Wenzetu wanatuacha katika hili la reli!

MtuKwao

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2006
Posts
268
Reaction score
73
Wakati nguvu zetu nyingi zimeelekezwa kwenye malumbano jinsi ya kugawana fito (Serikali 1, 2, 3 ..), mengine yanatupita.
Kenya, Uganda, Rwanda na S. Sudan wameanza kujenga Reli ambayo inatoa ushindani wa moja kwa moja kwa reli ya kati, bandari ya Dar es salaam na maslahi ya Tanzania kwa upana wake: mapato, ajira, kunusuru barabara na linkages nyinginezo katika uchumi!

Cha kusikitisha ni kwamba kwa nini hatujaona mpango kama huo wa kufufua reli ya Kati na kujenga zingine KWA VITENDO SIYO MANENO!

Tumwombe Mwakyembe aione hatari kwa uchumi wetu na atafute fedha kwa ajili ya ujenzi huu. Aende WB, AfDB, Ujerumani (ambao walijenga - nafikiri wangependa kuendelea kukumbukwa kwa hilo), huko China, Japan nk kupata mikopo ambayo nafikiri inalipika kwa sababu mapato ya reli na bandari ni mazuri na yataiwezesha TZ kulipa mikopo hiyo, hata ibikibidi kuwepo kwa rail toll. Ni nafasi ya Mwakyembe kufanya HILI MOJA TU, ujenzi wa reli hii standard gauge, high speed (at least 120 km/h), nchi hii imkumbuke kwa hilo kama ambavyo tutamkumbuka Magufuli kwa ujenzi wa barabara.

Plan B: Ikishindikana tunaweza ku-mobilise mikoa kuchangia rasilimali, ikiwa ni pamoja na kutoa nguvu kazi na wahandisi kusimamia kujenga reli hii kwa muda mfupi tu, kama ujenzi utafanyika vipande vipande bila hata kuchukua mkopo mkubwa. Naamini hili linawezekana, linahitaji tu uongozi!

TUANZE SASA!
======================================================





Source;BBC
 

Kama wanashindwa kutekeleza ahadi zao wenyewe unategemea nini? Ubadhirifu, Ufisadi, Rushwa, Madawa ya Kulevya, sasa wameanzisha sera ya kuwaingiza watoto wao kwenye mfumo wa utawala wa kichifu unategemea nini hapo? Hayo malori yao wanayofanyia biashara ya kusafirisha mafuta, makontena na mizigo kwenda kwenye migodi na nchi za jirani itapataje faida kama watakubali na kusimamia ujenzi wa Reli ya kisasa ambayo ni ya UMMA? Labda nayo waibinafshishe waichukue wao kama walivyochukua majumba ya umma na viwanda vya UMMA kwa bei cheee.... Hapa kwetu bila PEOPLES POWER usitegemee mabadiliko chanya..............
 
Nadnani bado wanafanya upembuzi yakinifu wa mchakato wa kumpata mkandarasi wa kupembua na kutathimini ulazima wa kuwa na reli, baranara au airport!, baada ya hapo sasa litakuja nani atajenga? na nani ale 10%.....hapo sasa wenzetu reli itakuwa tayari kisangani

 
Ushauri mzuri sana natamani ningekuwa kiongozi wa hii nchi. Nakuomba upeleke barua binafsi juu ya hili jambo kwa mwakyembe najua atafanyia kazi.
 
Hawa jamaa wanapiga bao sisi tumebakia watazamaji tu kwa sababu ya upuuzi wa watawala wa CCM.
 
Hivi unakumbuka bail Out ya 1.+ Tril kwa Ajili ya pamba?
Hivi hii walishahiriw ana nani?
Je hii haikutosha kujenga Reli?
 
Mbona na mwakyembe amefikia pazuri ktk hilo! au nyie mnafuatilia vya nje kuliko vya kwenu? au ndio nyie mnaofuatili ligi za nje kuliko za kwenu? hello hello Tanzania eneza upendo.


selfish
 
Wakati wenzetu wanajenga nguvu za kiuchumi sisi tunawaonesha nguvu za kijeshi ili kuwatishia. Huu ni ujinga! Tutabaki nyuma kama mkia wa mbwa milele huku tukijidai tuko imara na wakati huo huo rais wetu kila kukicha yuko safarini kutembeza bakuli la kuomba omba
 
Haiwezekani . Na wala hatuhitaji reli hivi mkuu atafanyabiashara ya malori saa ngapi nyie waTanzania vipi?
 
Mkuu, pamoja na kwamba japan wana mpango wa reli ya kati lkn nchi yenyewe kama nchi ni ngumu kuamua kuwa serious na mtandao wa reli nchini mana biashara ya usafirishaji ni ya kwetu, na dili za ujenzi na ukarabati wa barabara ni za kwetu. Huu ndio ukweli ulioghubika idara ya usafirishaji na ujenzi. Malori yetu yafanye kazi lkn pia barabara zivunjike tukarabati na kujenga. It will take time mkuu
 
Safi sana nimeiona hiyo kwenye BBC habari.Tumebaki na mipasho na matusi bugeni.Nampongeza Mheshimiwa Lugola kwa kujua Chama chake kinaendesha selikari KISANII.
 
Mbona na mwakyembe amefikia pazuri ktk hilo! au nyie mnafuatilia vya nje kuliko vya kwenu? au ndio nyie mnaofuatili ligi za nje kuliko za kwenu? hello hello Tanzania eneza upendo.

selfish

Ingekuwa vizuri ukapataja hapo pazuri palipofikiwa, tupate amani! Hello, Hello, endeleza Tanzania!
 
Kwamba mkataba wa kujenga bandari mpya Bagamoyo umesainiwa kati ya TZ na China ni jambo zuri. Cha ajabu na kusikitisha ni kwamba Bandari inahitaji reli nzuri na ya kisasa ambayo ujenzi wake haumo kwenye makubaliano yoyote mpaka sasa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…