Recent content by macho_mdiliko

  1. macho_mdiliko

    Kuna shida gani? Vijana wengi wanaohitimu wa kozi ya IT hawawezi kutengeneza website

    Gradute fresh kutoka shule hawezi kufanya project kubwa kwa usahihi. Siyo kwenye hii field tu, ni kazi zote. Hata pilot akimaliza mafunzo haingii moja kwa moja kufanya kazi peke yake, anakuwa chini ya mabingwa kwa muda fulani. Madaktari hivyo hivyo. Mainjinia hivyo hivyo.
  2. macho_mdiliko

    Kuna shida gani? Vijana wengi wanaohitimu wa kozi ya IT hawawezi kutengeneza website

    Haya mambo mwambie asome mwenyewe na asingojee mwalimu amtafunie kila kitu.
  3. macho_mdiliko

    Kuna shida gani? Vijana wengi wanaohitimu wa kozi ya IT hawawezi kutengeneza website

    Kwa nini unadhani mtu akisoma IT ni lazima ajue kutengeneza website kwa utaalam? Wewe ndiye mwenye tatizo. Information Technology ni field pana sana na unaweza ku-specialize kwenye mambo mengi. Kuna magwiji wengi wa IT ambao hawawezi kutengeneza website kwa kitaalam. Naona mawazo yako ni kama...
  4. macho_mdiliko

    Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu

    Jaribu kusoma kwa ufahamu. Kwanza mimi sihusiki kwenye kulipwa pension. Nilichosema nikuwa kama wanataka waanze mikataba mipya badala ya kubadilisha njiani. Ikianza mikataba mipya wale waajiriwa wapya watakuwa na nafasi ya kukubali mfumo wa pension ili waajiriwe au kukataa na kutoajiriwa. BTW...
  5. macho_mdiliko

    Makanisa yanaanza kutekwa na wanasiasa kwasababu ya fedha

    Mkuu nilikuwa nazungumzia kutekwa na wanasiasa. Hayo ya kutekwa na ibilisi sina ujuzi nayo ndugu yangu.
  6. macho_mdiliko

    Makanisa yanaanza kutekwa na wanasiasa kwasababu ya fedha

    Uko sahihi kabisa. Watumishi wa Mungu ambao ni feki siku hizi wako wengi mno. Nilishangaa sana kipindi cha Magufuli hata kanisa Katoliki lilikuwa limeingia kwenye mtego na kumfanya Magufuli kama ndiye mhubiri wa wakati wa Ibada.
  7. macho_mdiliko

    Makonda aamuru kukamatwa mara moja wezi wa millioni 478

    Nakubali. Haya ndiyo maisha ndani ya CCM. Makonda asitufanye wajinga. Yeye mwenyewe ni mpigaji mkubwa.
  8. macho_mdiliko

    Vijana tunaomba umri wa kustaafu uwe miaka 45 hiari na 55 lazima

    Ama kweli kua uyaone. Huzungumzii tatizo la ajira bali unapendekeza umri wa kustaafu uwe 45 ili vijana kupata nafasi!!!! Nilikuwa najua kuwa tuna tatizo la elimu ya kukariri lakini sikujua kuwa tatizo ni kubwa kiasi hiki!!
  9. macho_mdiliko

    Makanisa yanaanza kutekwa na wanasiasa kwasababu ya fedha

    Haya mambo yameshamiri sana kuanzia kipindi cha Magufuli. Nyuma ya hapo sikuwahi kuona nyumba za ibada zikitumiwa sana na wanasiasa.
  10. macho_mdiliko

    Vijana tunaomba umri wa kustaafu uwe miaka 45 hiari na 55 lazima

    Hizi ni kama akili za panya. Badala ya kutaka matatizo ya upatikana ajira yapatiwe ufumbuzi wewe unataka kuhamisha kutoka kwa vijana kwenda kwa umri wa kati. Tanzania elimu yetu inatufanya tusitafakari kidogo. Tatizo la ajira linatokana na uongozi mbovu wa CCM na siyo muda wa kustaafu.
  11. macho_mdiliko

    Nairobi Kenya: Mzungu apigwa kipigo Cha mbwa Koko na Security wa Petrol Station baada ya kumwita Nyani mhudumu wa kuuza mafuta

    Kuna video inasambaa ikionyesha mzungu akipigwa kwenye kituo cha mafuta ''Kenya''. Hii video ipo tangu mwaka 2020 na tukio lilisemwa kutokea South Africa.
  12. macho_mdiliko

    Sababu ya watu kuogopa kutoa ushahidi kwenye baadhi ya matukio aliyo shuhudia live na wengine baadhi hukimbia kabisa

    Mkasa wa kusikitisha unaoonyesha serikali iliyoshindwa kila kitu. Tatizo ni kuwa mtanzania ukimwambia tudai katiba mpya itakayotupa viongozi bora atakwambia ''katiba haileti chakula mezani''
  13. macho_mdiliko

    Kosa kubwa alilolifanya Hayati Magufuli ni kutokuelewa utofauti wa adui na mpinzani

    Haya wengi tuliyasema wakati akiwa hai, kwenye kilele cha urais wake. Tulimwambia aangalie sana, wapinzani wake kama kina Lissu, ni watu wanaompenda sana na wanaanika upungufu wake ili arekebishe. Tukamwambia maadui wake wakubwa wako CCM na wengi ni wale wanaomwimbia mapambio ya kumtukuza...
  14. macho_mdiliko

    Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

    Sikiliza: Mahakama ndiyo inaamua alipwe kiasi gani kulingana na uzito wa case. Kiwango alichotaja hakiwezi kukwamisha malipo iwapo atashinda kesi, sana sana mahakama inaweza kusema kiasi ni kikubwa hivyo kipungue.
  15. macho_mdiliko

    Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019

    Hii ni moja ya comment chache sana kwenye hii thread ''yenye akili''. Unaonekana wewe ni mtu ambaye uko well informed, educated na una exposure. Comments nyingine nyingi zimejaa ''uchafu wa ubongo'' wa kibongo-bongo. Yaani mambo seroius wanaleta mzaha au wanaonyesha chuki kwa mwathirika.
Back
Top Bottom