1960: Vita za kutafuta nguvu, umafia na mikono itendayo miujiza

Jul 3, 2022
47
81
Kidokezo,

Wakati fulani nimekua nikijiuliza maswali magumu yenye majibu mepesi, na nimekua nikitoa majibu mepesi katika maswali yenye majibu magumu. Ni kwa sababu ni hulka yangu kufikiri na kuyatazama mambo kwa jicho la tatu na mlango wa sita wa fahamu.

Kiu ya binadamu mdadisi siku zote ni kutaka kujua kila jambo lenye utata linalojitokeza katika maisha yake ya kila siku.Aghalabu ndio maana leo hii Dunia inajiuliza baadhi ya maswali magumu.

Nani aliwaua Abraham Thomas Lincoln na John Fritzgerald Kennedy?

Nani alipanga mfanano wa miaka ya matukio hadi mauaji ya John Fritzgerald Kennedy na Abraham Thomas Lincoln?

Je, ni kweli Abraham Thomas Lincoln hakufa ila alipelekwa kuishi kwenye mahandaki ya siri huko Argentina?

Na Adolph Hitler je?
Vipi kuhusu Black budget pale USA?
Vipi kuhusu kitendawili cha JESUITS na BLACK POPE pale Vatican?

Mara nyingi jibu iepesi linalotajwa na wengi kuhusiana na maswali ya aina hii ni moja tu CONSPIRACY na Kuamini ni hadithi za kutungwa.

Aina hii ya maswali ndiyo ilinichochea kufatilia visa vya wanahabari wawili waliotikisa maslahi ya watu f'lani Africa na Marekani familia zao zikaishia kuomboleza.

Genesis.

Sometimes in Black African.

Usiku wa taeehe 27 November 2016, simu ya Mr.Robert Kimani iliita katikati ya usiku mzito wa giza la kifikra lililobeba kila aina ya alamu kumtahadharisha dhidi ya gari aina ya TOYOTA LAND CRUISER 200 SERIES V8 yenye namba ''MISS-711"ambalo lilikua likimundama kwa zaidi ya wiki mbili.

Naliita giza la kifikra kwa vile sijui ndio kujiamini sana kutokana na umahiri wake wa kupangua matukio kadhaa ya kumpokonya uhai au lah!?Sina hakika kama intelijnsia yake ilimuambia hakuna tishio lolote dhidi ya nafsi yake au ndio ule msemo wa siku yako ikifika imefika?Sijui kabisa ila ninachojua gari hii ilibeba hatma ya pumzi yake iliyokua ikiwindwa kutoka 2005 hadi wakati huo.

Kwa kipindi cha miaka 11 huyu bwana kupitia makala zake katika gazeti moja la The Investigator alikua akiwafumbua macho wananchi juu ya kile kilichokua kikiendelea chini ya kapeti ndani ya chama cha Constitutional Movement Unity (CMU), naweza kusema alichagua kuwa kiherehere kwa sababu kuu mbili.

1.Bias(upendeleo)
2.Kiinua mgongo

Ilifika wakati kipimo cha uvumilivu kilipungua na kuwalazimu wahusika kusafiri kiasi cha maili zaidi ya 1220 kumtafuta mtu atakaefanya kazi ambayo Idara nyeti ilishindwa kwa miaka hiyo 11 kiasi kwamba alinatizwa jina la utani na baadhi ya wapenzi wa makala zake na kumwita ''The mastermind" kutokana na kupangua matukio sita ya kupokonywa uhai.

Uandishi wa habari za kiuchunguzi haujawahi kua mwepesi kwa mwandishi huru asieegemea upande wowote au kwa yule aliegemea upande wenye maslahi nae, lakini hawa wote hua hawako salama.Hii inatokana na ukweli kwamba habari waandikazo hua ni tishio la maslahi ya wanaoandikwa.

Usiku huu ulikua na alamu zote kwa Bw.Robert Kimani kua roho yake iko mashakani lakini bado alipuuza ushauri wa mhariri wake wa kutoenda kuonana na Sheikh.Abdullah Mbarouk Shabaan katika hoteli hii.

Kuna nyakati nikifikiria nahisi Mhariri wake alikua na ABC ya nini kinaenda kumkuta mtendakazi wake ila hakutaka kumpa onyo la moja kwa moja akamuacha, nasema hivi kwa sababu siku zote anguko la mtu huletwa na watu wake wa karibu.

