Na ndio shida iko hapio sasa, Ni kwa nini hao wanaouziana dagaa wa Kigoma hatuwaingizi kwenye mfumo, ili wote tufaidike? Nikimaanisha wao walipe kodi, Serikali ipate mapato, na iwarudishie huduma? Tatizo liko wapi? Afrika sio Kisiwa, hatuwezi kuishi kwa kanuni zetu pekee yetu, ni LAZIMA tufwate mfumo wa Dunia unavyokwenda, hatuna jinsi, kuna jamii nyingi pia walikuwa wanishi kama sisi na walikuwa na hiyo sekta isiyo rasmi kubwa tu, wakajifunza kutoka kwa wengine na wakafanikiwa kuboresha maisha yao!
Kwamba Afrika si kisiwa na inabidi twende na dunia ni suala jingine kabisa ambalo linahitaji mjadala mahsusi kama huu, bila shaka hata hapa tunaweza kuuchomeka kama sehemu ya mjadala huu.
Na kuna watu wataweza hata kukuambia kwamba mojawapo ya matatizo ya Africa ni kwamba imekuwa kisiwa kwa miaka mingi, kuanzia kijiografia . Na pale ambapo haijawa kisiwa, this has been to Africa's disadvantage (slavery, colonialism, neo-colonialism, unfair trade and unregulated globalization) .
Jared Diamond katika "Guns, Germs and Steel" kagusia jiografia, which is relevant to the island concept. Africa doesn't have the advantage of Eurasia, two continents bordering on a massive but penetrable land barrier in the Urals and even more penetrable further south by the various straits and passageways from the Caspian to the Dardanelles. That Africa, specifically Sub Saharan Africa, is literally a geographical island (if you count the Sahara as a sea of sand) cut off from the rest of the world until very recently, and that even with the advent of air travel and mass migration, we are yet to fully integrate in the world economy.
Nyerere mentioned this as a challenge to Sub Saharan Africa in one of his South to South commission speeches. Akasema wa Mexico wakiona mambo magumu watakimbilia Marekani, North Africans (ambao wengi hata hawajihesabu kama wa Africa, ila kama a "Middle-Easterners" wanaweza hata kuogelea mkondo wa Gibraltar kwenda Ulaya. Waafrika wa Malampaka je? Hata waogelee vipi hawavuki Kampala na Kisumu! Kwa hiyo inabidi wawe inventive na kujua kujitegemea.
Some would even go further and argue that Africa is more like visiwa ambavyo hata havifanyi biashara na kuwasiliana vya kutosha ndani yake. Unaweza kusafirisha kontena kutoka Dubai mpaka Mombasa kwa USD 1500 ukaambiwa kulisafirisha kutoka Mombasa mpaka Kampala ni USD 4500. Intertrade (formal albeit, we circle back) in Africa is below 15%, mostly around 10%. By comparison, in North America and Western Europe this is around 40-60%. Go figure.
Nilipotoa mfano wa dagaa Kigoma sio kama nasema tubaki hivyo na biashara informal. Nilikuwa naonyesha tu kwamba hizi habari za kutumia formal economy kupima zinaweza kuwa nzuri kwenye nchi zenye systems, lakini huku kwetu zikatuonyesha kwamba sisi ni masikini kuliko tulivyo.
Ukimwambia Mmarekani kwamba Afrika watu wanaishi kwa bajeti ya chini ya USD 2 kwa siku ataona hao ni masikini kuliko walivyo, simply because bajeti yake ya kula tu inaweza kuchukua USD 15 kwa siku. Kwa hiyo hafikirii Purchasing Power Parity, anafikiria dollar figure tu.
Tuko masikini, labda tunahitaji kujiuliza zaidi. Lakini mimi nafikiri maswala ya kiuchumi yatatatuliwa tu tukitatua masuala ya elimu kwanza.
Ili kusudi ukianza kumueleza mvuvi wa dagaa habari za umuhimu wa kulipa kodi akuelewe, na aweze kuifuatilia kodi yake imletee maendeleo.
Otherwise utamuingiza katika formal economy, utamtoza kodi na VAT. Kodi italiwa badala ya kuboresha huduma, na yeye kwa sababu analipa kodi za ajabu atashindwa kujikimu na biashara itakufilia mbali.
Formalization bila elimu inaweza kuua uchumi.
Ukitaka kujua chanzo cha umasikini Afrika angalia elimu.