Watumiaji simu soma hii ~ Nomophobia

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,267
Reaction score
25,557
Nchi ya Singapore karibu kila raia anamiliki simu ya kisasa ya mkononi, raia huko ni milioni sita pekee.

Kwa sababu ya uraibu huu nchi imejenga kiliniki maalum ya kuwashugulikia walio na tatizo la Nomophobia, yaani kuipenda simu kupindukia. Mmoja anayepitia matibabu ya kuugua kwa kuikosa simu ni kijana wa miaka 19 wa Korea Kusini, Emma Yoon.

Amekua na tatizo hili tangu mwaka wa 2013. Anasema akikosa simu hasa kuisahau, moyo wake unaanza kupiga kwa kasi, anatokwa na kijasho, na hawezi kufikiria hadi aipate simu.
Imekua ni kama mmoja ya viungo vyake.

Wazazi wake wanasema penzi la simu alilonalo mwanao limeathiri maisha yake ikiwemo kushindwa kwenda shuleni wakati mwingine.
Lakini hofu sasa ni kwa watoto wachanga ambao pia nao
wamejipata kwenye uraibu huu.

Utawaona watoto wa miaka 10 wakishindwa kucheza na wenzao eti kwa sababu hana simu ya kuchat, simu siku hizi bara Asia inatumika kufanya kazi ya ziada
miongoni mwa wanafunzi ama ukipenda homework.

Ndio maana hata China wamefungua kiliniki yao ya kutibu
Nomophobia.
 
Duuuh!
Ko mkuu, ukitumia sana simu ndo unapata huo ugonjwa ama vepee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…