Pendekezo langu ni kwa mamlaka zinazohusika kukomesha hili jambo kwanza kwa kuyashika magari yanaoshwa hayo maeneo,na kutoa faini kubwa kwa kufanya hivyo naamini hakuna mtu atakayepeleka gari lake lioshwe hapo na waosha magari watakosa magari ya kuyaosha.
Mwisho tunawaomba wenye magari jamani hayo magari mnaweza kuoshea majumbani kwenu au sehemu maalumu za kuogesha,tutunze barabara zetu na mazingira kwani wenye magari ndio mtakuwa watu wa kwanza kulalamika barabara ikianza kuwa kama mashimo ya Tora bora au Kandahar
Kutokua na ajira sio maanake ndio uvunje sheria,kila mtu akidai afanye anavyotaka kwa kisingizio cha ajira ndio mwanzo wa watu kufanya mambo ya hovyo hovyo basi itabidi,je itakuwa sawa kwa mfano mtu afunge Ng'ombe wake pale mjini Posta eti kwa kisingizio cha kujipatia kipato,na tujalibu kulinganisha mambo je ni lipi jema watu wagongwe na magari au barabara ziharibike au waosha magari waendelea na shughuli zao/ kwa hakika ni upuuzi kusema waosha magari wabaki kisa wanapata mkate,Unadhani hao vijana ajira yao itakapo kufa watafanya kazi gani ingali hawana elimu? Ninge kuona wa maana sana kama unge sema watafutiwe maeneo maalumu ili wafanyie kazi zao hapo...
Hawa vijana inawezekana hapo mwanzoni kabla ya kujiajiri na hiyo kazi ya uoshaji wa magari walikuwa vibaka, na sasa wame ondokana na hiyo kazi wameamua kujiajiri wenyewe ili kujikimu kimaisha...
Hawa vijana wanapata pesa yao nzuri sana kwa gari moja wanaosha wa tsh 2000 n a kwa siku wana weza kuosha hadi gari 5 kwa mtu mmoja,
mtaani kwangu kuna sehemu hawa vijana wanaosha magari na mimi huwa na waunga mkono kwa kupeleka gari langu pale wanioshee,maana hao vijana ni wa mtaani kwangu.
Na cha kushangaza kuna car wash hapo hapo hao vijana wanapo osha magari kwa maji machafu na wateja wengi wanakimbilia kwa hawa vijana na car wash imefungwa kwa kukosa wateja.