Yanga yaichapa Vancouver White Caps

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Mabingwa wa soka nchini leo wamewanyuka mabingwa wa America ya kaskazini Vancouver white caps kwa mabao 3-0, kwenye uwanja wa Taifa. Mabao ya wababe hao wa jangwani yaliwekwa kimiani na Jerry Tegete mabao mawili na Mike Barasa bao moja. Ushindi huo ni dalili nzuri kabla ya kukipiga na Ally Alhy ama National ya Misri Ijumaa hii.

Dokezo; Team kama hii inafaa kweli kujipima nguvu na timu yetu ya taifa??
 
Hakuna sababu kucheza na Stars maana Yanga ni Imara zaidi katika ukanda huu wa Africa Mashariki!
 
Nawapongeza Yanga timu yangu ya Jangwani!!

Na bado mechi tatu tu za ushindi atawazwe bingwa ktkkt ya ligi!
 
Last edited:
MABAO mawili yaliyofungwa na Jerry Tegete katia dakika za 38 na 41 muda mfupi uliopita yameiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Vancouver Whitecaps ya Marekani katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Taifa

VANCOUVER Whitecaps, mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Marekani ya Kaskazini walikianza kipindi cha kwanza kwa ‘mkosi’ baada ya kiungo mshambuliaji wake Burgess Tyrell kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya tatu ya mchezo baada ya kumpiga ngumi Amir Maftah wa Yanga.

Tyrell alimpiga ngumi Maftah ikiwa ni kuonesha ishara ya kuchukizwa na kitendo cha beki huyo alichomchezea muda mfupi kabla.

Awali Yanga ilionekana kucheza kwa kuwasoma wapinzani wao ambao walionekana kudharau maamuzi ya mwamuzi katika sehemu kubwa ya mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.

Krosi safi ya kiungo mshambuliaji Shamte Ally iliyopigwa kutoka upande wa kulia wa Uwanja Taifa (Uwanja Mpya) katika dakika ya 38 ilimkuta Tegete akiwa katika nafasi nzuri na kuweza kufunga kirahisi, kabla ya kufunga Tegete alimpiga chenga kipa Nolly Doy.

Mpira ulioanzia kwa Nurdin Bakari kisha kumfikia Shardack Nsajigwa aliyepiga pasi safi kwa Tegete uliweza kuipatia Yanga bao la pili lililofungwa na Tegete katika dakika ya 41 ya mchezo huo, bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Mpira haukuweza kubadilika sana kipindi cha pili kama ilivyokuwa ikitarajiwa na watazamaji wachache waliojitokeza kushuhudia mchezo huo, lakini walikuwa ni Yanga waliopata bao la tatu katika dakika ya 51 lililofungwa na Mike Barasa baada yakazi nzuri ya Mwalala.

Mara baada ya mchezo huo, mmoja wa wachezaji wa Whitecaps, Bellisomo Luca aliiambia Nifahamishe kuwa wamefungwa kwa sababu ya kuzidiwa na hali ya hewa ya joto ya jijini Dar es Salaam.

“Tumecheza chini ya kiwango, joto ni kali sana tofauti na tulivyozoea,” alisema Luca mwenye asili ya Afrika.

Naye kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema; “(Vancouver Whitecaps) NI timu nzuri hasa kwa majaribio ya katika kipindi tulichopo”

Timu hiyo itacheza mwingine wa kirafiki na Simba, Machi 12 mwaka huu katika Uwanja huo kabla ya kucheza na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Machi 14.

Source: Nifahamishe.com
 
Tumeshinda but it was nothing more than a runabout for the boys. Chuji did well, akihaha uwanja mzima huku akitoa mapande baabkubwa na watu wakimshangilia huku wakielekeza vifijo na nderemo kwa Maxio Maximo aliyekuwepo uwanjani.

Alivyoingia Ambani jukwaa kuu alishangiliwa sana - amerudi mchana leo akitokea to what it has been described as a successfull train in China.

Bring on Al Ahly!
 
Ambani karudi,well hii ni habari njema kwangu
 
Mara baada ya mchezo huo, mmoja wa wachezaji wa Whitecaps, Bellisomo Luca aliiambia Nifahamishe kuwa wamefungwa kwa sababu ya kuzidiwa na hali ya hewa ya joto ya jijini Dar es Salaam.

"Tumecheza chini ya kiwango, joto ni kali sana tofauti na tulivyozoea," alisema Luca mwenye asili ya Afrika.

Naye kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema; "(Vancouver Whitecaps) NI timu nzuri hasa kwa majaribio ya katika kipindi tulichopo"

Timu hiyo itacheza mwingine wa kirafiki na Simba, Machi 12 mwaka huu katika Uwanja huo kabla ya kucheza na timu ya taifa ‘Taifa Stars' Machi 14.

Source: Nifahamishe.com

Mi nilidhani visingizio kama hivi huwa anatoa yule mnyama na wenzake kumbe mpaka hawa nao ... mhh yanga wanatisha
 
Mi nilidhani visingizio kama hivi huwa anatoa yule mnyama na wenzake kumbe mpaka hawa nao ... mhh yanga wanatisha

Na kweli wanatisha mwanawanii,Yanga Daima Mbele Nyuma Mwiko...Makamuzi yataendelea mpaka ndani ya Cairo...lol
 
Flavio

sinkala-albums-sinkala-picture354-flavio.jpg
 
Huwa hawakosagi sababu hawa, Kwani kukubali Yanga wanatisha utaugua?

Hongera Yanga kwa ushindi wa mabao 3, lakini mkumbuke hao jamaa walicheza muda mwingi wakiwa na upungufu wa mchezaji mmoja. Jitahidini ili mtutoe kimasomaso Misri, lakini muache matusi mkishinda.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom