salaam kwa wote jaman,,,
mim ni ke jaman,nna mpnz wang wa mda mrefu na najua ananipenda nami nampenda but kuna kitu kinanipa mawazo wadau,mi nna kaz na mpnz wang ana kaz but anawaza kuiacha sabab hawampi salary yake.
no.1,mpnz wang anataka nimwambie kila pesa navyotumia yani hata kununua nguo,kusuka niseme,na anataka tuunganishe pesa tufanye biashara pamoja,mh,na wasiwasi nae kwa kweli!!!.
no,2,mwakani alipanga aje kwetu kuposa na badae mahari,lakini mpnz wang hana kaz ya uhakika yan ofisini kwao wanakaa hata miezi minne hawapew mshahara na wala hawawajali.sasa ataweza kweli kutoa hiyo mahari au tusubili had apate kazi ya uhakika hata kidogo.but yey analazimisha kwamba lazima afanye sa nawaza akishindwa si tutaaibika jamani.nifanyeje??
inamaana uamifu na upendo wako kwake uko shakani sababu halipwi mshahara?
kwani anavyosisitiza kupeleka mahari we umeshamuuliza hela atatoa wapi? labda kuna akiba ameweka. Ongea nae taratibu uje. kama anatarajia we umpe hapo ndo litakuwa janga. Au labda mwenzio anaogopa utamuacha maana amefulia ndo maana anataka akuwahi kabla mabazazi yenye hela hayajagundua. Mhakikishie usalama.
Kitendo cha kudhibiti hela zako ni kuwa kujiamini kwake kama mwanaume kumepungua kutokana na kukosa kipato. Hapo usimlegezee lakini tumia hekima. Si kitendo kizuri kutumia mabavu kwenye hela za mwenzio ingawa ni vizuri wenza kuwa wawazi kwenye mambo ya hela. Ingawa hamjaoana bado, dalili za mvua ni mawingu. Kama una hakika ni mpenzi wako wa siku nyingi na mnapendana basi huu ni upepo unapita, tulieni. Cha msingi msiharakishe kuposana. Malizeni kwanza haya matatizo yaliyopo: namna ya ku-handle maswala ya hela zake, zako na zenu. Hili ni muhimu sana kwani limevunja ndoa nyingi. Hilo swala la kuunganisha hela mfanye biashara sioni kama ni tatizo kama litafanyika mkiwa ndoani na baada ya makubaliano. We ndo unamjua mtu wako, ila tunashauriwa kutokufanya maamuzi hasa maamuzi magumu tukiwa na mashaka.
Kama Unawaza Sana Pesa Basi Hakuna Mapenz Ya Kweli Apo