Wiki moja kabla ya usiku huo.

Narudi.......

Sehemu ya 02, post 13
Sehemu ya 03, post 30
Sehemu ya 04, post 37
................................................................
Mussa Daniel Mayagila
(iamindustrious)
There is story in everything
 
Ukirudi naomba uni-tag K11
 
1960:VITA YA KUTAFUTA NGUVU, UMAFIA NA MIKONO ITENDAYO MIUJIZA.

Sehemu ya 2.
........................

Wiki moja kabla ya usiku huo.

Dar es Salaam, Tanzania.

Mr.Robert Kimani aliwasili na ndege ya shirika la Ethiopian Airlines akitokea La Paz, Bolivia ambako alienda kukutana na faili No.711 ambalo yawezekana hakujua unteti wake uligusa maslahi ya makundi fulani ndani ya chama tawala Cha CMU.Kitu ambacho sina hakika kama alijua au hakujua ni kwamba alikua anavuka mstari wa uandishi wa habari kwenda upambe ambao hapa kwetu tunaita ''Uchawa" Naam mbaya zaidi hakujua unyeti wa faili hilo.

Ratiba yake ilikua sio kutua hapa amankwa lugha akrama ya kibantu cha nchi ya wanaopaswa kuondoa mashangazo nao wanashangaa!Ni kua hakua na safari yoyote ya kuja Dar es Salaam ila ndege ndiyo iliyolazimika kupita hapa kama ratiba yake ilivyokua.Hapa hawakukaa sana ikaruka na kuendelea kukata wingu na kupasua anga hadi Nairobi-Kenya.

Naam hapa ndipo ilikua mwisho wa safari yake!Lakini ujio wa hapa ulihusu ''Maokoto" f'lani aliyoahidiwa wakati akimnadi mtu fulani kule BLACK AFRICAN kwa wakati huo U$1Dollar ilikua ni Bshs.1760 na Senti kadhaa.Tuwekane sawa.Hapa wakati anapewa hiyo kazi ni 2005 kuelekea Januari 2006 ndio Dola ilikua na thamani hiyo, safari hii ya hapa ilikua ni 2016 yaani miaka 11 baadae.

Taarifa zinadai aliahidiwa kiasi cha U$D.300K ambayo kwa pesa ya kwao kwa wakati huo(2005) ni Black African shillings.528M.Naam ''NUSU BILIONI" na mpaka wakati huo 2016 anapotia maguu yake katika ardhi iliyoumeza mwili wa Dedan Kinathi, Jomo Kenyatta na wapiganaji wa Mzungu Aende Ulaya Mwafrika Apate Uhuru(MAUMAU) hii Dola 300K ilikua inacheza kwenye Bshs.858M yaani kwa kipindi cha miaka 11iliongezeka kiasi cha kama Bshs.330M kutokana na anguko la shillingi yao kulikoifanya Dola ipande thamani.Kwa vile makubaliano yao yalikua ni U$D.300K na miaka yote walimpiga danadana kumlipa yeye hakutaka kuelewa kitu alikomaa na kushikilia bomba anaitaka U$D.300K ambayo Sasa ilikua ni sawa na Bshs.858M.

Jamaa alikua na roho ya kichaga mbele ya mdaiwa sugu mwenye roho ya kikurya, hapa ndipo ramani ya vita ilipoanzia na mchori wa kumpeleka kibra ulikoanza kuchorwa na wakora walipewa gawio la Mwandishi wakalipiga na kumuacha mjini mbaya sasa aliyefanyiwa kazi(Mnufaika wa kazi ya Mr.Robert Kimani) alishavuka mstari wa mauti miezi kadhaa nyuma.Jamaa hakua na mtu wa kumdai zaidi ya dalali aliempa tenda hiyo maana alishapenyezewa kua mzigo ulitoka tangu February 2006 marehemu alipoukwaa kiti cha enzi.

Kwa hiyo safari hii ya hapa Nairobi alikuja kuonana na Adv.Kelvin Odhiambo wakili msomi kwa hapa kwetu mfananishe na ''Shangazi" najua utaniuliza kwa nini?Jibu ni kua Bw.Robert Kimani baada ya kuona halipwi halafu ana info gawio lake Kuna mtu analithibiti kibabe aliamua kumfata huyu wakili akamfungulie kesi mmliki wa kampuni ya UTOPIAN GENERAL ENTERPRISES & CO, LLC Bw.Rashid Marangwe ambae ndiye alimpa hiyo kazi.Wakili huyu alikua na mdomo wa moto haswa kwa lugha za skuli tunaeza mwita ''Mnoko" au ''Goroko" lakini ma Negro wanaweza mwita ''Snitch".

Nimemfananisha na ''Shangazi" kwa sababu kuu moja akiamua kukupika ukiingia kwa kumi na tisa zake halafu faili lako analo!Hutoboi.Halafu unajua pesa mwanaharamu aisee wakili alipoambiwa pesa inayotakiwa kutoka ni Bshs.858M na yeye akapewa kamisheni mzigo ukitoka tu anasepa na Bshs.330M kiroho safi.Wakili mizuka ikapanda akakusanya vitabu haraka sana akakwea pipa hadi Black African halafu toleo la The Investigator siku ya tarehe 20 November 2016 likatoka na habari ya ''BW.ROBERT KIMANI AMPELEKA MAHAKANI KIGOGO WA UTOPIAN"

Weee!!Huyu mmliki kuipata hiyo habari ikabidi amwite Bw.Kimani wayamalize kimya kimya maana kulikua na tenda ya serikali anaifukuzia ilikuwa na thamani ya Bshs.130Bilioni ilihusu ujenzi wa apartments.Sasa aikose Bshs.858M tu!?Tayari kashatoa kishika uchumba kwa wahusika na kilichosubiriwa ni kuweka sahihi TU mradi uanze halafu anaibuka huyu na kashfa za kutapeliwa, sikutaftana ubaya!?

Kitaalamu hii round Bw.Rashid Marangwe alikua hana namna ya kukwepa kumlipa maana alichotarajia kulipwa ni kikubwa lakini kinachoweza kumkosesha asilipwe zaidi ya Bshs.130Bilion ni kidogo mno.

Kikao lilikua cha moto!Bw.Rashid Marangwe alitaka kumlipa Ile Bshs.528M ambayo ndio pesa halisi ya dau la mwaka 2005 lakini Bw.Kimani alikomaa alipwe Bshs.858M ambayo ni sawa na U$D.300K kama walivyokubaliana mwaka 2005,Ilifika wakati wakaanza kutishiana maisha!Naam jasho la mkikuyu haliliwi kibwege halafu kumbuka huyu Bw.Robert Kimani alitoka La Paz, Bolibia kuliona ''faili No 711" hapa wakati anaongea tayari alikua na ABC za nini kitatokea siku chache zijazo na akamdokeza kwa maneno machache tu kuwa.

''Boss wa nchi anakuvuta kibrah akubutue, nipe Bshs.858M nikuuzie ramani ya vita usepe kabla hakijanuka!"

Kuna faulo zilifanyika 1998 katika vitabu vya wahasibu benki kuu ya BLACK AFRICAN, Kuna pesa ya kutakata ilichotwa!Hiyo pesa ilikua na mahusiano mazuri sana rafu za 2006 ambazo zote mbili Bw.Rashid Marangwe alihusika kama Play maker!Kuna watu walikua wanamtamani kuanzia yeye na mali zake, na hii info aliyopewa na Bw.Kimani alishanyetishwa kitambo ila hakujua anataka kubinywa korodani kwa ishu gani?Maana alikua mtu wa dili, na dili alizopiga hazihesabiki na alitaka kujua dili ipi inayotaka kumsweka nyuma ya nondo ili ajue anaipangua vipi.

Wakabishana sana mwisho wa siku akakubali yaishe akatoa mzigo wooote! Bshs.858M huu mzigo ukapita nchi tatu toka huko kusini hadi kisiwani.Watu wakagawana mpunga pale hoteli pendwa wakatawanyika kila mtu kivyake maana hadi kuupata kuna mhuni wa Kisiwani alihusika pakubwa akakatiwa kama TShs.102M hivi kama una makumbukumbu kuna tukio la ma-khaki kadhaa walilambwa vyuma nyakati ambazo ''UTAKATISHAJI PESA ilikua hoja kubwa sanaa Kisiwani mwaka huo!Naam wazee wa fursa waliona hili dili wakataka kupita nalo juu kwa juu waliona pesa yatima inaingia huku inatokea kule wasijue mziki ulianzia wapi?Wakadandia tu!Wakalambwa vyuma wakapotea kisa kutokutosheka na mishahara yao.

Pesa....pesa....pesa...pesaaaaa!!

Bw.Kelvin Odhiambo akavuta gawio lake Bshs.330M akasepa zake na Bw.Robert Kimani akabaki na kilichosalia akakipitisha alikokujua mpaka kikafika Kisiwani viherehere waliodhani kila fursa ya kupita nayo wakajimix kwenye ''Periodic table" wahuni wakawaundia ''chemical equation" wakajaaa haikuchukua round wakaanza ku-flow kuelekea makaburini.

Mimi nikajifunza kitu kimoja tu!''Sio kila anaevaa kanzu ni muislamu wengine ni wasabato"

TOGWA LIKAPATA NZI.

Unajua hili gazeti la The Investigator (code) pale Black African lilikua km Washington Post, Daily news, New York Times au The Guardian, lao!Lilisifika kwa kuandika habari nzito nzito na za moto lwelikweli kashfa!Ufisadi, wizi na madili ya maokoto.Na Mwandishi mkuu alikua ni Bw.Robert Kimani yaani alikua na habari nyeti na za uhakika kama Fabrizio Romano kwenye soka.Watu walimpenda na kumfuatilia zaidi kila toleo watu waliruka nalo hivyo huyu jamaa alikua ni kama Tupac vile alivyokua anawaingizia hela Death Row Records au Kanumba na kuinogesha Bongo movie kwenye kazi za Mtitu G na sound track zake za keep babe ''Nti! titi! tiii!" au Musa Banzi na movie zake kutisha.

Jamaa alikua analitengenezea hela gazeti hilo kwa siku lilikua linatengeneza zaidi ya nakala 100k kwa Bei ya Bshs.650 ambayo ni kama Bshs.65M lilikua linatoka kwa siku tatu kila wiki Jumatatu, Alhamis na Jumamosi kwa wiki ni Bshs.195M (65×3) kwa mwezi (195×4) ni kama Bshs.780M sasa ndio utajua huyu Bwana alikua na nguvu kupindukia hadi mabosi walimheshimu maana alikua ni pesa kwao.Kwa kifupi alikua ni Mwandishi wa maana japo alikua na certificate TU!Hapa ndio misemo ya ukiwaongoza class hakikisha unawaongoza na kwenye maisha!

Kuna story zinadai sijui alikua mjenzi huru, sijui alieangaziwa na nuru lakini mimi siziamini sana.

Sasa baada ya kupewa ile pesa yake akatambaruka zake! Huku nyuma akamuachia msala Bw.Rashid Marangwe.Kivipi?Ile habari ya kutaka kumfikisha bosi huyu mahakamani ilizagaa mitaani na raia wakataka kujua sakata lao linaendaje?Ni wakati huu pia Kuna vipenyo waliopewa kazi na bosi wa nchi walianza kuwaungia mikia wawili hawa kutaka kujua ilikuja kuwaje wakafikishana mahakamani!?Ili hali inafahamika walishiriki wote zile faulo za 2005 kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ubosi.

Hapa ndio inakuja pichani TOYOTA LAND CRUISER 200 SERIES V8 ikimlia doria Bw.Robert Kimani.Naam twende taratibu!Wakati anatua pale Kenya nilieleza ramani ya vita ndipo ilipoanzia kuchorwa mnakumbuka?

Naam huyu Bw.Robert Kimani alimfuata mafia mmoja wa Bolivia kwenye ulimwengu wa mihadarati anaitwa DON RUI ACOSTA ana miliki mashanba ya zao la coca linalotumika kutengeneza vilivyomuua Masogange baada ya kuonekana analeta nzi kwenye togwa la mabosi wake kutokana na kuandamwa sana na mamlaka, na vitu hivyo vilimsotesha kisutu ''last born" wa taifa.Naam wabongo wanaita ''Ngada" ana mashamba huko Cochabamba, chapare-Bolivia ni mtu wa kukurukakara sana na DEA wa USA inaaminika alikua anamuuzia sana Pablo Escobar hili zao, japo ni tetesi tu.

