2000 Toyota Land Cruiser VX 100 Diesel for Sell

sasa kwa nini hataki kusema mojakwa moja kua ni lexus, anaficha nini hii ni biashara kwa nini asiwe transparent. ok by the way hayo yoote uliyoyaeleza humu mi nayajua nilichotaka jamaa aweke uwazi zaidi. haya changamkia biashara hiyo, uwe na siku njema ndugu

Mkuu,

Hii gari sio Lexus. Na kama unajua magari utaijua lexus kwa kuiangalia tuu. Hii gari show ya mbele na nembo ndio lexus ndio maana nimekuambia njoo uangalie. Na ingekuwa lexus si ningesema kwanini nivishe? Kuna aibu gani gari kuwa Lexus.

Na uje uone registration zake.
 
Nilichokiona ni kwamba hii ilikuwa Lexus cygnus ya petrol hivyo kavua ingine kaweka ya vx 1HD Diesel bottom line.
Mkuu,

Hakuna kitu cha aina hiyo. Imenunuliwa UK na ipo hivo hivo ilivyo. Hakuna engine iliyobadilishwa unaweza kuja na fundi wako kuinspect.
 
Ngoja nimpigie sim Ray nimuulize ila Ya Kanumba kama kaishaiuza.
Maana wateja waliikimbia Lexus ile kwa kunywa mafuta mpaka yeye mwenyewe Ray ikawa inamshinda kutoka nayo.
 
ndio jamaa anataka kutuingiza chaka, Lexus yeye anaita toyota. umakini unatakiwa katika kutangaza biashara, hapo inaweza kuonekana kuna utapeli flani, hayo ni maoni yangu tu lakini

Kwani hujui kwanba Lexus ni kampuni dada ya Toyota?? Google huone..
 
ndio jamaa anataka kutuingiza chaka, Lexus yeye anaita toyota. umakini unatakiwa katika kutangaza biashara, hapo inaweza kuonekana kuna utapeli flani, hayo ni maoni yangu tu lakini

Jamani, kwani Lexus inahundwa na kampuni gani? Maoni yako kuhusu gari hayana ukweli wowote Lexus ni Toyota kama ilivyo Prado, Rav4, Krugger nk.
 
Mkuu,
Show wa mbele mtu unabadili kama unavyobadili rim. Ila hii ni VX sio lexus

Kama unataka nipigie nije kukuonesha

Mbona unatuchanganya, hiyo ni gari yako kweli au ni dalali mara useme ni Lexus mara useme hapana ni Toyota yaani mwenye mali hujui kama Lexus ni Toyota!!

Kitu kingine unasema grill ya mbele unabadirisha kama rim, mbona nembo ya nyuma inaonyesha ni Lexus au gari siyo ya kwako mkuu.
 
Vitu vyote hivo nilibadilisha mimi kutoka VX kwenda Lexus. Ni 'upgrade kit' ya Lexus. Inauzwa sets zote unatoa za VX unaweka Lexus. Ndicho kimetokea na Gari ni yangu. Sio dalali.

Ninajua Lexus na Toyota ni kitu kimoja. Naelewa Lexus ni luxury brand ya toyota. Utofauti wake upo kwenye comfortability. Sasa hii ni VX imewekwa Kits za Lexus. Naamini unanielewa sasa.

Ni kama vile mtu unabadili radio ya toyota na kuweka ya mini cooper. Au nembo ya altezza unaweka Lexus
 
Mkuu,

Hizo ni specification za gari. Maana yake ni turbocharged diesel engine. Ni mambo yanayoongeza ufanisi wa uendeshaji gari.
valves 24 maana yake turbocharged?

nadhani kwa mtumiaji maana yake engine kubwa kiufanisi, lakini pia inakunywa mafuta mengi kwa sababu ya ma valve mengi, ma cylinder sita. Lakini kwa diesel engine unywaji wa mafuta sio kuhofia sana kwa sababu ya uchomaji mafuta wa ufanisi zaidi kuliko gari ya petroli.
 
Upo sahihi kabisa. Asante.
 
We jamaa ni mbishi. Hapo unaona wanakwambia mechanically identical bado unabisha nini??na unazoziona mtaani sio zinataka kufanana na toyota. Ni identical. Just different brands kwa ajili ya masoko. Hata hiyo lexus ukiingalia ndani designs zote na spares ni toyota. Nenda marekani katafute altezza kama utapata. Zote ni lexus. Na sababu kubwa ni kodi,ni ngumu sana kwa makampuni ya kijapani kuimport gari marekani kwakua mmarekani anafavor kampuni za ndani. So magari wanayoyatengenezea ndani ya marekani au kuyaingiza marekani kwa agreement maalum na serikali wanayabrand upya. So american lexus=Japanese toyota. Umenisoma?

Sio kweli brother, Lexus sio American wala haikubuniwa kwa ajili ya mauzo ya Marekani, Lexus ni Japanese na ni luxury brand ya Toyota, kama ilivyo Infinity kwa Nissan
Pia sio kweli kwamba Marekani hakuna Toyota, kuna Lexus tu. Toyota ni moja kati ya Brand zinazouzika zaidi marekani. Mfano Toyota RAV4, CAMRY nk zipo za kumwaga karibu kila jiji la Marekani.
 
Wengi wa wachangiaji humu ni kujifanya ujuaji mwingi kumbe ovyo tu. Kama huna hiyo 35m piga tu kimya sio kubishabisha upuuzi.
 
Vitu vyote hivo nilibadilisha mimi kutoka VX kwenda Lexus. Ni 'upgrade kit' ya Lexus. Inauzwa sets zote unatoa za VX unaweka Lexus. Ndicho kimetokea na Gari ni yangu. Sio dalali.

Ninajua Lexus na Toyota ni kitu kimoja. Naelewa Lexus ni luxury brand ya toyota. Utofauti wake upo kwenye comfortability. Sasa hii ni VX imewekwa Kits za Lexus. Naamini unanielewa sasa.

Ni kama vile mtu unabadili radio ya toyota na kuweka ya mini cooper. Au nembo ya altezza unaweka Lexus

Unabishana na maskini wabishi jomba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom