Habari za muda huu wana JF, mimi ni mkazi wa mbezi (dar) takribani wiki ya tatu sasa naona magari ya abiria yanayosanya ruti za mbezi yamekuwa shida sana sio shida kuyapanda bali hayapiti kabisa na hivyo kusababisha msongamno wa watu wengi sana vituoni (athari zake zipo wazi sana sina haja ya kuzitaja) kwa mfano ijumaa iliyopita nimesimama dakika 50 nzima kusubiria gari la mbezi posta lakini halikupita mpk ikanibidi niunganishe magari mbezi-ubungo, ubungo posta.
Katika utafiti wangu mfupi nilioufanya nimegundua kwamba mainsource ya tatizo hili ni sumatra kivipi, mradi wa mabsi yaendayo kasi uanendelela (dart) hivyo ukikamilika utafanya yaje magari spesho ya kupita katika barabara hizo kwa hiyo magari ya sasa yanapaswa kubadilisha ruti, hivyo kama una gari lako la biashara katika barabara ya mororgoro leseni ikiisha wanakupa ya muda mpk mwezi wa sita mwakani kama serikali ilivyotangaza yenyewe, amabpo ndipo itakuwa mwisho kwa magari ya kawaida ktk barabra hiyo ,magari mengi yanashidwa kurenew mstari wake kwa kuwa sumatra wanataka cha juu kikubwa mno kuanzia laki 6 mpk laki 8 ili upate mstari mpya mpk mwezi wa sita mwakani kwa hiyo wamiliki wengi wa magari wanaona ni bora kubadilisha ruti hivyo kupelekea magari mengi ya mbezi posta kuwa haba, katika utafiti wangu huu huu nimegundua kwamba mabasi mengi ya yalikyokuwa yanasanya ruti hii ya mbezi yamehamishiwa ruti ya chalinze, kibaha na msata na machace ubungo tegeta.
Rai yangu
Serikali inapaswa ichukue hatua madhuti juu ya swala hili kwani wananchi tunaotegemea magari haya tunaumia mno kwa magari mengi kupungua ukizingati na foleni iliyopo kwa sasa hivi,najua watu mbali mbali na viongozi wa kiserikali wanapita jf ambao swala hili lipo ndani ya uwezo wao kulisolve ,ingawaje sijui kurenew mstari shilingi ngapi?
Ila kiasi cha liaki 6-laki 8 sio stahiki, fair wala reasonable just kwa miezi sita tu na kama wamililki wa magari wanazidi kuhama ruti serikali inapsawa kutafuta njia mbadala kutusaidia wakazi wa mbezi na tunaoutumia barabara ya morogoro.
Nafungua mjadala
Source: Mimi na madereva wa magari ya mbezi-posta, ubungo-chalize na msata