Wasafi wanahamia CCM, wachafu wanahamia CHADEMA

Maswa utahangaika sana lakini hakuna aliye msafi humo CCM!!. Hata huyo unaemwamini chunguza vizuri wizara alizopitia na ndio zinaongoza kwa kupata hati chafu toka kwa Auditor General. Unaona huku ukijisaulisha!! Tukuiteje?! ZWAZWA SIO

Leo kina Change na wenzie wako huko, hamsemi kitu!! Wakihama kwa sababu yoyote mtaanza kupiga mhwano!! UPUUZI. Leo kina Masha kurudi CCM wamekuwa wasafi?!
 
Zamani ndiyo ilikuwa hivyo siyo sasa
Kwani mtu kama Lazaro kahamia lini au kwako zamani umamaanisha nini?

Mimi nafikiri ungesema wachafu wote wakishasafishwa na chadema basi ni ruksa kurudi kwao ccm yaani wale wote waliofuata ujazo wa matumbo yao na sio mapinduzi ya fikra.
 
Masha ana tuhuma gani ya ufisadi kama lowasa?
 
Waliotangaza kuwa Nyarandu ni fisadi ni chadema hao hao
 
Masha ana tuhuma gani ya ufisadi kama lowasa?
Huyu aliyeshindwa ku deliver akiwa serikalini na hata alipokuwa upinzani!!!. Huyu alienda kuombewa po na mzazi wake asiendelee kuuza nyumba za mzee?!!
 
Kwa maana hiyo CCM ni dubwasha la kupika watu wachafu wakati Chadema ni kiwanda cha kutengeneza watu safi wenye maadili mazuri.
Hiyo ilikuwa zamani.. Sasa hivi thubutuuu
 
Cha kushangaza ni kuwa hao majizi,wala rushwa n.k hawajawahi kutiwa hatiani.
 
Jiandaeni kumpokea Chenge msafishe
 
Wangapi waliopokea viroba vya hela ya mboga wapo CCM, au ufisadi wao utaanza wakiwa nje ya CCM, hao hatuwaongelei,tuwe 'fair' tunapojadili mstakabali wa nchi ,wapo waluotajwa meli zao kusafirisha meno ya ndovu hatuwazungumzii kabisa.
 
Hao hao wakihamia chadema wanapokewa kwa shangwe
 
Chadema ni kama Mugabe!!Mugabe kaponzwa na mke wake na kutosikia kwake!!chadema inaponzwa na Mbowe!! Halafu huwa nafurahi sana chadema inaposema wanaohama eti wamenunuliwa!!safi sana!!
 
Kwa upande wa wanachama wanaohamia CCM kuanzia Masha, Mkumbo, Mwigamba, Katambi wote ni wasafi na hawana hata tone la ufisadi wala matumizi mabaya ya madaraka kama wale wanaotoka CCM na kwenda CHADEMA!
kwa kuwa hao nao wameelekea kunako wachafu ni muda tu nao watakuwa takataka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…