Wanyama na tabia za binadamu

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Habari zenu wandugu!

Mimi leo nilitaka tujadili kuhusu tabia zetu Binaadamu kwa kulinganisha na tabia za Wanyama. na jinsi tabia zinavyoharibu maendeleo katika jamii zetu, kama vile familia, vikundi vidogo vyenye lengo fulani zuri tu la maendeleo. Tabia ni kama ngozi huwa ni ngumu kubadilika, mara nyingi tumekua tukiwakimbia watu wenye tabia tofauti na tulizo nazo, tunashindwa kufanya kazi nao kwasababu hatufanani tabia zetu matokeo yake malengo yetu yanavunjika.
Wafuatao ni baadhi tu ya Wanyama na tabia zao, ambazo Mimi na wanaJF tunazo na wakti mwingine ni vikwazo kwa watu wanaotuzunguka.Ni vema ujijue wewe upo kwenye kundi lipi kati ya makundi haya ya wanyama na tabia zao,Ikiwezekana na ubadilike kabisa.
Twende kazi!

1.
PUNDA: anaposema "Siendi" haendi hata umpige na gogo la mbuyu. kuna watu ambao waking'ang'ania wazo moja hata aambiwe ukweli aje, habadilishi wazo lake.
2: SIMBA: Huyu ni mgomvi" watu wenye tabia za simba wapo tayari kupigana kwa vyovyote vile na yeyote yule anayeingilia mipango ama matakwa yao.
3: SUNGURA: yeye ni kutimua Mbio tu. Watu wenye tabia ya Sungura siku zote hawatatui tatizo, wakiona ugomvi ama vuguvugu la ugomvi linataka kutokea haraka sana wanabadilisha maada. Hawa ni waoga

4: NYANI: Anapumbaza na Mcheshi, Mara nyingi watu wenye tabia za nyani huwa wanapenda kuwa wachekeshaji sana na wanapumbaza wenzao pale wanapokua wanafanya mambo muhimu.

5: NYOKA: Huyu huwa anapenda kujificha kwenye nyasi na huruka ghafla na kung'ata. Wapo watu wenye tabia kama za nyoka, Mara nyingi huwa wanakaa kimya kwa muda mrefu wakati jamii fulani ikiwa inashiriki kufanya jambo, lakini endapo wakisema jambo moja tu huaribu kila kitu kinachoendelea.

6: KOBE: Huyu upenda kujiingiza ndani ya nyumba yake endapo mazingira hayapo shwari, na hujitoa anapohisi hali imekua shwari nje. Wapo watu watabia kama za kobe, hupenda kujitoa kwenye jamii ama kundi endapo kuna matatizo, hawatoi mchango wowote ule, kama wa mawazo, pengine wangependa jamii isifahamu kama wapo ndani ya hiyo jamii ili wasisumbuliwe kabisa.

7: TEMBO: Anatabia ya kuangusha miti barabarani, na kuzui njia ili chochote kisipite hadi atakapo amua yeye. Wapo Ndugu zetu wenye hizi tabia, wanakua wasumbumbufu, wababe huzuia kundi kuendelea na shuguli zake kufikia malengo yaliyopangwa.

8: MBUNI: Huona kila kitu kipo sawa wakati wote, hawafikiri kama kuna tatizo kamwe. Wapo watu wenye tabia kama za Mbuni, mara nyingi huinamisha kichwa chake kwenye mchanga, hukataa kabisa kukubali kama kuna matatizo.
 
Umesahau wenye tabia ya nguchiro kutukana msasi akiona shimo
 
umesahau vinyonga wanabadilika badilika leo wako ukawa kesho wako bungeni
 
Leo ndio nimejua kua Mbuni ni mnyama zamani nilijua mbuni ni ndege.]

Ndege ni wanyama!
Wanyama wamegawanyika katika makundi mengi.
KUNA mammalia[ambao wengi ndio hudhani ni wanyama],
Aves[ndege],
reptilia[jamii ya mijusi],amphibia[jamii ya vyura],
Samaki n.k.
Pia kuna wasio na uti wa mgongo kama panzi,inzi,minyoo,sisimizi n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…