Alikutana na huyu bwana kama second plan endapo Bw.Rashid Marangwe ataleta UJUAJI amwagiwe vyuma!Maana alichoka kudai okoto lake toka 2006.Kwa kifupi aliwapa Mafia uhuru wa kumrudisha mavumbini Mzee wa Dili(Bw.Marangwe) .Kitu ambacho hakujua sasa!Maskini, huyu Mafia alishapewa amri za kumchabanga vyuma mwandishi huyu na mkora Bw.Rashid Marangwe.Usishtuke!Ni hivi alichoka kudaiwa na isitoshe pesa yenyewe alishakula Sasa kudaiwadaiwa akaona ni zaidi ya kero akaona amrudishe tu kwa muumba.Kwa lugha nyepesi huyu Mafia Don Rui Acosta alipewa tenda za mauaji kutoka kwa watu wawili bila wao kujuana kama waliuziana roho zao kwa Israel mmoja.

Kwa vipi ramani ya KIFO ilianzia hapa Nairobi!?

Kumbuka Bw.Robert Kimani aliuza roho ya mdeni wake kama second plan endapo akikataa kutoa pesa!Sasa mdeni si akatoa pesa?Pesa ilipotoka Don Rui Acosta akataka apewe japo kiramba mchuzi mkikuyu akakaza kamba kama mangi wa kichaga?Asijue Kuna mfungwa muhimu wa Don Rui Acosta Yuko nyuma ya nondo kisa makala zake gazetini.Kukataa kutoa kiramba mchuzi akawa kajivika kitanzi!Roho yake ikaanza kuwindwa!

Pesa pesa pesaaa!Mwanaharamu sana!

Sasa wale vipenyo katika nusanusa zao wakagundua kuna pesa ya kuoshea roho Bshs.858M ilitoka kwa Bw.Rashid Marangwe weeee!!Wakaanza kuichorea ramani waipate!Naam walijua Ile kesi ilihusu hayo maokoto na ndipo hapa wakaanza kumpigia doria Bw.Robert Kimani ilia wainyake hiyo pesa wasijue ni kwa vipi huyu mwandishi huwa anakwepa na kupangua mishale ya kunyang'anywa roho? Naam Mkikuyu alikua mkora!Wa chichini ukijirengesha anakulamba vyuma anatulia zake kona kumngoja mwingine alete unoko!Fuatana Fuatana weeeh!!Mara paap Kuna siku vipenyo kadhaa wakamvamia viwanja na kuntoa hadi ndani ya TOYOTA LAND CRUISER 200 SERIES V8 lao wakapukutisha 'U$D 5.7K" wale jamaa walipoenda kulala hawakuamka yaani walilala mazima.

Africanism religion in actions! Superstition is real vipenyo Waka gone to glory na kupumzika in everlasting peace.

Naam mizimu ikaondoka na roho za vipenyo sita waliogawana Ile U$D5700, tamaa ........tamaaaa.......tamaaa.Hapa sasa wakaingia kazini die-hard battle wao na yeye yeye na wao kisa Bshs.858M maadui waliokua na kiu ya roho yake wakaongezeka!Nilisema Bw.Rashid Marangwe aliachiwa msala eeh!?Baada ya kutoa Ile pesa Boss wa nchi nae akaamua kula nae sahani Moja kwa Dili la Bshs.130Bilion akalikosa, alipofikiria kashatoa Bshs.858M bila kupata alichohisi atakipoteza endapo hata toa pesa ya watu akapagawa!Hiyo haikua hoja kabisa hoja ni kwamba alipotoa Ile pesa Bw.Robert Kimani akamwambia Boss anakusakama sababu ''uliwahi kula pisi yake na kumtelekeza halafu ukampa vitisho" ilikua mwaka 2003 hiyo kipindi hicho Boss ni chawa tu!

Sasa kulikosa dili akafikia conclusion kua Bw.Robert Kimani alimnyetisha info wa kupika!Makusudi Ili hali akijua Boss anawainda dili hilo nae akaanza kumuwinda asijue; mwandishi alimdanganya Ile apate pesa yake!

Bw.Robert Kimani akapata maadui watatu
1. Vipenyo.
2.Bw.Rashid Marangwe.
3.Don Rui Acosta.

Yaani wiki moja akatengeneza maadui hatari 3 na bado akaendelea kudunda bila woga mkikuyu!?

Narudi
...............................................................
Mussa Daniel Mayagila
(iamindustrious)
There is story in everything
 
Back
Top Bottom