takashi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 905
- 188
Hii ni hoja na nilikwisha wahi kupambana na Prof. Ali Mazrui kupitia gazeti la Nation mwaka 1994. Hakuna sabsbu yoyote ile ya msingi kwa Zanzibar kuwa na wawakilishi wengi si tu katika bunge la muungano bali pia katika baraza la wawakilishi. Huu ni utapanyaji wa raslimali za nchi.
Hoja ya kuwa Zanzibar iwakilishwe kikamilifu katika bunge la muungano haiendani na kuwa na utitiri wa wabunge. Kwa kigezo kuwa mbunge wa kuchaguliwa awakilishe walau watu laki moja na nusu hadi mbili Zanzibar ilitakiwa iwe na wabunge sita. Ukilegeza kigezo hicho na kusema basi iwe na uwakilishi wa kutosha wabunge wake wasingezidi 20. Na kwa vile wanatokea katika sehemu moja ya muungano basi mamlaka yao kikatiba yangebakia yale yale kama yalivyoainishwa kwenye Katiba. Hivyo wanakuwa na uwakilishi unaofaa na nguvu kamili. Ikimaanisha kwamba kama muswada unatakiwa kupitishwa na idadi fulani ya wabunge kutoka Zanzibar basi idadi au asilimia hiyo inapatikana kutokana na wabunge hao wa Zanzibar. Sasa suala hili la kuwa na mbunge mmoja anawakilisha watu elfu nne ni kitu ambacho hakiingii akilini hata kidogo. Kama walitarajia kuwa Wazanzibar watanyamazishwa kwa kupendelewa na kuwa na watu wengi bungeni hilo wamenoa. Huwezi ukamnyamazisha watu kwa kuwapa upendeleo kwani kesho wale walioupata upendeleo huo wanaamini kabisa kuwa ule haukuwa upendeleo bali haki yao.
Kwa mfano hapo Marekani Jimbo dogo la Delaware lina mjumbe mmoja tu (idadi ya watu ni 885,000) katika Baraza la Wawakilishi. Na jimbo la Hawaii lina wawakilishi wawili wakiwawakilisha watu 1,295,000. Ni wazi kuwa kuna haja ya kupanga upya kabisa idadi ya wabunge kutoka Zanzibar. Vilevile kuna haja ya kuangalia majimbo mengine bara ambayo yalimegwa kwa ajili ya kuwalinda wanasiasa fulani na kukomoa vyama vya ushindani. Haya ni kama majimbo ya Hai na Sia pamoja na ya Singida Mashariki na Kaskazini. Ni lazima tuwe watu makini na tusitapanye pesa zetu kwa ajili ya kutaka kupata sifa au kuwatuliza watu fulani kwani kiu yao ya kupata zaidi haitakwisha.
waZanzibari wanataka serikali tatu je wewe unataka ngapi? huwezi kuwaamlia unavyotaka wewe...Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa hivyo... jiulize nani analazimisha Muungano? naomba jibu...