Bollo Yang
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 440
- 57
Leo kweli nimeamini Watanzania wanaweza kuwahi maofisini..hakuna cha anaepanda dala dala wala mwenye gari binafsi, watu wengi leo (Wa Dar) wamefika maofisini kabla ya saa moja asubuhi..mnaonaje wadau kama hii ndio ingekua kawaida....
Labda Bollo Yang huwa anaingia saa mbili leo kaona abadilishe ratiba iwe saa moja
wa tz tu wavivu sana na kupenda visingizio sana. Mfumo mzima ungekuwa km leo hata foleni zisingekuwepo, trafik wanawajibika ipasavyo. Kutoka mwenge mpaka morocco hakuna foleni barabara nyeupeeeeeeeeeeee
Hahahaha umeniwahi yaani leo saa kumi na moja asubuhi barabara zimechangamkaaa!! Duh ingekuwa hivi kila siku mbona tungekuwa mbali kimaendeleo!!
Haswaaa hili nalo swali. Maana imagine mtu anaingia ofisin saa tatu asubuhi anapiga blaa blaa hapo an anatunga safari hewa za kikazi, saa sita anakwenda lunch hadi saa nane anarudi kazini kusign off maana saa tisa anatoka ofcn (serikalini).Hivi takwimu za watanzania kufanya kazi ni masaa mangapi kwa siku,Isije kuwa tunadai mshahara bora kumbe utendaji ni masaa 3 kwa siku