Sidhani kama usomi ni kigezo cha kuwa kiongozi bora.Tanzania tuna viongozi bora ambao ni elimu ya ngumbaro.Lakini pia nitanabahishe kuwa wasomi wachache wanaipaka matope nchi yetu kwa ulafi binafsi na hulka ya wizi huku wakitumia mipenyo dhaifu iliyopo.Tukumbuke tulikuwa na mtu kama Dr.Tuntemeke Sanga,msomi lakini alikuwa na uchungu na nchi yake na mpaka anakufa alikuwa mtu wa kawaida sana.Tulikuwa na watu wasiokuwa wasomi lakini viongozi bora kama akina Kuwayawaya S.Kuwayawaya (Mb) na waliitumikia nchi kwa namna ya pekee sana na hawakuwa na tamaa hata kidogo.Kwa hiyo ulafi,wizi na hulka ya udanganyifu ni tabia tu ya mtu binafsi na kamwe hainakisi usomi au u-ngumbaro wa mtu.