Tatizo wamekariri, kwao wao maana ya mabadiliko ni kuitoa CCM madarakani. Siyo kosa lao ila ndivyo walivyokaririshwa na wagombea wa vyama vyao.
Ushauri wangu tu ni kwamba waanze kujifunza nini maana ya mabadiliko ya kweli, kisha wajifunze ni kiongozi gani anaweza kuleta mabadiliko ya kweli. kisha wazisome tena ilani za wagombea wote na wawasikilize wagombea wanapohutubia bila ushabiki wowote na wafanye maamuzi kwa kuingalia Tanzania ya miaka 10 ijayo...
Kama utafanya hivo utagundua wazi kuwa Rais anayetufaa kututoa hapa tulipo na kutupeleka mbele ni John Pombe Magufuli... Mimi, wewe na yule tumpe kura zetu