Maruku Vanila umenigusa, Ruberts na Bigaraone nimewapata. Mimi natokea Jimbo la Nkenge na mbunge wa jimbo langu anatokea CCM na anaitwa Mhe. Asumpta Nshunju. Pamoja na wabunge wengine wa mkoa wa Kagera naamini ujumbe wetu kupitia JF ama wanausoma au watapewa na wasaidizi wao. Mimi ninamtumia Waraka Mhe. Asumpta Nshunju nasema hivi; Mhe, wananchi wa jimbo la Nkenge walikuamini wakaweka tumaini lao kwako. Wewe pia uliwaahidi kuwa utashughulikia kero zao zote na utakuwa nao bega kwa bega. Nao wana Nkenge wakakupa jukumu hilo kwa kumnyang'anya kijiti DR Kamala wakaweka tumaini lao kwako. Sasa elewa kero za wananchi wa Nkenge zimezidi na kwa uchache kwa sasa wanakabiliwa na ukosefu wa madawa wewe unafahamu kuwa pale Mugana DDH, Bunazi Hosp, Kashasha HC,Igayaza HC, Bugandika Disp n.k vifaa tiba ni tatizo na sasa limeongelewa Bungeni, tatizo la mnyauko wa migomba linazidi kutamalaki nawe hujashughulikia huku ukijua kuwa ndizi ndo chakula chetu kikuu, ujenzi wa shule za sekondari za kata umedoda majengo yamekuwa mapagala na wewe uko kimya. Matatizo ni mengi na yanazidi kila kukicha. Sasa ni wakati muafaka kwa wewe kudhihirisha kwamba ama wananchi wa Jimbo la Nkenge walikosea kukuchagua kuwa Mbunge wao au basi hawakukosea nawe uko pamoja nao hivyo shiriki kikamilifu kuwawajibisha viongozi wazembe na mafisadi. Vinginevyo, mimi sitasubiri mwaka 2015, nitaanza sasa hivi, nitaongea na ndugu, marafiki na majirani na wana Nkenge kuwa sasa utufai. Kimsingi tunafuatilia yote yanayoendelea Bungeni na hata utumishi wako tangu uwe Mbunge.