Mkuu wangu
COPPER, mie nashangazwa na kitu kimoja tu na hii shule! Wakati sie tunasoma secondary, kati kati ya miaka ya 90, Mzizima walikuwa wanatuburuza ile mbaya hapa Dar!! Yaani jamaa walikuwa hawafai, walikuwa wanapiga paper kwa sifa! Nakumbuka kulikuwa na mtoto mmoja wa kidosi(msichana) alikuwa kama fido dido aisee!! Lakini huyu fidodido alikuwa mwanaharamu.....alituburuza kwenye mock na national, bila kujisikia haya!!
Sincerly, nilizani hii shule siku hizi haipo! Mdogo wangu akanihakikishia kwamba bado ipo! Pamoja na kunielekeza hadi physical address ya pale ilipo(ilibidi afanye hivi coz' niliamini haifahamu) lakini bado sikutaka kuamini kabisa!! Nikaamua siku moja niingie NECTA website ili niitafute kwenye matokeo! NIKAIKUTA! Sio siri, HADI LEO SIJAAMINI! Zile One za Kupenda sifa hazipo tena! Hata hizo Division Two, ni adimu! Miongoni mwa wakali wao 2012(form IV results) wana Three! Matokeo yao 2012 haya hapa: DIV-I=0, II=2, III=2, IV=20, FLD=6 !!! Wamekumbwa na nini hawa watu?! Hii sio Mzizima ninayoifahamu mimi....ile miaka ya 90(especially mid 1990s), hapa DSM, piga ua, Mzizima inakuwa Top zingine ndo zinafuata!