha at lower rpm hata ukiwa na mzigo ni kama haisikii mchanganyiko mafuta yapo ya kutosha engine haifanyi kazi kubwa sana haipigi kelele hata ikiwa na mzigo gia hadi mliman unapanga no prob ina nguvu at lower rpm
 
Back
Top Bottom