Idd Ninga JF-Expert Member Joined Nov 18, 2012 Posts 5,539 Reaction score 4,854 Sep 1, 2020 #1 WASO NA MAONO,WATAWACHAGUA Naam Haina ubishi,hao Wasojitambua Wasojielewa Waso na maono. Tuseme tu Ndio wao,viherere Barabarani,na vikengele Vigelele,wapiga makofi Tutawachagua. Tena Kwa mara nyingine Tuwape ulaji Wale,wanenepe Si ndio. Hivyo Tena,hivyo hivyo Ndivyo tunataka,tumelogwa Tena mchawi,amekufa Labda kwa ngoma,ama Corona Tuna balaa. Watachagua Waso na akili Hawana malengo,limradi Siku ziende Mahohehahe Wasobadilika Kila siku wale wale Wanaogopa Wakijitisha Watetemeka. Watawachagua Ili tuteseke,tutaabike Sisi na wao,wao si sisi Waso na maono,ndio mikosi Tufanye nini. Tuamueni Tuwatoeni,tuwatimue Watukimbie,walikotoka Tumewachoka ? Hatuwataki. Kweli Waso na maono Watawachagua Watowachagua Hawana maono. Idd Ninga Arusha +255624010160 iddyallyninga@gmail.com
WASO NA MAONO,WATAWACHAGUA Naam Haina ubishi,hao Wasojitambua Wasojielewa Waso na maono. Tuseme tu Ndio wao,viherere Barabarani,na vikengele Vigelele,wapiga makofi Tutawachagua. Tena Kwa mara nyingine Tuwape ulaji Wale,wanenepe Si ndio. Hivyo Tena,hivyo hivyo Ndivyo tunataka,tumelogwa Tena mchawi,amekufa Labda kwa ngoma,ama Corona Tuna balaa. Watachagua Waso na akili Hawana malengo,limradi Siku ziende Mahohehahe Wasobadilika Kila siku wale wale Wanaogopa Wakijitisha Watetemeka. Watawachagua Ili tuteseke,tutaabike Sisi na wao,wao si sisi Waso na maono,ndio mikosi Tufanye nini. Tuamueni Tuwatoeni,tuwatimue Watukimbie,walikotoka Tumewachoka ? Hatuwataki. Kweli Waso na maono Watawachagua Watowachagua Hawana maono. Idd Ninga Arusha +255624010160 iddyallyninga@gmail.com