Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 734
Mabingwa wa soka nchini leo wamewanyuka mabingwa wa America ya kaskazini Vancouver white caps kwa mabao 3-0, kwenye uwanja wa Taifa. Mabao ya wababe hao wa jangwani yaliwekwa kimiani na Jerry Tegete mabao mawili na Mike Barasa bao moja. Ushindi huo ni dalili nzuri kabla ya kukipiga na Ally Alhy ama National ya Misri Ijumaa hii.
Dokezo; Team kama hii inafaa kweli kujipima nguvu na timu yetu ya taifa??
Mkuu taratibu....Hakuna sababu kucheza na Stars maana Yanga ni Imara zaidi katika ukanda huu wa Africa Mashariki!
Tumeshinda but it was nothing more than a runabout for the boys. Chuji did well, akihaha uwanja mzima huku akitoa mapande baabkubwa na watu wakimshangilia huku wakielekeza vifijo na nderemo kwa Maxio Maximo aliyekuwepo uwanjani.
Alivyoingia Ambani jukwaa kuu alishangiliwa sana - amerudi mchana leo akitokea to what it has been described as a successfull train in China.
Bring on Al Ahly!
Mara baada ya mchezo huo, mmoja wa wachezaji wa Whitecaps, Bellisomo Luca aliiambia Nifahamishe kuwa wamefungwa kwa sababu ya kuzidiwa na hali ya hewa ya joto ya jijini Dar es Salaam.
"Tumecheza chini ya kiwango, joto ni kali sana tofauti na tulivyozoea," alisema Luca mwenye asili ya Afrika.
Naye kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema; "(Vancouver Whitecaps) NI timu nzuri hasa kwa majaribio ya katika kipindi tulichopo"
Timu hiyo itacheza mwingine wa kirafiki na Simba, Machi 12 mwaka huu katika Uwanja huo kabla ya kucheza na timu ya taifa ‘Taifa Stars' Machi 14.
Source: Nifahamishe.com
Mkuu taratibu....
Mi nilidhani visingizio kama hivi huwa anatoa yule mnyama na wenzake kumbe mpaka hawa nao ... mhh yanga wanatisha
Yanga oyeeeeeeeeeee! Basi hiyo March 12th lazima mi-simba itakojolewa na hawa vibonde toka Canada....Yanga inatisha kama ukimwi!
Matusi hayo!. Yebo Yebo wameshinsa sababu jamaa walikuwa wachache toka dkk ya 3.
Huwa hawakosagi sababu hawa, Kwani kukubali Yanga wanatisha utaugua?
Flavio