Tumia Halotel ndio mtandao uliopo zaidi vijijini by the way vijijini ndani kabisa hakunaga mitandao mpaka uende sehemu Fulani....mfano nilikua kijiji cha Namhanga wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro. Eneo hilo la karibu na ofisi za kijiji hamna mtandao wowote unaopatikana wala Huduma sijui M-PESA hakuna. Inakulazimu kwenda umbali fulani kutafuta mtandao wa Airtel mingine haipatikani.
Mara nyingi porini hamnaga mtandao mawasiliano ya uhakika huwa ni radio call.. Ama simu zinazotumia satellite badala ya minara... Rediocall hutumika zaidi na vyombo vya ulinzi kama polisi kwa ajili ya kuhakikisha mawasiliano, ukienda mt.Kilimanjaro, Meru , mbugani nk. Kazi za namna hii nazipenda sana mkuu nipe connection