Naomba nikufahamishe kitu ndugu yangu, wanapokuambia kifurushi cha mwezi maana yake ni kwamba "expire date" yake ni baada ya siku 30. Kwa hivyo kama matumizi yako siyo makubwa unaweza kukitumia ndani ya muda huo, na kama ni makubwa unaweza kukimaliza hata ndani ya dakika 10.
Mi nachukia sana kuona wana JF wanachangia mada za udini, ubaguzi na chuki dhidi ya wengine. Haiko poa kabisa. Nawashauri wajifunze kupenda kila mtu kwa sababu hii dunia ni kubwa sana, hivyo huwezi jua ni nani siku moja atakuwa msaada kwako. Si ajabu, siku moja unaemchukia na kumbagua anakuja...
:A S-confused1: mamma yangu!!!!??? Hebu sikia hii; mwekezaji analipia eka moja ya ardhi Tsh. 220 kwa mwaka. Imekaaje hii wana JF?
Source: Bunge Jioni hii.
Mi airtel wananichanganya sasa, hizi bundle zao mpya wameweka MB chache kwa hela nyingi wakidai kwamba zina kasi zaidi. Mbona sioni tofauti yoyote na ile ya 400MB/2500Tsh, au ndo kuibiana kisayansi. Pia wanadai kwenye simu tunaongea kwa Tsh1/sek, ni uongo mtupu, tunalipia zaidi ya Tsh2/sek...
Wana JF, haya ni maajabu ya mussa, hivi kwenye dunia hii kuna mji unaitwa KAAMBOONI? Hebu angalia na wewe kwenye hiyo web waliyoorodhesha miji itakayoathirika na tsunami, labda nimesoma vibaya.
Huyu mama ni mpuuzi kabisa £/<@§:~{¤*#`¿ zake. Anaacha kutoa hoja binafsi kuhusu umeme, kupunguza foleni Dar, mfumko wa bei, watoto wanakwenda form 1 hawajui kusoma wala kuandika, wagonjwa 8 kitanda kimoja, air Tanzania, reli ya kati nk. anaongea ujinga huu. Hebu mzomeeni kwanza!!
:disapointed: Ndugu! bado unaumiza kichwa kuhusu Balali. Kibongobongo huyu mtu ameshakufa, hata akija leo serikali itasema "ni mzuka wake tu, wananchi msiogope"
Askari akiwa ndani ya sare anaruhusiwa kuipigia saluti maiti ya kiraia, kijeshi, hata ya mtoto mchanga. Ila huyo raia aliyevaa magwanda ya chama sijui amepata wapi authority ya kupiga saluti ya kiaskari. Akifanya tena, hebu mlete kwangu haraka sana nimfunze nidhamu. Sawa?
Hawa viongozi wetu mi hata siwaelewi. Hii inanikumbusha ileee... Obama kashinda urais, Kenya wakafanya sikukuu (hawakwenda kazini) wakati Marekani kwenyewe hawakuwa na muda wa kufanya upuuzi huo. What a shame!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.