Duh! Afande Fusi mnamkumbuka na unoko wake? Mie nilikuwa Operation Kambarage. Afande Balua na Omari walivyokuwa wanoko wanatukwepesha ndege. Kablasi na punda wake na alivyokuwa anajitafutia misifa.
Mkuu zile 'lokoo' ulizikwepa vipi? Wako akina dada walikuwa wanalala kwenye mahanga ya wanaume wawahi lokoo, ukichelewa ilikuwa ni kifo. Tulikuwa tunakwenda Kwa Msanga weekend kubadilisha mlo, chakula maarufu ilikuwa mihogo na kuku wa kienyeji kishushio chai ya rangi. Genda Genda the untold stories of migunga..
It sounds like ndie huyo, atakuwa alihamia Oljoro baada ya kuondoka Mgambo. Nikiwa mgambo kuna kuruta walikuwa wanaletwa toka Oljoro kuja Mgambo JKT kama adhabu. Jamaa alisomea Israeli na alikuwa anatembeza ukomandoo kikosini. Kuna stori moja pale mgambo kuruta walitoroka shamba wakajichimbia kwenye kichaka wanakula machungwa jamaa akawazukia na kuwarusha kichura hadi kikosini.
wee muhengaUkweli wale tulikuwa nao Mgambo 1978 - 79 (Operation "USHINDI") tuwasiliane. Mimi nilikuwa Kombania "B" nawakumbuka afande Anthony, Mkombozi, nk.
Mimi nilikutana na Mtono Malale JKT, dash we acha tu!Mimi sikuwa Mgambo ila hili jina la Mtono linanikumbusha afande mmoja kule Oljoro JKT alikuwa anaitwa Ali Mtono, kama ndo huyo basi jamaa alikuwa nuksi kishenzi miaka hiyo ya 1989/90 operation Program ya chama.